Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Urinary Tract Infection (UTI): Chanzo, Dalili na Kinga/Tiba yake

Mimi nina mtoto wa kiume, hakuwahi kuugua UTI kwasababu nilimtahiri akiwa na miezi 2 tu. Hakikisha anapooga msikalishe kwenye maji kwa sababu kuna wakati anayakojolea, msimzoeshe kuvaa pempers wakati wote. Kwa umri aliofika mjaribisheni kuvaa kaptura nyepesi.
 
Wazazi wa siku hizi wanavalisha pampers watoto hata wanaoongea. Sijui toilet training itafanyika lini.? Ndo maana uti kwa watoto haziishi. Nakumbuka wakati mdogo mama alikuwa anatuweka katikati ya miguu yake na kutuambia tunye. Basi tulikuwa tunajisikia raha hata kama hujabanwa unamwambia, mama kunya! Ili tu akupakate kwenye miguu yake kwa stail ya kunya.
 
Wandugu jambo?
Ktk familia yetu kuna watu 3 wanasumbuliwa sana na hii UTI. Tumeenda kwa hospitali ila hakuna ahueni.

Please, ajuae dawa yake au kinga anihabarishe tuokoe kizazi hiki.
Barikiwa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wandugu jambo?
Ktk familia yetu kuna watu 3 wanasumbuliwa sana na hii UTI. Tumeenda kwa hospitali ila hakuna ahueni.

Please, ajuae dawa yake au kinga anihabarishe tuokoe kizazi hiki.
Barikiwa!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Pole UTI inasumbua sana kupona huenda dawa wanazopewa bacteria wanaresist kwa uhakika kawafanyie Urine culture itaonyesha dawa gani iko active na ipi inareact kwa hao bacteria, wanywe maji mengi pia itasaidia kudilute urine kupunguza maumivu
 
Pole UTI inasumbua sana kupona huenda dawa wanazopewa bacteria wanaresist kwa uhakika kawafanyie Urine culture itaonyesha dawa gani iko active na ipi inareact kwa hao bacteria, wanywe maji mengi pia itasaidia kudilute urine kupunguza maumivu

Asante kwa ushauri mkuu. What about men, yaweza kuwa-affect?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wadau
Naomba mnisaidie tena, UTI visababishi vikuu ni nini? Je, kuna dawa mahsusi kuizuia? Inatesa sana jamani, inatesa. Maji yanatumika sana, lakini bado sijaona improvement yake!
Ushauri tafadhari.
Asanteni.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Wadau
Naomba mnisaidie tena, UTI visababishi vikuu ni nini? Je, kuna dawa mahsusi kuizuia? Inatesa sana jamani, inatesa. Maji yanatumika sana, lakini bado sijaona improvement yake!
Ushauri tafadhari.
Asanteni.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Pole,
UTI kitaaamu humaanisha mkojo "mchafu"....husababishwa na wadudu wa aina nyingi kutegemeana na aina ya jamii yake,
Pili, kuna mazingira yanayosababisha hasa uchafu(kupungua kwa usafi), magonjwa ya zinaa, na upungufu wa utumiaji ya maji.

Ni vizuri kupima mkojo, na ikishindikana kuotesha wadudu walio katika mkojo na hasa kuzingatia dawa.

Fuatilia thread nyingine zilizo JF Doctor zinazohusu UTI!
 
Zingatia unapo pata tiba akikisha una tibia na mwenzio, hilo pia tatizo,, unapo tibiwa peke yako mkija kukutana kimwl mnaambukizana tna..
 
Pole,
UTI kitaaamu humaanisha mkojo "mchafu"....husababishwa na wadudu wa aina nyingi kutegemeana na aina ya jamii yake,
Pili, kuna mazingira yanayosababisha hasa uchafu(kupungua kwa usafi), magonjwa ya zinaa, na upungufu wa utumiaji ya maji.

Ni vizuri kupima mkojo, na ikishindikana kuotesha wadudu walio katika mkojo na hasa kuzingatia dawa.

