Acha uzushi na siku nyingine usilete upuuzi kama huu hapa.Kama imekutokea wewe usidhani kila anayevaa pambo hili ni mmoja wa hao wako waliokutokea.
Kwa faida yako na wengineo, huwezi kumsoma mtu kitabia kwa jinsi alivyojipamba. Udhaniaye ndiye basi utakuta siye and vice versa. Kuna wengine wana fikra mbaya au potofu na hawa wanaposikia "tetesi" basi hawakawii kuanza kusema ni "ushahidi".
Katika kila jamii hapakosekani watu wenye mitindo ya maisha iliyo nje ya kawaida.Watu kama hawa hawawezi kutofautishwa na wengine kwa maana ya mavazi au mapambo.Inapotokea wanaonekana nao wamejipamba kama " wengine" basi wenye akili finyu hurukia kutoa tafsiri ambazo hazipo kama mnavyosema hapa.Kwa taarifa yenu vikuku, vishaufu, hereni ( hata wanaume huvaa siku hizi) za masikio na hata sehemu nyingine za mwili ni pambo tu linaloweza kuvaliwa na mtu yeyote bila kutangaza chochote.
Hatuwezi kuacha kuvaa mapambo yetu ati kwa vile kuna watu wachache wasiojua, wanaeneza tetesi na uvumi.......