Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Mhhh...ni juzi tu nimegundua kuwa mpenzi wangu ana U.T.I....sikuwa na uelewa mkubwa sana so nikaona nihabarike zaidi wikipedia ndo nikakutana na hiyo habari kuwa U.T.I ni rahisi sana kuwapata wenye ujauzito na isipotibiwa vizuri ikaisha kwa mama wajazito inaweza kusababisha pre-mature birth(kuzaa njiti) na disabilties nyinginezo kwa huyo mtoto...hivyo ushauri wangu kwako ni vema uhakikisheunalitibu kwa kina hilo tatizo lako haraka iwezekanavyo...

Cha pili naomba nisaidiwe hapa jamani kama mpenzi wangu ana U.T.I namimi ntakosa kweli???....na madhara yake ni nini kwa wanaume??
 
mhhh...ni juzi tu nimegundua kuwa mpenzi wangu ana u.t.i....sikuwa na uelewa mkubwa sana so nikaona nihabarike zaidi wikipedia ndo nikakutana na hiyo habari kuwa u.t.i ni rahisi sana kuwapata wenye ujauzito na isipotibiwa vizuri ikaisha kwa mama wajazito inaweza kusababisha pre-mature birth(kuzaa njiti) na disabilties nyinginezo kwa huyo mtoto...hivyo ushauri wangu kwako ni vema uhakikisheunalitibu kwa kina hilo tatizo lako haraka iwezekanavyo...

Cha pili naomba nisaidiwe hapa jamani kama mpenzi wangu ana u.t.i namimi ntakosa kweli???....na madhara yake ni nini kwa wanaume??

u.t.i haiambukizi jamani
 
u.t.i haiambukizi jamani

Sasa kama haiambukizi kwanini kwenye zile causal factor na sexual intercourse imejumuishwa??...alafu ye alipofika hospitali akaulizwa una mpenzi??? Unamwamini??...mara ya mwisho ulikutana naye lini??...hauna mimba wewe???....haya ni baadhi tu ya maswali aliyoulizwa....sasa nachanganyikiwa ukinambia haiambukizi
 
Nina tatizo hili la UTI kujirudia mara kwa mara naomben msaada wa matibabu kwa kina kwan nimetibiwa huu mwaka unaisha lakin kila nikipima tena inaonekana ipo japokuwa dalili zake hupungua kwa mara ya kwanza nilikua nakojoa mara kwa mara, maumiv wakat wa kukojoa, maumivu chini ya kitovu, homa lakin kadri mda unavozid kwenda dalili hizo zimepotea ila ugonjwa haujaisha nin tatizo wajamen ukizingatia kipind hichi ni mjamzito je ugonjwa huu utaniletea matatizo kwa mtoto atakae zaliwa??????

Kwanza napenda ujue kuwa UTI ni very common kwa mama mjamzito lakini pia inaonyesha hata kabla ya kupata ujauzito haukuwahi kutibiwa vizuri. Nakushauri uende kwa daktari na umweleze historia ya ugonjwa huo toka mwanzo. Kuna vipimo utakavyofanya na kupewa dawa kulingana na majibu ya vipimo. Wakati mwingine kwa akina mama wajawazito watu huwa wanachanganya kukojoa mara kwa mara na dalili za ugonjwa wa UTI. Kukojoa kwa mara kwa mara kwa mama mjamzito kunaweza kusababishwa na kukandamizwa kwa kibofu cha mkojo na huo ujauzito!
 
Sasa kama haiambukizi kwanini kwenye zile causal factor na sexual intercourse imejumuishwa??...alafu ye alipofika hospitali akaulizwa una mpenzi??? Unamwamini??...mara ya mwisho ulikutana naye lini??...hauna mimba wewe???....haya ni baadhi tu ya maswali aliyoulizwa....sasa nachanganyikiwa ukinambia haiambukizi

yap ni lazima aulizwe hayo maswali kwa sababu yanahusiana na ugonjwa wenyewe ila mimi nilikutana na specialist wa magonjwa ya kike akaniambia kwamba huu ugonjwa hauambukizwi sasa na mimi inanipa confusion
 
u.t.i haiambukizi jamani
Hii ilikua niimani ya kizamani kwamba U.T.I. haiambukizwi au mwanaume habati U.T.I. lakini recently, imekuja kugundulika kwamba inaambukiza kwahiyo akiwanayo mmoja tu katika sexual network basi wote shuruti mtibiwe, vinginevyo itakua haiondoki na inaweza ikawa sugu na kukusababishia matatizo ya kutokushika mimba kwa mwanamke au kutoshikisha mimba kwa mwanaume. Kama haupo kwenye mahusiano, sana sana kwa wanawake, basi ni kuhakikisha tu kwamba mazingira ya huko (kwaukweli) yanakua makavu usiwepo unyevu unyevu hasa wakati wa joto.
 