Fuatilia thread nyingine zilizo JF Doctor zinazohusu UTI!

hata mi nasubr majibu, maana mkojo mchafu na washapandikiza nasubr yalojiri
 
Urinary Tract Infections (UTI), inasemekana inasbabishwa sana na akina dada kujiosha kinyume wakitoka either haja ndogo au kubwa. Vagina mara nyingi ina bacteria ambao ni normal flora (wanailinda papuchi ba hawaleti madhara). Sasa mdada akianza kujiosha baada ya kujisaidia anapeleka kidole kutoka kwenye papuchi kwenda kwenye clitoris (kikojoleo). Hapo ndipo anapo wapa access wale bacteria wa kwenye papuchi kuingia njia ya mkojo ambayo yenyewe huwa haina bacteria kama wa kwenye papuchi. Hapo ndo msala unapo anza, kwani bacteria u-ascend kufuata mirija ya mikojo hadi kwenye kibofu na sometimes hadi kwenye Figo.
 
Hua mnaniacha hoi mnavokuja huku mnasahau kwenda kwa dokta, vocha unayotumia kuingia JF ungekusanya ifike buku tatu uende kumwona daktari umuulize akupime akupe ushauri, ile hela unayolipa ya kumuona dokta sio ya kumuangalia sura tu, hata kumuuliza maswali unayotaka kujua pia, ni hela yako ile.... watu wanasoma miaka mitano wanamaliza wanaspecialize, kichwani wana mengi sana unaweza kutwa na matatizo chungu nzima umekaa tu
 
Okay ni Hivi
UTI (Urinary Tract Infection) ni infection ya njia ya mkojo,, bacteria wanaosababisha mara nyingi ni E.coli ambaye anapatikana katika utumbo mpana na kwenye kinyesi,,
Ni tatizo linalowapata wadada zaidi kuliko wakaka kwasababu ya ufupi wa njia ya mkojo na ukaribu ulipo na sehemu ya haja kubwa,, wakati wa kujisafisha haja kubwa inashauriwa kwanza utumie maji, pili hakikisha uchafu wa haja kubwa hausogelei huko mbele
Kwa wakaka kama akiwa anafanya sex na kupitisha dudu yake maeneo karibu ya haja kubwa ndo ni rahisi na wewe kuambukizwa.. kwahiyo sex ni vyema ifanyike kiusafi kwa kuzingatia hili
Matibabu:😀awa inayoweza muua E.coli mf ciprofloxacin 500mg bd 7days, ama amoxi-clav 625mg bd 7 days au gentamycin injection 150mg stat then 75mg od 5 days

Natumaini nimekupa mwanga::
 
UTI Dawa yake ni maj jitahd kunywa maji mengi kadri uwezavyo hata mim tatizo hilo lilinisumbua sana.
 
Hi,
Sio mara zote UTI inasababishwa na ngono zembe.Sababu ziko nyingi haswa kwa wadada mfano:
-kutumia ndoo ya kudekia chini kwa kuogea
-kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri na jua.
-kutokuflash choo kwanza kabla ya kutumia,hata kama kwa macho unakiona ni kisafi sana(kutokana na maumbile yetu ya wadada ni rahisi kuambukizwa hata magonjwa ya zinaa kwa njia hii so ni vizuri kabla ya kutumia choo hakikisha kama ni cha kufyashi umemwaga maji kwanza ya kutosha ndipo utumie.
-Kutokujikusha vizuri maeneo ya siri pindi uogapo au utawazapo,mdada unatakiwa kuhakikisha unajikausha vizuri wakati umalizapo kuoga/kutawaza ili vimelea vipendavyo kukaa sehemu ya unyevunyevu visipate nafasi.
-Hakikisha taulo unalotumia ni kavu na safi daima.

Nimewasilisha.
 
  • Dalili za ugonjwa wa UTI kwa wanaume‏
UTI_240.jpg



UTI ni nini ?


Maambukizi katika sehemu yeyote ya njia ya mkojo husababisha maradhi na matatizo ya aina mbalimbali. Mara nyingi tunapozungumzia UTI, huwa tunalenga maambukizi yanayosababishwa na vimelea
(bakteria) au chochote kile kinachoweza kusababisha UTI huingia katika njia ya mkojo kutokea aidha nje ya mwili au hata ndani ya mwili kwa njia ya damu au vinginevyo.

UTI huweza kumpata mtu yeyote bila kujali jinsia au umri. Hata hivyo, yapo makundi ambayo kutokana na sababu za kibiologia na kinga ya mwili kushuka au kuwa ndogo huathiriwa zaidi na tatizo hilo. Makundi hayo ni pamoja na watoto, wazee na wanawake.

