Urusi kuangushwa na Uturuki katika Mgogoro wa Azerbaijan na Armenia. Je, huu ndio mwisho wa Urusi?

Swali sasa ni Je, Kwa hali inavyoenda duniani huku Ccm wakiwa wanawategemea China na Urusi, CCM itaendelea kuwa hai katika miaka michache ijayo
Kwa bavicha kila kitu lazima mkihusishe na siasa za ccm na chadema. Ccm inaitegemeaje Urusi?
 
Missiles ambazo zinakuwa launched kwenye silo na hizi ambazo zipo kwenye mobile vehicles kiusalama bora hizo ambazo zipo kwenye mobile vehicles, kwasababu leo utaziona hapa kesho utazikuta kule. Sasa kama kuna umbea umevuja kuhamisha missiles ni rahisi sana.
 
Kwani Urusi ilishiriki kwenye hiyo Vita moja kwa moja kama Uturuki ilivyofanya?
Na hii ndo tofauti ya Mabeberu na Shia. Beberu haingii kwenye beef yakijinga ambayo anaamini hatapata wese, gas, madini e.t.c

Sasa Mwarabu yeye yuko tayar kupoteza dola kibao kuingiza jeshi mahala flan just kuwatetea Waislam wawili. [emoji23][emoji28]
 
biashara ya kati ya russia na azerbaijan ni kubwa kuliko russia-armenia sababu population ya azerbaijan ni kubwa sana kulinganisha na population ya armenia milioni 9 vs million 2, lakin kisiasa russia yuko karibu sn na armenia kuliko azerbaijan ambaye amediversify sn mahusiano yake kwenda west turkey na israeli,
kuhusu issue ya libya ni kweli vyote hvyo ulivyoandika but operation ya haftar kuichukua tripoli imekwama sababu ya mtu mmoja tu naye ni turkey, pili serikali ya GNA ndiyo yenye uhalali wa kisiasa libya hvyo km bado inaexist ni ngumu sana haftar putin UAE na al sisi kunufaika kama wanavyotarajia ndio maana walikua wanapush kuichukua tripoli, kwa hali ilipofikia sasa haftar hawez tena kuichukua tripoli maana GNA imejiimarisha sana kwa msaada wa uturuki lkn pia ndio serikali inatambuliwa kimataifa, ndio maana hata support ya urusi kwa haftar ni covert tu urusi hadharan amepinga kutuma silaha au wapiganaji huko ila uturuki wala hafichi, kimsingi solution ya mgogoro wa libya haiwezekaniki bila mturuki kuridhika, km unafikiri mturuki hajawa kikwazo kwa urusi pale libya unaweza usiwe sahihi
 
huu ni mtazamo wa zamani sn bro, sasa hivi watu wanashndana kukabana kwenye nyanja za kiuchumi maana huku kwenye nyanja za kijeshi kumeshabalance hakuna mkubwa mwenye wazo la kumvamia mkubwa mwenzie kijeshi, ila utavamiwa kiuchumi na kisiasa na ndio hapo swala la ushawishi anaosema huyu bwana linapokuja, hii sio habari ya AK-47 au S-400 Huku ni swala la EU ama EURASIA, Huku ni issue ya partnership ya armenia na EU itaiathiri vipi urusi, huku ni swala la uturuki kujiimarisha kisisasa caucasas ambako ni backyard ya mrusi, au maritime deal kati ya uturuki na libya inawaathiri vipi ugiriki misri pamoja na supporters wa haftar kule mashariki mwa libya, watu wanapambana wasizibiwe njia za wao kufanya mambo yao ukizubaa wanakusuffocate kisawa sawa
 
na chakuongezea hapo silaha kubwa mturuki anayolingia ni mahala nchi yake ilipo, mrusi atatamba atambavyo lakin ana maslahi pale kuanzia gas pipeline yake kwenda ulaya pamoja kuaccess Mediterranean kutokea black sea through bosphorus, mmarekan naye na NATO wote lazima wapite pale kwenda black sea, lakin pia ni km buffer kati ya ulaya na mashariki ya kati na ataendelea kuwa hvyohvyo maana wazungu hawatamuingiza EU, kuna faida nyingi sana uturuki anazo sababu ya geographical position yake hvyo kumfanya aitajike na kila mtu eneo lile na wengineo wa mbali, lakin pia kwa sasa ni edorgan ana ushawishi mkubwa sana kwe ulimwengu wa kiislamu hata km viongoz wa kiarabu hawampendi ila wananchi wao wanamkubali hii nayo ni faida kubwa sana, ukichanganya na hizi dili zake za azerbaijana na libya ni changamoto kdg kwa putin ukizingatia wana mitazamo tofauti syria na ukraine pia
 
Kama ulinzi na usalama ni mtazamo wa zamani basi waivunje NATO wabaki na EU na blocks kama NAFTA au Schengen.

Kiuchumi sikatai.
 
Reactions: RTI
Kama ulinzi na usalama ni mtazamo wa zamani basi waivunje NATO wabaki na EU na blocks kama NAFTA au Schengen.