asante kwa elimu
 
Asante kwa ushauri...nitamwona dakrari kwa usalama zaidi
 
Sasa kama haiambukizi kwanini kwenye zile causal factor na sexual intercourse imejumuishwa??...alafu ye alipofika hospitali akaulizwa una mpenzi??? Unamwamini??...mara ya mwisho ulikutana naye lini??...hauna mimba wewe???....haya ni baadhi tu ya maswali aliyoulizwa....sasa nachanganyikiwa ukinambia haiambukizi

UTi haiambukizwi kwa njia ya ngono!

Ila kwa huwa njia ya mkojo kwa akina mama ni fupi sana, bacteria ni rahisi kupanda (ascend) kwenda kwenye kibofu na hivyo kisababisha UTI kwa wepesi kiliko wanaume!

Suala la kujamiiana linakuja pale ambapo, kwa kuwa magonjwa ya zinaa dalili zinatokea kwa uchache kwa akinamama kulinganisha na wanaume basi hiyo ascending infection inaweza kuwa imetokana na ama ugonjwa wa zinaa ama wadudu walio normal flora katika maeneo yanayozunguka njia ya mkojo!
 
Nina tatizo hili la UTI kujirudia mara kwa mara naomben msaada wa matibabu kwa kina kwan nimetibiwa huu mwaka unaisha lakin kila nikipima tena inaonekana ipo japokuwa dalili zake hupungua kwa mara ya kwanza nilikua nakojoa mara kwa mara, maumiv wakat wa kukojoa, maumivu chini ya kitovu, homa lakin kadri mda unavozid kwenda dalili hizo zimepotea ila ugonjwa haujaisha nin tatizo wajamen ukizingatia kipind hichi ni mjamzito je ugonjwa huu utaniletea matatizo kwa mtoto atakae zaliwa??????

Unapimwa kipimo gani kuambiwa una uti?
unaposema dalili zimeisha ila unakua bado na ugonjwa una maana gan?
unakunywa dawa gani kujitibu?
ujauzito uko umri gan?
 
MziziMkavu eti ni kwanini hiyo hapo juu
mate pia sio mazuri wakati wa shughuli..!! tukiachilia mbali unywaji wa maji ya kutosha kusafisha chumvichumvi kwenye figo,na usafi wa kutawaza na kinasa/pichu< ajitahidi kupata hewa wakati mwingine kama ni mnene oxygen inahitajika kunako kinanilii..Pia kama anakaa muda mrefu bila kupata tendo kuna aina ya normal flora wanakuwa pathogens wakipata PH Fulani...ajitahidi kuwa na wakati wa kuhudumia maeneo hayo kila mara au mpenzi wake amsaidie kama yeye yupo busy. asante.
 
Nenda hospitali wafanye culture and sensivity watajua utatibika na dawa gani bila hivyo utakuwa unapewa dawa kwa kubahatisha.
 
MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO.

UTI_240.jpg

Tuliangalia maana ya Urinary Tract Infection (UTI), aina za ugonjwa huo na dalili za awali anazoonesha mgonjwa wa UTI.

UTI husababishwa na bakteria waitwao Escherichia Coli na Staphylococcus Saprophyticus ambao huathiri mfumo mzima wa mkojo. Tuliona pia kuwa aina kuu mbili za ugonjwa huu kutegemea na mahali palipoathiriwa. Aina ya kwanza ni Acute Cystitis

ambapo kibofu cha mkojo hushambuliwa na aina ya pili ni Pyelonephritis ambapo figo ndiyo hushambuliwa na bakteria wa ugonjwa huu.

Dalili za awali tuliona kuwa ni kuhisi haja ndogo mara kwa mara, sambamba na maumivu makali wakati wa kujisaidia haja ndogo,

kukojoa mkojo mchafu, wenye rangi ya njano, ukiwa umechanganyikana na usaha (Dysuria), maumivu ya tumbo, kutokwa na

uchafu unaotoa harufu kali, kushindwa kukojoa, licha ya kubanwa na haja ndogo na homa kali.