Watoto ni waathirika wakubwa wa UTI na yaweza kusababisha maambukizi kusambaa hadi kwenye damu na mwiili mzima na hatimaye kusababisha kifo. Maumbile ya watoto na utegemezi walio nao wakati wa kujisaidia inaweza kuwa ni sababu hatarishi kwa wao kupata

tatizo hili. Vile vile kinga yao ya mwili bado huwa bado haijakomaa kuweza kuhilili uvamizi wa vijidudu mbalimbali kwenye miili yao.

Wanawake kwa upande wao huathiriwa na UTI hasa kutokana na mfumo mzima wa maungo yao hasa ya mfumo wa mkojo kuwa na urahisi wa kuingiliwa na bacteria. Mathalani, mrija wa mkojo yaani urethra ya mwanamke ni fupi sana ukiliganisha na ya mwanaume na hivyo vijidudu au bakteria kupata urahisi wa kuingia ndani.
Ukubwa wa tatizo

UTI ni tatizo kubwa katika jamii na jinsia. Hata hivyo hakuna data au taarifa kamili juu ya ukubwa wa tatizo hili katika maeneno mengi Duniani hasa katika nchi zinazoendelea zilizo na miundombinu duni na changa ya afya. Utunzaji wa kumbukumbu ni tatizo linachongia pia ukosekanaji wa taarifa.

Kwa kiasi kikubwa tatizo la UTI huathiri wanawake zaidi kuliko wanaume, zaidi ya mara mbili kwa kukadiria. Karibu kila mwanamke katika maisha yake anaweza wa kupata UTI japo mara. Pia uwezekano upo kwa tatizo kujirudia mara kwa mara.

Sababu za UTI


UTI yaweza kusababishwa na vijidudu vya namna nyingi. Mathalani ni vimelea (bakteria) japo pia na jamii nyingine ya vijidudu vinaweza kusababisha UTI. Bakteria aina ya Escherichia coli kwa kiasi kikubwa ndio inayosababisha UTI japo pia bakteria wengine wapo. Vijidudu hivi vyaweza kuingia katika njia ya mkojo kutokea nje ya mwili au hata kwa kupitia damu ya mhusika.


Kwa wanawake, fangasi katika sehemu za siri imekuwa ni tatizo kubwa sana. Uwepo wa fangasi hasa kwenye uke na maeneo jirani pia huweka mazingira ya mvuto kwa bakteria kuvamia maeneo hayo na kuleta maradhi, hasa UTI.

Kwa wanaume mara nyingi kutokana na maumbile yao na mfumo mzima wa mkojo na viungo vyake, huwa siyo waathirika wakubwa wa UTI.

Vihatarishi

Sababu hatarishi
(risk factors) za UTI zipo nyingi, kulingana na umri, jinsia na mazingira ya mhusika. Mfano sababu hatarishi za mtoto mchanga kupata UTI si sawa na mtu mzima jinsia ya kike. Maumbile na mfumo wa kibiologia ya mwanamke humweka katika nafasi hatarishi zaidi ya kupata UTI. Vile vile ngono, tena ya mara kwa mara ni moja ya sababu zinazoweza kuchangia mtu kupata UTI.

Kwa kupitia ngono, bakteria waliopo katika sehemu za siri za mhusika vinaweza kupata nafasi ya kupenya na kuingia katika mfumo wa njia ya mkojo kwa urahisi zaidi.

Sababu nyingine ni upungufu wa kinga mwilini kwa sababu yeyote, ikiwamo ujauzito kwa wanawake na ugonjwa wa kisukari (diabetes). Lakini pia, sababu nyingine kadha wa kadha zinazosababisha upungufu wa kinga mwilini.

Dalili za UTI je?

Dalili za UTI kwa kiasi kikubwa hutokana na umri na jinisia ya mhusika, lakini zaidi kisababishi
(cause) ya UTI. Dalili zinaweza kuwa kusikia maumivu wakati wa kukojoa, homa na maumivu katika viungo vya mkojo, kuhisi kuhitaji kukojoa mara kwa mara na pia mkojo kuwa na hali ya kuunguza wakati wa kukojoa.

Nyingine ni maumivu ya tumbo chini ya kitovu na au mgongo kwa chini. Mkojo wenyewe unaweza onekana wenye damu au usaha.

