Sexer
JF-Expert Member
- Oct 22, 2014
- 8,440
- 8,149
Gavana wa jimbo la Belgorod nchini Urusi ameishutumu Ukraine kwa kushambulia ghala lake la mafuta katika mji huo.
Vyacheslav Gladkov alisema kupitia Telegram kwamba moto mkubwa uliozuka Ijumaa asubuhi kwenye ghala hilo, ulisababishwa na mashambulizi ya anga kutoka kwa helikopta mbili za Ukraine.
Awali alisema kuwa watu wawili walijeruhiwa, lakini hakukuwa na hatari yoyote ya kutishia maisha. Wakazi wa mitaa ya karibu waliondolewa wakati maafisa wa zima moto wakikabiliana na moto huo, alisema.
Hatua hiyo inajiri siku mbili tu baada ya eneo hilo pia kushuhudia milipuko mwingine katika jengo la kuhifadhia silaha. Belgorod iko kaskazini mwa mpaka na Ukraine.
Ukraine haijathibitisha kuhusika na milipuko au mashambulizi hayo.