Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Ndivyo navyoweza kusema,
Hii ni kwa wale wanaokaza sana,yaani mnaishi kitumwa mno.hii ni Kwa watu wa mikoani
Ni rahisi kukuta mtu anakula vitu vya ajabu au sehemu isiyoridhisha kwa madai ya kubana bajeti.
Kuna mtu anaweza kumaliza hata mwezi hajawahi kula nyama na familia yake kisa anabana bajeti,kwake nyama ni anasa,Maharage,mboga za majani za kutembeza ndiyo rafiki kwake.
Nyie mnalalamika kupanda Kwa bei ya kilo ya nyama yeye hata haongei ni vitu havimuhusu, mtu huyu hata friji hana ,la nini? ili ahifadhie nini?
Yeye vitu vyake vyote ni nusu na robo ananunua kwa mangi unga na mboga ya Kula siku hiyo hiyo imeisha hiyo hana time ya kuweka bajeti ya mwezi anaona kama pesa inaisha.
Mtu huyu siyo choka mbaya unakuta ana nyumba kadhaa katikati ya mji kapangisha,ana vijimiradi kibao anaendesha. Makusanyo yake yanafika milioni tano mpaka sita Kwa mwezi kwenye biashara zake kama faida.
Bado hajachukua Kodi kwenye majengo yake,chaajabu kwenye maisha yake hana hata smartphone ,simu ambazo zinarahisisha kupost vitu au biashara zetu hususani mtandao wa WhatsApp.
Havai vizuri,nguo zake pamoja na viatu anavyovaa havivuki 30000/-
Mtu huyu hana usafiri wa uhakika,anapanda daladala,akizidi sana ni pikipiki usafiri hatari sana huu .
Mtu huyu haamini katika elimu watoto wake wamesoma Sana wameishia form four tena shule za kayumba.
akaunti za benki kila moja inaanzia milioni 700 kwenda juu.
Maswali yangu hizi hela anamtafutia nani?
Hali vizuri,
Havai vizuri,
Hana usafiri,
Nyumba nzuri zote kapangisha halafu anaishi kwenye kagofu tu.
Pesa mnamtafutia nani?
Badilikeni wakuu,haswa watu wa mikoani