Urusi yapeleka vifaa vya kijeshi kufanya mazoezi Carribean pembezoni mwa mipaka ya Marekani

Urusi yapeleka vifaa vya kijeshi kufanya mazoezi Carribean pembezoni mwa mipaka ya Marekani

Mkuu wakati mwingine ukikaa kimya unapata credit.

Ukraine inasaidiwa hii vita na nchi ngapi? Wamepeleka vifaru vyote ambavyo wanasema ndio main battle tanks vyote vimelipuliwa.

Wametuma kila aina ya drones za kisasa zilizopo NATO hakuna kitu. Hivi unajua Ukraine imepotrza eneo lenye ukubwa sawa na UK? Unajua taifa lilikua na watu 38m + na sasa wapo chini ya 25m. Hivi unafahamu the best agricultural land and industrial areas zipo chini ya Urusi?

Kila siku anaambiwa kaa chini tuongee hataki anasema atashinda vita. Unafahamu 28% ya deni la Ukraine lipo kwa makampuni 2? N.k

Pia fikiria Urusi ina vikwazo 17,000+ hakuna nchi duniani iliwahi kuwekewa vikwazo hivyo na bado nchi inauchumi imara kuliko walioweka vikwazo.

Mwisho hakuna nchi hata moja Ulaya inayoweza kupigana na Urusi aidha yenyewe au collective west haipo. Hata USA peke yake hawezi kupigana na Urusi.

Kasome nuclear doctrines za mataifa wenye nazo. Pia ukiza tacticle nuclear missiles za nchi za NATO na Urusi na madhara yatokanayo kisha ujiulize nani anaweza kupigana na URUSI
Mahaba niue shida kwelikweli russia iishinde USA? Hii russia inayosaidiwa na iran (drones), north korea (missiles) na china kuikabili ukraine? Hii russia iliyouza alaska kwa USA, hii russia iliyomeguka from soviet baada ya akili kubwa ya USA kuimaliza USSR?
Russia kamwe hana ubavu wa kuishinda USA achilia mbali europe eunion pasipo USA kwenye vita napo hana huo ubavu.
 
Hitler aliiteka karibu nusu ya Ulaya ila alishindwa , Marekan kafanikiwa kuishawish Ulaya kumkabiri Putin , bado huon hili ni pigo kwa Urusi ? kama Ukraine imemsumbua je Ulaya wakiingia itakuwaj ?

Mtu mweusi huchambua mambo kimahaba sana , kama Putin angekuwa na nguvu angesema ataikabiri ulaya na Marekan directly na sio kupeleka meli tu , maana Macron ashasema atatangaza kuwa Ulaya ipo vitani na Urusi
Wewe naye tumia akili,kama tokea miaka hiyo Ulaya nzima imeungana na USA kuunda NATO kwa ajili ya kumkabili Urusi ndio ataanzaje kusumbuliwa na Ukraine??

Na huko kusumbuliwa unavyosemea ni kupi?? Maana Urusi amechukua zaidi ya 25 ya Ardhi ya Ukraine na kujenga hiyo miji upya.
 
Walioshuhudia vita vya 1 & 2 vya Dunia waliona wanafaidi sasa sisi ndio tunaenda kufaidi kuona vita vya 3.
 
Ni mjinga pekee ambayo anaweza kuamini Russia inaweza kupandana na USA,Achilia mbali mataifa mengine ya NATO.
Mtu agundue nuclear miaka hiyo ya 40s uje umtishie na hizo hizo nuclear seriously!!
Russia atakutana na kitu ambacho atakikumbuka miaka trillion 1 mbele.
Tatizo watu wanaandika wakiweka mahaba mbele.
Putinya tokea vita ianze mara kibao linatishia russia ina nyuklia russia ina nyuklia🤣😂😆 utafikiri wenzake wana manati
Na sasa zele anamgonga nje ndani.
 
Jana Putin kawajibu Marekani na wasirika wake.

Kwamba Ukraine haina uwezo na nyenzo za kupigwa makonbora ya masafa marefu bila support ya USA na Allies. Ukraine atakuwa anavuta TU kitufe lakini vingine lazima vifanywe na mataifa makubwa US, UK France n.k. Hii maana yake na wao wameingia vitani rasmi.

Majibu yake ni kwamba Urusi itazipa nchi maadui wa US, UK n.k ambazo zinaweza kuzipiga kupigwa makonbora kwenye maeneo strategic ya NATO.

Pili wataimarisha ulinzi wa Anga kuhakikisha yanaharibiwa makonbora hayo.