Kwa watoto, dalili kama mwili kuchemka, kutapika, kulia mara kwa mara, maumivu ya tumbo, kupoteza hamu ya kula na kuishiwa

nguvu ni miongoni mwa dalili za ugonjwa huu.

Leo tunaendelea na sehemu ya pili ambapo kwa pamoja tunachambua namna unavyoweza kupata ugonjwa huu.

Ngono zembe
Kwa vijana wadogo wanaopitia kipindi cha mpito kuelekea utu uzima, tendo la ngono zembe linatajwa kusababisha maambukizi katika njia ya mkojo kwa asilimia 75- 90. Si kwa vijana pekee, hata watu wazima nao hupata ugonjwa huu kwa kufanya ngono bila

tahadhari. Hii ni kwa sababu Escherichia Coli hupatikana kirahisi kwenye viungo vya uzazi.

Sababu za kimaumbile

Wanawake wanatajwa kuwa wepesi wa kuambukizwa UTI kutokana na maumbile ya viungo vyao vya uzazi. Kwa kuwa wanapotaka kwenda haja ndogo ni lazima wachuchumae, mkojo hugonga kwenye kuta na sakafu za choo na kubeba uchafu wenye

bakteria wasababishao UTI kisha kugusana na sehemu za siri ambapo uambukizo huanzia hapo. Matumizi ya vyoo visivyofanyiwa usafi wa uhakika, huwaathiri wanawake kwa kiasi kikubwa.
Upasuaji wa njia ya haja ndogo (Catheterization)

Kwa wale wenye matatizo ya kibofu ambao hulazimika kufanyiwa upasuaji wa kuwasaidia kupata haja ndogo kwa kutumia mipira maalum (Urinary Catheterization), wapo kwenye hatari kubwa ya kupata

maambukizi ikiwa upasuaji hautafanyikwa kwa umakini wa kutosha.
Matumizi ya pedi zisizo na ubora
Wanawake wanapokuwa katika siku zao za mzunguko wa hedhi, endapo watatumia pedi (sanitary pads)

zisizo na ubora au ambazo muda wake wa matumizi umekwisha, wanaweza kupata maambukizi haya. Pia wale ambao hawana uwezo wa kununua pedi na badala yake hutumia vitambaa, kama hawatazingatia usafi ikiwa ni pamoja na kuanika juani na kupiga pasi, nao huwa katika hatari kubwa ya kupata maambukizo.

MATIBABU

Ugonjwa wa UTI hutibiwa kulingana na hatua uliyofikia. Endapo mgonjwa atawahi mapema hospitali baada

ya kuanza kuona dalili za awali, matibabu yake yatakuwa rahisi kuliko mgonjwa atakayechelewa kwani

maambukizi yatakuwa yamepanda na kufika kwenye figo, jambo ambalo ni hatari kiafya.

Baada ya kupimwa na daktari, mgonjwa atapewa dawa za Antibiotics ambazo kama zitatumika kiufasaha

kwa kufuata dozi, atapona ndani ya siku chache. Aina ya dawa atakazopewa mgonjwa zitategemeana na

vigezo vya daktari ikiwa ni pamoja na umri , uzito, afya na historia ya mgonjwa.

Ikiwa mgonjwa atachelewa kwenda hospitali na ugonjwa kusambaa sehemu kubwa, matibabu yake yatakuwa

magumu ambapo ataandikiwa dozi kubwa za dawa atakazotumia kwa siku nyingi ili kupona. Dozi hizo

zinaweza kuwa mchanganyiko wa Antibiotics zaidi ya moja na dawa za aina nyingine.

MUHIMU:
Ikiwa mgonjwa atachelewa sana kwenda hospitali, atapatwa na hatari ya kuharibika kwa viungo vya ndani

vya uzazi, hali inayoweza kusababisha ugumba au utasa hasa kama mirija ya mfumo wa uzazi itaathiriwa.

Unashauriwa kuwahi hospitali mara unapoona dalili zisizo za kawaida katika mfumo wa mkojo badala ya kununua dawa na kunywa bila kupimwa.

NAMNA YA KUJIKINGA

Kwa kuwa tulishajadili jinsi unavyoweza kupatwa na UTI, namna ya kujikinga ni kuepukana na visababishi vya ugonjwa huu.

