Ni ruhusa kwa Wanawake wote wanaojisikia kuvaa cheni miguu yote au mguu mmoja kufanya hivyo. Cheni hizi zimeanza kuvaliwa na Wanawake sehemu mbali mbali duniani miaka mingi tu lakini miaka ya karibuni urembo huu umependwa sana na Wanawake wengi na hivyo kuwa maarufu zaidi. Wanaotaka kusema yale wanayoyafikiria kuhusu cheni hizo waacheni wafurahishe nafsi zao lakini ukweli unabaki pale pale kwamba ni urembo tu na hakuna maana nyingine yoyote ile. Mwanamke akivaa cheni shingoni ni urembo, akivaa mkononi ni urembo, akivaa kiunoni ni urembo lakini akivaa mguuni/miguuni tu KOSA!!! Miguu miwili anacheza kote kote, mguu wa kulia/kushoto sijui upuuzi gani! hahahahahaha LOL! Kazi kweli kweli!