Hivi mtoto wa nje anawezaje kunipiga kwenye urithi ambao nimepambana na baba yake kuutafuta. Ninachojua kisheria mwenza mmoja akifariki basi urithi unagawanywa 50 kwa 50,, sasa katika ile 50 ya marehemu mke ana asilimia yake na watoto wana asilimia yao.
Na binafsi nimeshasema kama mwanaume ataleta mtoto wa nje mapema sana nitamwambia kama ni kujenga au kutafuta urithi wa mwanae mapema ingali yupo hai. Na hivi najua na sheria kimchongo. Baadhi ya watoto hawana shukrani kama mama alimlea leo hii anawezaje akauza nyumba zote halafu mke halali akakae wapi. Tena mtoto ambaye amepatikana ndani ya ndoa.Thubutu yake
Sent using
Jamii Forums mobile app