Kwa watoto dalili pekee kubwa ni homa. Hii inaweza kuambatana na kushindwa kula vizuri, kulia lia sana na hata kutapika.
Matibabu ya UTI

Matibabu ya UTI kwa kiasi kikubwa unapatikana bila shida na usumbufu mkubwa maadam tatizo lijulikane mapema na kwa usahihi. Utaratibu mzima wa matibabu hutegemea majibu ya maabara, kisababisho cha UTI na umri pia wa mhusika


Pamoja na hayo, UTI ni ugonjwa unaozuilika. Kwa ujumla suala zima la kuzingatia kanuni za afya bora hasa ya mwili na mazingira ni suluhisho tosha kwa tatizo la UTI.


Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.

Dawa ya Maradhi ya UTI:

Kwa Mtu Mgonjwa wa Maradhi yoyote inatakikana awe anakunywa maji Uvuguvugu anapo Amka Asubuhi

kabla ya kupiga mswaki Unywe Glasi 2 za Maji ya Uvuguvugu na baada ya kupiga Mswaki Unywe glasi 1 na

kabla ya kunywa chai unywe Glasi moja ya maji ya Uvuguvugu kila siku Ufanye hivyo kwa wakati wa

asubuhi.
Na Wakati wa Mchana Dakika 15 au dakika 30 kabla ya kula chakula cha Mchana unywe maji ya Uvuguvugu Glasi 1.

Na Wakati wa chakula cha Usiku unatakiwa unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 2 kabla ya kula chakula cha usiku.


na unywe Maji ya Uvuguvugu Glasi 1 kabla ya kwenda kulala usiku. Jumla utakuwa umekunywa glasi 8 kwa siku huu ndio


utaritibu wa kutibu kila maradhi hapo juu uwe unakunywa kila siku mpaka upone hayo maradhi yako na huenda


ikachukuwa muda wa miezi 3 ukifulululiza kunywa hayo maji ya Uvuguvugu utakuwa umekwisha pona maradhi yako



Unywaji wa maji mengi ili kupata mkojo mwingi ili pengine uweze kusafisha njia ya mkojo nayo pia inashauriwa. Inashauriwa pia kukojoa mara tu baada ya tendo la kujamiiana. Kwa watoto ni muhimu kuzingatia matumizi sahihi ya pampers hasa kubadilisha kwa wakati.

TIBA MBADALA YA MARADHI YA (UTI) PATA MAFUTA YA KHARDALI KUNYWA KIJIKO KIMOJA ASUBUHI KIJIKO KIMOJA MCHANA NA KIJIKO KIMOJA USIKU KWA MUDA WA SIKU 3 AU SİKU 7 KISHA NENDA KAPIME HAYO MARADHI YAKO YA (UTI) UTAKUTA HAKUNA TENA INSHALLAH.

318px-Mustard_oil.JPG

MAFUTA YA KHARDALI KWA KIINGEREZA YANAITWA MUSTARD OIL.


Dawa ingine ya kutibu Maradhi ya UTI ni hi hapa kwa jina inaitwa Grape seed extract

pGNC1-2331338t300x300.jpg

Mustard oils for UTI treatment

Mustard oils derived from horseradish root and the nasturtium herb can be used as treatment for UTI, according to a 2006 study published in the Arzneimittel-Forschung journal. The study found that a combination of extracts from

horseradish and nasturtium, two plants from the mustard family containing volatile mustard oils as the

active ingredients, demonstrated antimicrobial properties, meaning they kill or inhibit the growth of

microorganisms like bacteria. Researchers stated that the combination of these two supplements is a rational treatment for UTI and upper respiratory infections.

In a similar study published in the
Arzneimittel-Forschung journal that same year, participants took either antibiotics or an herbal drug combining horseradish and nasturtium. The group who took the antibiotics

experienced a 87.9 percent decrease in symptoms versus 81.2 percent in patients who took the herbal drug.

However, researchers found that the herbal drug had a clear advantage because the participants taking the supplement needed fewer supportive procedures and administration of concurrent medication.

Grapeseed extract

Grapeseed extract may also be an effective treatment for UTI and other infections. The supplement promotes activity to fight bacteria that are causes of urinary tract infections.

Grapeseed extract also has antifungal and antiviral properties to treat infections caused by fungi or viruses.
The University of Maryland Medical Center recommends taking 100 milligram capsules or five to 10 drops of liquid grapeseed extract three times a day for treating infections.



 
Back
Top Bottom