Nimezaliwa katika family ya kifugaji
Maisha yangu ilikuwa ni uchungaji kama sehemu ya maisha halisi ya jamii yangu ilionizunguka
Kadri umri wangu ulivyo ongezeka ndivyo nilivyo anza kutamani mambo mbalimbali kulingana na rika langu
Vijana wengi wa rika langu walipendelea kuvaa shanga shingoni mwao huku zikitafautiana na shanga zilizo valiwa na wamama watu wazima na mabinti waliokuwa wanachipukia
Sikuwahi kufahamu chimbuko la utamaduni huu wa uvaaji wa Shanga wapi ilikuwa ni chimbuko lake katika jamii yangu
Naamini wengi tulivaa kama fashion kulingana na utashi tuliokuwa nao
Shanga zilivaliwa sehem mbalimbali katika mwili wengine Shingoni, Wengine miguuni, Wengine walizivaa kiunoni hasa watoto wakike..
Lakini thamani ya shanga nilikuja kuiona pale nilipofika mjini kwa Mara yakwanza nakuongozana na mjomba katika Ibada ya mkesha wa pasaka siku hiyo nilijisikia furaha sana pindi Shemasi alipokuwa anainua rozari juu kama ishara ya msalaba kilicho nitia furaha moyoni ni pale nilipogundua kuwa rozari ilikuwa imetengenezwa kwa Shanga..
Kadri siku nilizoishi mjini nilianza kugundua kuwa watu wa mjini walikuwa hawavai shanga kwenye miili yao kama sisi wa kijijini lakini wao walizipa majina shanga zile na zikawa na hadhi kuliko zakwetu
Shanga hizi za mjini ziliitwa rozari kwa wafasi wa Masihi na wafasi wa mkweli muaminifu wao kumbe waliziita Tasbihi..
Uhusiano wa shanga na mwanadamu haukuishia misikitini na makanisani pekee Bali hata watu waliosadiki kutokuwepo kwa Mungu nao walitumia Shanga kutambika
Kumekuwepo na aina nyingi za shanga kulingana na kipato chako ndivyo na thamani ya Shanga itakavyo kuwa
Kuna Shanga zitokanazo na Vito vya thamani kama Tanzanite. Amathisit, Agate, Moonstone, Diamond, na Ruby pamoja na dhahabu..
Lakini pia kuna shanga zitokanazo na prastic na mifuko ya railoni
Hizi zote ni shanga
Wataalaam hutengeneza bidhaa hizi kufatana na mahitaji ya Wateja Shanga ambazo hutumika ktk Ibada zipo hutengenezewa aina ya fulani ya kuzitambulisha kuwa ni Shanga za Imani gani..
Hizi siku hizi huvishwa hata vyombo vya usafiri kama magari utazikuta zimeninginia kwenye site Millar ya seats ya dreva. Kama dreva muislam utaangalia Shanga ipi kaivalisha gari yake
Pia kama mkristo nae utaangalia aina ya shanga kwenye gari lake..
Nimekuwa nikijiuliza huu utamaduni wa Shanga na mwanadamu hasa muafrica ulianza karne gani na kuna mahusiano gani kati ya mungu na Shanga katika kumuabudu au pia kuna mahusiano gani kati ya Shanga na Urembo? Au Shanga na mapenzi?
Mimi bado sina majibu tusaidiane....