Rais wa Urusi Vladimir Putin alijadili ushirikiano wa kisiasa, kibiashara na kiuchumi, pamoja na athari za vikwazo vya Magharibi na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na Rais wa Senegal Macky Sall katika mji wa Sochi kusini mwa Urusi hapo jana (Ijumaa).
Putin na Sall walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano, ikiwa ni pamoja na umuhimu wa kuimarisha mazungumzo ya kisiasa pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na kibinadamu kati ya Urusi na nchi za Afrika, Kremlin ilisema.
Putin alisema kuwa Urusi iko tayari kuendeleza uhusiano wa kibinadamu na nchi za Afrika, akitaja nia kubwa ya Urusi katika utamaduni wa Kiafrika.
Sall pia alibainisha athari za vikwazo vya Magharibi kwa Urusi, akiongeza kuwa nchi nyingi za Afrika ziliathiriwa moja kwa moja na mzozo wa Russia na Ukraine.
"Vikwazo dhidi ya Urusi vimezidisha hali hii, na kwa sasa hatuna nafaka kutoka Urusi, hasa ngano ... muhimu zaidi, hatuna mbolea ... na hii ina madhara kwa usalama wa chakula katika Afrika," Sall alinukuliwa na Kremlin akisema.