1. Epuka kufanya mapenzi bila kinga kwani tulishaona kuwa ngono zembe inachangiakwa kiasi kikubwa tatizo hili kwani bakteria wa E. Coli wanaosababisha ugonjwa huu wanapatikana kwa wingi kwenye viungo vya uzazi.

2. Usafi wa vyoo na mabafu
Kama tulivyoona kwamba sababu za kimaumbile nazo zinachangia kwa kiasi kikubwa, inashauriwa kuwa vyoo hasa wanavyotumia wanawake, visafishwe kwa dawa ya kuua wadudu (disinfectant) ili kuwaepusha na hatari ya kupata maambukizi.

3. Kuishi kwa misingi ya afya bora
Watu wanashauriwa kuishi kwa kufuata kanuni za afya bora ili kuepukana na maradhi ya kibofu au figo yanayoweza kulazimu mtu kufanyiwa upasuaji na kuingizwa mipira ya kusaidia kupata haja ndogo (catheterization).

4. Pia wanawake wanashauriwa kutumia pedi (sanitary pads) zenye ubora na ambazo muda wake wa matumizi haujaisha.

5. Maziwa ya mama yanasaidia kuzuia maambukizi ya ugonjwa huu kwa watoto hivyo akina mama wanashauriwa kutowakatisha kunyonya watoto katika umri mdogo.

6.
Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.

TIBA MBADALA YA MARADHI YA (UTI) PATA MAFUTA YA KHARDALI KUNYWA KIJIKO KIMOJA ASUBUHI KIJIKO KIMOJA MCHANA NA KIJIKO KIMOJA USIKU KWA MUDA WA SIKU 3 AU S&#304;KU 7 KISHA NENDA KAPIME HAYO MARADHI YAKO YA (UTI) UTAKUTA HAKUNA TENA INSHALLAH.

318px-Mustard_oil.JPG

MAFUTA YA KHARDALI KWA KIINGEREZA YANAITWA MUSTARD OIL.

Dawa ingine ya kutibu Maradhi ya UTI ni hi hapa kwa jina inaitwa Grape seed extract

pGNC1-2331338t300x300.jpg

Mustard oils for UTI treatment

Mustard oils derived from horseradish root and the nasturtium herb can be used as treatment for UTI, according to a 2006 study published in the Arzneimittel-Forschung journal. The study found that a combination of extracts from

horseradish and nasturtium, two plants from the mustard family containing volatile mustard oils as the

active ingredients, demonstrated antimicrobial properties, meaning they kill or inhibit the growth of

microorganisms like bacteria. Researchers stated that the combination of these two supplements is a rational treatment for UTI and upper respiratory infections.

In a similar study published in the
Arzneimittel-Forschung journal that same year, participants took either antibiotics or an herbal drug combining horseradish and nasturtium. The group who took the antibiotics

experienced a 87.9 percent decrease in symptoms versus 81.2 percent in patients who took the herbal drug.

However, researchers found that the herbal drug had a clear advantage because the participants taking the supplement needed fewer supportive procedures and administration of concurrent medication.

Grapeseed extract

Grapeseed extract may also be an effective treatment for UTI and other infections. The supplement promotes activity to fight bacteria that are causes of urinary tract infections.

Grapeseed extract also has antifungal and antiviral properties to treat infections caused by fungi or viruses.
The University of Maryland Medical Center recommends taking 100 milligram capsules or five to 10 drops of liquid grapeseed extract three times a day for treating infections.

UTi haiambukizwi kwa njia ya ngono!

Ila kwa huwa njia ya mkojo kwa akina mama ni fupi sana, bacteria ni rahisi kupanda (ascend) kwenda kwenye kibofu na hivyo kisababisha UTI kwa wepesi kiliko wanaume!

Suala la kujamiiana linakuja pale ambapo, kwa kuwa magonjwa ya zinaa dalili zinatokea kwa uchache kwa akinamama kulinganisha na wanaume basi hiyo ascending infection inaweza kuwa imetokana na ama ugonjwa wa zinaa ama wadudu walio normal flora katika maeneo yanayozunguka njia ya mkojo!

Shukrani kwako mkuu
 
Dr. asante kwa maelezo
mate, unamaana ya mdomoni au yale ya kuondoa msuguano......

Back
Top Bottom