Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,512
- 2,980
Za asubuhi ndugu zangu, kwema?
Kwa wale wanajamii forums wenzangu wafuatiliaji wa siasa za kibabe na za kimikakati za nchi za magharibi hasa Marekani. Bila shaka mtakubaliana na mimi kwamba sasa Russia (itake isitake) inakwenda kugawana baadhi ya majimbo yake ya mpakani na Marekani kupitia mgongo wa vita yake (Russia) na Ukraine.
Ni nani asiejua kwamba toka miaka mingi iliyopita, lengo kuu la Marekani na washirika wake lilikuwa ni kuigawanya Urusi vipande vipande ili iwe na eneo dogo, jeshi dogo na uchumi wa kawaida kwa ajili ya masilahi mapana ya kijeshi, kiuchumi na kiubabe kwa Marekani na washirika wake!
Hata kugawanyika kwa umoja wa nchi za Soviet pia kulikuwa na mkono wa Marekani na washirika wake, ambao wanataka kuiona Russia inakua nchi yenye kaeneo ka kawaida, jeshi la kawaida na uchumi wa kawaida kama ilivyo Iran, North Korea, Venezuela nk.
Sasa basi, kwa vile mkakati wa kuigawanya Urusi kwa njia ya kawaida ulishindikana, ndo ukatengenezwa mkakati wa kuanzisha zengwe katika mipaka ya Russia kwa kuitumia nchi ya Ukraine huku Marekani akiamini kwamba zengwe hilo lingeweza kuzaa matunda kwa kuishawishi Russia (bila kujua) iingie katika vita na Ukraine, na hatimae baadae Urusi itapoanza kuwa weak (kuelemewa) kutokana na vita hivyo.
Marekani na washirika wake waitumie nafasi hiyo kuitwanga Russia (kupitia jeshi la Ukraine) na hatimae kuingia mpaka Russia kama vile Russia ilivyoingia Ukraine. Ukraine itapoingia Russia, Marekani ataendelea kutuma silaha nzito nzito mno za kijeshi ili kuwapa nguvu zaidi wanajeshi wa Ukraine kuteka baadhi ya majimbo ya Russia yaliopo katika mpaka na Ukraine.
Ikumbukwe kwamba Marekani na washirika wake hawajaingia kwenye hii vita kijeshi, lkn wamekuwa wakituma silaha mbali mbali kwa jeshi la Ukraine ili kutimiza mipango yao, na kwa kiasi kikubwa zimeleta mafanikio makubwa kwa jeshi la Ukraine.
Mmarekani chini ya CIA yake sio mjinga wa kutuma tu mamilioni ya dola na silaha nzito nzito kwa Ukraine bila kujua hizo hela atazirudisha vipi. Bila shaka anajua anachokifanya, na huu ni mkakati wa muda mrefu ambao Putin bila kujua ameingia kichwa kichwa vitani asijue madhara yake ya baadae.
Vita hii ni kama mpira wa miguu ambapo timu iliyoanza kushambulia, sasa inashambuliwa huku wachezaji wake hadi wa akiba wakiwa hoi bint tabaani wasijue nini kifanyike ili kuzuia kufungwa.
Vita ilianza kwa Russia kuishambulia Ukraine na kuleta furaha kubwa huko Moscow hali iliyokuwa inapelekea Putin kuongea kibabe na kwa kejeli kubwa dhidi ya Ukraine na washirika wake (Marekani, UK)
Lakini sasa vita imegeuka, Russia sasa ndio inashambuliwa, furaha ya Moscow imegeuka majonzi, mpaka wanajeshi wa akiba wamepelekwa Ukraine, lkn kichapo ni kilekile.
Putin anataman ipatikane suluhu hata kesho ili Marekani asipate nafasi ya kukamilisha mission zake, ila ni kama vile amechelewa,,, na yeye kutafuta suluhu kupitia yeye mwenyewe hawezi, maana itaonekana ameshindwa vita alivyoanzisha, hivyo itakuwa aibu kwake, kwa jeshi lake na nchi yake.
Marekani anapokuwa na lengo la kuvamia nchi fulan kwa ajili ya masilahi yake fulan, basi huwa na njia nyingi tofauti tofauti za kukamilisha lengo hilo bila kujali itamchukua muda gani, na atapata kwanza hasara kiasi gani.
Tuliona alivyotumia mgongo wa Osama kuivamia Afghanistan, tuliona alivyotumia mgongo wa silaha sijui za sumu kuivamia Iraq chini ya Sadam Hussein, tuliona alivyotumia mgongo wa waandamanaji kuivamia Libya, na sasa anatumia mgongo wa jeshi la Ukraine kuivamia Russia.
Japo si kwa nchi yote, lkn kuna baadhi ya maeneo tutakuja kusikia yalivamiwa, kutekwa na kushikiliwa na jeshi la Ukraine (kumbe nyuma ya pazia) maeneo hayo yatakayotekwa yatakuwa chini ya usimamizi wa Marekani.
Hivi sasa Ukraine ishaanza kurudisha maeneo yao yaliotekwa, na kuyarudisha nyuma tena kwa kasi majeshi ya Russia. Ni swala la muda tu mtakuja kuona haya niliyoandika hapa yanatokea, na Putin hatothubutu kurusha bom la nyuklia hata 1, maana kwa vile Mmarekani atakuwa katika baadhi ya maeneo ya ardhi yake, basi akijaribu kurusha atajikuta anajiangamiza yeye mwenyew na watu wake.
Miezi kadha iliyopita China ilitaka kufanya kosa lile lile alilofanya Mrusi, eti alitaka kuivamia Taiwan aifunze adabu. Mimi kwa kutambua hatari iliyopo mbele ya China endapo angeivamia Taiwan, nilikuja fasta fasta kutoa ushauri wangu kwa ndugu zetu wa China ili kuiepusha na mtego uliokuwa umetegwa na wakubwa pale China angethubutu tu kuivamia Taiwan.
Sina haja ya kuweka link ili kuwachosha wasomaji, kwahiyo naweka tu kipande cha picha ya onyo langu hapo chini. Ila atakaetaka kuusoma uzi wenyewe niliowaandikia wa China atautafuta mwenyew ausome kwa kutulia.
Karibuni kwa uchangiaji zaidi, hasa kwa wale wenye uelewa mpana kuhusu malengo na mikakati ya vita hii.
Moderators najua kuna jukwaa la international, lkn nimeuleta uzi huu uku kwa sababu zangu 🙏
Nawatakieni siku njema.