Kuna hoja nimeiona humu mara kadhaa kwamba, Ukraine ikijiunga NATO, itavamiwa na Urusi.
Sasa, mimi nimekwisha hoji humu mahali kwamba; endapo Ukraine itajiunga NATO, itapelekea NATO kupata upenyo zaidi wa kuilinda Ukraine kwa kutumia Article 5 ya Mkataba wa Washington (North Atlantic Treaty).
Maana yake ni kwamba, uvamizi wowote wa kijeshi dhidi ya Ukraine, utahesabika kama uvamizi dhidi ya NATO (collective defence). Hivyo NATO kama jumuiya ya kujihami italazimika kuilinda Ukraine kijeshi.
Katika mazingira kama hayo, lipi ni jambo rahisi na lenye nafuu zaidi kwa anayetaka kuivamia Ukraine?
1) Kuivamia Ukraine mapema kabla haijaingia NATO ukiwa ni mpango wa kubadilisha utawala uliopo na kuweka vibaraka?
Au,
2) Kuisubiri Ukraine ijiunge NATO ndipo uvamizi ufanyike, kitu ambacho kitaipa NATO fursa ya kuingilia kati kwa kuitisha Article 5 ya Mkataba wa Washington?