Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Marekani imekuwa ikifuatilia mwenendo wa meli za kijeshi ambazo zimeonekan zikielekea upande wao kwenye visiwa vya Carribean.
Haijajulikana kiuhakika meli hizo za kawaida za kijeshi na zile za kubebea ndege zitatia nanga eneo gani,hata hivyo inakisiwa itakuwa ni Venezuela na Cuba.Mazoezi hayo ya kijeshi yanatarajiwa kuanza wiki chache zijazo.
Katika siku za karibuni kuhusiana na vita vinavyoendelea kule Ukraine na hasa pale baadhi ya nchi za NATO kutoa ruhusa ya silaha zao kutumiwa na Ukraine kupiga popote ndani ya Urusi,nchi hiyo imesema ruhusa hiyo itajibiwa kwa namna stahiki.
Jibu jengine la Urusi kwa hatua hizo za nchi za NATO limetolewa na raisi Vladmir Putin hapo jana,pale aliposema nchi yake itawapa silaha wapinzani wa kila nchi itakayotoa silaha kwa Ukraine ili iipige Urusi.