Urusi kuangushwa na Uturuki katika Mgogoro wa Azerbaijan na Armenia. Je, huu ndio mwisho wa Urusi?

Jeshi la Russia na la US wana doctrine tofauti sana na hata mifumo ya silaha wanatofautiana mno.

Wakati US ana Minuteman kwenye silos, Russia anazo Yars kwenye TEL na Sarmat kwenye silos. Yars ni mbadala wa silo endapo zikiharibiwa. Ukishakuwa na mbinu ya kuharibu silaha za adui, unatafuta njia za kuzuia mbinu kama hiyo uliyonayo adui asiwe nayo kuitumia dhidi yako.

Russia anachoamini ikianza vita atashambulia silo za US. Kwa vile wote wanaruhusu preemptive strike, What if US naye akashambulia silo za Russia?
JIBU: Zitabaki TEL
 
Nakubaliana nawe kuwa "makomunisti" ya URUSI yana uhusiano mkubwa wa KIBIASHARA zaidi ya ARMENI....

Ni kweli NAGORNO si eneo halali la ARMENIA japo ya kwamba INA WAKAZI WENGI WENYE Asili ya ARMENIA....

Ni sawa na Kama ingetokea IDD AMIN DADA angetushinda vita ya KAGERA na kubali na eneo la MUTUKULA....halafu kikapita kipindi JWTZ ikalikomboa eneo Hilo...sasa itakuwa ni kosa kwetu?!!!!

Nagorno ni eneo MTAMBUKA la AZERBAIJAN......
 
Sawa Mkuu....

Ila....

Japo ya kuwa ni kweli wana MIFUMO TOFAUTI...

Unaweza ukanielewesha ni kwanini US haigi kuwa na TEL huku akitambua kuwa TEL za Urusi zitabaki pale ambapo SILO zake zitakapopukutishwa?!!!!
 
Hivi mkuu ukitoa US, UK na Ufaransa ndani ya NATO kuna nchi yenye ushawishi zaidi ya Uturuki?

Huenda hata imeizidi Ujerumani?
 
Sawa Mkuu....

Ila....

Japo ya kuwa ni kweli wana MIFUMO TOFAUTI...

Unaweza ukanielewesha ni kwanini US haigi kuwa na TER huku akitambua kuwa TER za Urusi zitabaki pale ambapo SILO zake zitakapopukutishwa?!!!!
US ana bases nyingi nje ya nchi yake. Ana long range bombers nyingi kama B-2, B-52, B-1B na B-21 ijayo. Yeye haoni umuhimu wa kuwa na TEL kama silos zake zitashambuliwa atatumia hizo njia nyingine, zikishindwa kabisa atatumia Submarine Launched Ballistic Missiles (SLBM) ambazo hata Russia anazo pia.

Pia Russia ana bases za NATO zinamzunguka hivo kuwa na missiles za TEL inaongeza uwezo wa kushambulia mapema bases zilizokaribu yake. Ndio maana Russia ana Iskander ila US wala NATO hawana tactical missile ya range ndogo vile.
 
Hakika....

Halafu hizo TER ukizing'amua zilipo...ni rahisi mno KUZISHAMBULIA halafu yakitokea hapo basi inakuwa KAZI kubwa KUZIHAMISHA sehemu salama....na inachukua MUDA MREFU KUZIHAMISHA......

Kubwa ni kuwa US hazifanyi propaganda kwa raia wake KUZIONYESHA SILO....Urusi wao kila mwaka wanafanya PARADE viwanjani kujitapa NAZO kwa wananchi...vilevile kwa wale "vichaa" wa KOREA KASKAZINI😂😂 MIKOMUNISTI banaaa....

All and all SIKU ikitokea US akikutana na URUSI uso kwa uso ndio tutajua YUPI hana propaganda KOKO....
 
Hivi mkuu ukitoa US, UK na Ufaransa ndani ya NATO kuna nchi yenye ushawishi zaidi ya Uturuki?

Huenda hata imeizidi Ujerumani?
Ujerumani haipendi kiki wala ugomvi na haitaki kabisa kumiliki silaha nyingi. Tena bora kwa sasa Ursula von der Leyen sio Defense Minister maana yeye alikuwa hataki hata modernization ya silaha.

Ukilinganisha silaha anazotengeneza Ujerumani na wengine bado ana silaha nzuri sana kama diesel submarine, vifaru na magari ya vita, airfighters anazoshirikiana na wengine. Pia ana uchumi mkubwa ila bajeti ya ulinzi ndogo sana. Teknolojia yake kubwa mno hata UK anakaa.

Ujerumani ni sleeping giant. Akitakiwa kupigana let's say na Uturuki ataumia mwanzoni ila wacha afanye mass production na makampuni yake yajikute kukomboa taifa, Uturuki anagalagazwa. Uturuki anajitutumua kama proxies za Azerbaijan na Libya tu zinamtoa jasho kiuchumi sembuse superpower.
 
Silo hazioneshwi labda ukiona video kisha wakasema "at unspecified range" utajua ni wapi?

Hizo TEL hata ukiziona kwenye gwaride, vita ikianza hautazikuta Kremlin Square zitakuwa porini uko mfano kuna hiyo Siberia kuubwa na iko wazi. Kwanza TEL inatumia chini ya lisaa limoja kufyatua wakati silo inatumia maandalizi ya hadi siku nzima.

