DOKEZO URGENT: Binti wa miaka 16 ameozeshwa kwa lazima kama mke wa pili, huko Laela, Sumbawanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ahsanteni sana Wadau wa JF kwa taarifa hii. Huu ndiyo ushirikiano wa jamii tunaohitaji. Tunashughulikia. Ahsanteni kwa mawasiliano ya namba ya simu.
Piga kazi mheshimiwa! Huyo binti atakuwa anatoka familia za kifugaji (Wasukuma) wanaozesha sana mabinti wadogo.
 
Shukran mheshimiwa kwa kulichukua hili
 
Kwani sheria ya ndoa ya serikali ya Tanzania inasemaje kuhusu ndoa kama wazazi wa binti wa miaka zaidi ya 14 wameridhia aolewe? Serikali si ilishindwa kwenye kesi ya Rebecca Gyumi kupinga ndoa za utotoni serikali ikakata Rufani ikashindwa tena ikashauriwa irekebishe sheria hiyo ya ndoa lakini mpaka hakuna muswada wowote wa wa mabadiliko ya hiyo sheria ya ndoa uliofikishwa bungeni.

Kama serikali haipendi hizo ndoa za utotoni kwanini walikata rufani waliposhindwa mahakamani na Rebecca Gyumi? Haya mnayotuambia hapa ni maigizo tu,kama kweli serikali inadhamira ya dhati a basi hiyo sheria ya binti wa miaka 14 kuolewa ibadilishwe mara moja vinginevyo serikali ikae kimya tu
 
Hapo shida sio umri pekee, shida ni kwamba binti mwenyewe hajaridhia na hayuko tayari kuolewa!
 
Asante sana mh waziri kwa wepesi wako wa kuzingatia matatizo ya wtz kwa haraka. Mungu akubariki sana.
 
Habari za jioni ndugu yangu katika JMT. Nadhani utakuwa umefuatilia mrejesho wa serikali kuhusu hoja uliyoleta. Mara kadhaa kumekuwa na mrejesho kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali juu ya ajenda hii. Hata hivyo, sidhani kama ni sahihi kutotoa msaada na ushirikiano kwa hoja iliyopo sasa dhidi ya manusura ambaye anahitaji msaada kwamba, tukae kimya tu kwa kuwa bado ile hoja ya awali haijafikia mwisho.

Sidhani kama kukaa kimya bila msaada ni sahihi. Hivyo, Kila jambo tutafanyia kazi katika kudhibiti ukatili wa kijinsia kulingana na lilivyo sasa kwa mazingira ya Sasa na wakati ujao nao utafanya kazi kwa mazingira ya wakati huo. Tumeshampata mtoa taarifa Ili kumsaidia manusura wetu. Ahsante Sana, ubarikiwe. usiku mwema,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…