Kiuchumi sikatai.
hpn ulinzi na usalama c mtazamo wa zaman but huko tayari kuna balance na ni ngumu sana kuchange hiyo balance, coz saivi ikitajwa urusi na marekani watu wanaanza kujadili mambo ya kijeshi tu lakin kiuhalisia kuna vita kali sana kwe masuala ya mengine km nishati na uchumi kiujumla kuliko hayo mambo ya kiusalama kwa sasa
 
Mkuu sio propaganda ,kwani na ww unakubaliana na mtoa mada ya kwamba Erdogan amempiga bao Putin?
Alafu mkuu bwama utamu yuko wapi siku hizi aise? ametoweka kabisa jukwaani.
Mkuu putin anamahesabu makali San, unajua alivowagombanisha uturuki na USA na magharibi kwaujumla pale alipompa erdogan mkanda mzima wanamna alivokua atolewe madarakan na Hao jamaa kupitia mapinduz? Hebu vuta picha toka putin amuokoe erdogan nilin Hawa jamaa Waliachana, mm natabiri kama uturuki akizid kuungana hiv na rushia tutegemee hakun chamarekan Wal China Dunia itahikwa nahiz nchi mbili


Ngoja nitoe mfano kidogo ili kujenga hoja yang, putin amekutana kijeshi na erdogan sirya unaona walivoyamaliza hasa kule idlib? Je marekan hajaangukia pua baada ya Hawa jamaa kupanga mikakati Yao kuhusu sirya? Kule Libya walikua a uwanja wamapambano sim a kumbuka walimalizan vizur2 na baada yakumalizana marekan nawashirika wake wameambulia kitu? Turud Armenia na azabaijan, siniwao wamemaliza Yale mapigano Hakuna chamarekan Wal mfaransa wote wameangukia pua nachakushangaza Zaid yy putin na erdogan ndo majeshi Yao yanasimamia Aman, swali lakujiuliza haya yote yanayo tokea yanaiweka wapi marekan na wamagharibi? Maan tumezoea kuona haya mambo yanafanywa nawao kwenye migogoro yote dunian, hebu wajuvi tujikite hapo,

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€ nmecheka tu ulivyoihusisha ccm.
 
Nawewe unaamini kabisa yale yalikuwa ni mapinduzi yaliyopangwa na marekani kumtoa Erdogan??πŸ˜€πŸ˜€,Marekani wapange mapinduzi kwa vifaru 10?,seriously πŸ˜€ πŸ˜€
 
Nawewe unaamini kabisa yale yalikuwa ni mapinduzi yaliyopangwa na marekani kumtoa Erdogan??πŸ˜€πŸ˜€,Marekani wapange mapinduzi kwa vifaru 10?,seriously πŸ˜€ πŸ˜€
Ina maana ilikuwa ni mpango binafsi wa Erdogan kuwamaliza mahasimu wake wa kisiasa na kujilimbikizia madaraka?

Kama ndio hivyo huenda akawa amefanikiwa kuwa mmoja wa viongozi wenye nguvu zaidi Uturuki, ila kwa siasa zake za kimabavu,kidikteta na maadui aliojijengea ndani na nje ya Uturuki huenda asiwe na mwisho mzuri.
 
Ndio maana yake mkuu,ule ulikuwa mpngo wa Erdogan kuwamaliza wapinzani wake na kuongeza ushawishi wake na imani kwa watu wake.Aliwajua wapinzani wake,akaamua kutengeneza mapinduzi fake kwa kushirikiana na wanausalama.Sasa wapinzania wakala ndoano bila kujua its na trap.Marekani hawezi risk mapinduzi kwa kutumia vifaru 10 na ndege 4 eti kumpindua Erdogan.Ile ilikuwa operation ya kusafisha wapinzani wake na alifanikiwa kwa zaidi ya asilimia 90%.Eti leo marekani apangekumpindua erdogan halafu eti bado aruhusu kambi za marekani kuwapo turkey na ubalozi na mahusiano kuendelea,huyu sio erdogan ninayemfahamu..
 
Kwahiyo unafurahi tukikosa misaada kutoka katika hizo nchi?!!πŸ˜’
Siyo kufurahi,km una sifa za kunyimwa utanyimwa tu,kwani hata ukinuna ndiyo itakusaidia nini.Hela ni za kwao utawapangia.
 
Ila Erdogan amefanikiwa sana kuidhibiti Uturuki kwa sasa maana baada ya hilo jaribio kushindwa alisafisha kila idara kuanzia jeshi, mahakama,bunge,vyuo vya elimu na kuwaondoa aliowaona ni kikwazo kwake.

Kitendo cha kuwashambulia Wakurdi huko Syria kimempaisha Sana kwa raia wake , japo ulimwengu wa kiarabu umechukia mno na wanamuona kama mtu mwenye nia ya kujitanua na Sasa ndio wanafahamu walikosea sana waliposhirikiana nae kumhujumu Assad.

Hili bifu alilolianzisha na Saudia,UAE na Misri litakua kikwazo kwenye harakati zake za kujitanua,ndio maana mataifa ya kiarabu (isipokuwa Qatar) wameamua kumuacha mwenyewe aubebe mzigo wa Vita ya Syria.

Ila mkuu kwenye siasa mambo yanabadilika ghafula na kwa haraka sana, huenda na yeye huko mbeleni akakabiliwa na upinzani ndani ya chama chake au vuguvugu la raia na akaanguka.

Jamaa anaikamua nchi yake ili aendeshe siasa zake za kujitanua huko Libya,Syria na sasa Nagorno-karabakh, hili huenda likamponza.
 
Kibaya zaidi uchumi wake umezidi kupolomoka kila kukicha na sarafu yake inazidi kushuka thamani
 
Naona wazee wa vita bado mnatunishiana misuli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…