Kwenye silo unaona locomotive inaenda kisha inaishia porini na hakuna kituo. Unajua tiyari kuna silo. Siku wanashambulia utaona locomotive kwenye silo unajua missile imepelekwa, bado fuels na mengine. Kwenye TEL kila kitu kishawekwa uko kwenye ghala dude linatembea hata kulitrack huwezi itakuja kuliona pale tu litakapofyatua kombola ule moto unakuwa detected na satellite. Muda huohuo TEL inaondoka. Utashambulia saa ngapi?
 
Kwenye hii vita, aliyopoteza ni Armenia, kapoteza eneo na watu kwa maana ya askari
Uturuki hajashinda sababu plan zake hazijatimia
Azeri ndio kashinda
Urusi hajaingilia sababu lile eneo sio la Armenia, na pia ni kama adhabu kwa PM wa ambaye alikuwa anaegemea west na kujitengenga na Urusi
Pia kapata base kwenye ardhi ya Armenia kwa kigezo cha peace keepers
 
Prishtina ha ha ha haa
 
Ila kwa sasa vigogo wenye sauti na ushawishi ndani ya NATO unaweza kuiacha Uturuki kweli?

Kuhusu Ujerumani mkuu, hata kama akiamua kujijenga kijeshi huoni bado ni ngumu (kumbuka nchi za Ulaya zinaitegemea sana Marekani kiulinzi).

Kama unakumbuka kampeni ya kumtoa Ghadafi awali nchi za UK na Ufaransa ilibidi ziombe msaada kwa Marekani ili kuweza kuendelea na mashambulizi ya anga baada ya kukabiliwa na upungufu wa silaha na fedha na hii ilidhihirisha wazi utegemezi/udhaifu wao.

Tizama operesheni za Ufaransa za kupambana na Ugaidi kwenye nchi za Sahel, ambapo anahaha kuishawishi Marekani isiondoe askari wake huko maana tayari imeshalemewa na pia washirika wake wa Ulaya hawana uwezo wa kumsaidia (Ujerumani imekataa kabisa kupeleka askari huko)

Lakini angalia namna Uturuki ilivyojitanua Syria, Libya na kiasi kidogo (Iraq) bila msaada wa NATO.
 
Uturuki kaanza ushawishi mwaka jana kwa serikali ya GNA na pia mwaka huu kwa Azerbaijan. Pale Libya yupo pia UAE na Egypt, hawa hatuwezi kuwaita vigogo wa Middle East ingawa wako Libya.

Pale Syria yupo Uturuki ila ni mpakani kwake ana jambo lake na Wakurdi, hata hivo Iran naye yupo ila hatuwezi muita kigogo wa Middle East.

Ushawishi wa Uturuki ni sera za Erdogan za kuikamua nchi na kutengeneza influence nje. Ingawa zinatoa mazoezi kwa jeshi na silaha pia kutangaza silaha zake. Mfano waliolpoanza operations hizi ndio ikajulikana kuwa drone technology yao iko juu.

Uturuki umuhimu wake ni mkubwa ila uwezo wake usikuzwe. Bado ananunua helicopters, submarines, jets, air defence systems na mifumo muhimu kwa hizo NATO members. Na hata kutengeneza systems zake anategemea kwa kiasi hao wazungu, kinyago uchonge wewe alafu kikutishe!
 
Teh teh teh 🤣 🤣🤣...hao jamaa wanachangamsha sana jukwaa, japo wamejikita kwenye taarifa za kipropaganda.
Mkuu sio propaganda ,kwani na ww unakubaliana na mtoa mada ya kwamba Erdogan amempiga bao Putin?
Alafu mkuu bwama utamu yuko wapi siku hizi aise? ametoweka kabisa jukwaani.
 
NGOJA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA

HIVI UNAIJUA URUSI AU UNAISIKIA

NAHISI USA PEKE AKE NDO ANAIJUA ..........
MWISHO.....KUTOKUWEPO KWA HAO MABALOZ HAKUNA SHIDA ......TUNAPIGA KAZIIII
 
Kutokana na mwenendo aliounyesha Russia, ni wazi Armenia atafute njia ya kupunguza ukubwa wa kambi ya mrusi iliyopo Armenia huku akimkaribisha USA.
 
Kutokana na mwenendo aliounyesha Russia, ni wazi Armenia atafute njia ya kupunguza ukubwa wa kambi ya mrusi iliyopo Armenia huku akimkaribisha USA.
Urusi hawezi ruhusu kitu kama hicho.
 
Mleta mada Putin umri haujamtupa kwani anazidiwa na Kikwete 2yrs pia kuimaliza kijeshi Urusi sahau kwani NATO pamoja na maguvu yao walishashindwa, kusema Urusi ina uchumi mbaya si kweli isingekuwa ya pili Kwa kuuza silaha na vifaa vya kijeshi duniani baada ya US, kama unaichukulia poa Urusi Kwa sababu ya limbwata sijui la nani soma habari mbalimbali juu ya Urusi upatekuelewa na siyo kukariri Stori za vijiweni mwisho Putin haumwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…