Tatu amesema wao matumizi ya nyuklia ni kulinda mipaka yake, uhuru wake na usalama wake hivyo pale usalama wa nchi utakuwa hatarini haitasita kuitumia kama ilivyoandikwa Nuclear doctrine. Na kakumbushia maboom ya nuclear yaliyopigwa japani yalikuwa ni 20kilotan na mdhara yake yalionekana. Tactical nuclear za Urusi ni 70kilotani hivyo madhara yake ni 4times ya Hiroshima na Nagasaki. Hivyo Kila step ya NATO itajibiwaipaswavyo.
Inamaana hapo Cuba, Venezuela watashushiwa mizigo ya maana
 
Ni mjinga pekee ambayo anaweza kuamini Russia inaweza kupandana na USA,Achilia mbali mataifa mengine ya NATO.
Mtu agundue nuclear miaka hiyo ya 40s uje umtishie na hizo hizo nuclear seriously!!
Russia atakutana na kitu ambacho atakikumbuka miaka trillion 1 mbele.
Why NATO???????
 
Izo bangi anazozisema Putin. Anazo taarifa kamili kuwa G7 wote wanazo hayo manyuklia kama yeye. Kwa iyo akirusha moja anajibiwa na G7 wote atakuwa amekwisha vibaya na uzuri wa G7 uwezi kukuta wanajisifia Sofia upuuzi wa hayo manyuklia
Kwani sababu ya ulaya kugeuzwa watumwa wa America kupitia NATO ni Nini?
 
Tatizo watu wanaandika wakiweka mahaba mbele.
Putinya tokea vita ianze mara kibao linatishia russia ina nyuklia russia ina nyuklia🤣😂😆 utafikiri wenzake wana manati
Na sasa zele anamgonga nje ndani.
Kinachosemwa ni hivi unajua kabisa huyu bwana " mganga halisi wa kienyeji halafu unataka ukamloge" au "ni mchamungu sana Hadi wachawi wanakwama kwake na wewe unasema ngoja nijaribu." Hivyo elewa mwenye nyuklia hachezewi kwa namna yeyote ile.

Google kitu kinaitwa Tsar boom. Ujuwe nini kilitokea at 50kilotani halafu imagine 70kilotan itakuwaje
 
Mgunduzi wa nuclear ni USA
 
Na US inavyoogopa vita karibu na mipaka yake.
Dunia imechangamka kweli kweli! Wajinga wamebaki Afrika
 
Urusi ilikuwa ni USSR lakini hii Russia ni joka la kibisa tu hana lolote na mikwara ndio mingi, mwaka wa tatu ameshindwa kutulia Ukraine hadi amepeleka wafungwa vitani.

Yeye akili yote iko kwenye nyuklia na tayari watu wameshamjulia kwani kila moja ana nyuklia yake hivyo hakuna wa kutishiwa nyau.

Hakuna nchi itakayokubali kuchukua silaha za Mrusi na kisha eti ianze tu kuichokoza nchi yoyote ya Nato kisa wameambiwa na Russia, hiyo ndoto haipo na hiyo nchi haipo na kilichopo ni kwamba vita vya Ukraine lazima sasa vimalizike ili maisha yaendelee na dikteta Putin na genge lake wapelekwe mahakamani The Hague.
 
Jana Putin kawajibu Marekani na wasirika wake.

Kwamba Ukraine haina uwezo na nyenzo za kupigwa makonbora ya masafa marefu bila support ya USA na Allies. Ukraine atakuwa anavuta TU kitufe lakini vingine lazima vifanywe na mataifa makubwa US, UK France n.k. Hii maana yake na wao wameingia vitani rasmi.

Majibu yake ni kwamba Urusi itazipa nchi maadui wa US, UK n.k ambazo zinaweza kuzipiga kupigwa makonbora kwenye maeneo strategic ya NATO.

Pili wataimarisha ulinzi wa Anga kuhakikisha yanaharibiwa makonbora hayo.

Tatu amesema wao matumizi ya nyuklia ni kulinda mipaka yake, uhuru wake na usalama wake hivyo pale usalama wa nchi utakuwa hatarini haitasita kuitumia kama ilivyoandikwa Nuclear doctrine. Na kakumbushia maboom ya nuclear yaliyopigwa japani yalikuwa ni 20kilotan na mdhara yake yalionekana. Tactical nuclear za Urusi ni 70kilotani hivyo madhara yake ni 4times ya Hiroshima na Nagasaki. Hivyo Kila step ya NATO itajibiwaipaswavyo.
Urusi ni kelele nyingi tu, Nagasaki ilikuwa ni kupiga bila majibu, nchi za NATO zina majibu mazuri mpaka hizo nuclear anazozitaja kila vita ikiwa ngumu.
 
Marekani imekuwa ikifuatilia mwenendo wa meli za kijeshi ambazo zimeonekan zikielekea upande wao kwenye visiwa vya Carribean.

Haijajulikana kiuhakika meli hizo za kawaida za kijeshi na zile za kubebea ndege zitatia nanga eneo gani,hata hivyo inakisiwa itakuwa ni Venezuela na Cuba.Mazoezi hayo ya kijeshi yanatarajiwa kuanza wiki chache zijazo.

Katika siku za karibuni kuhusiana na vita vinavyoendelea kule Ukraine na hasa pale baadhi ya nchi za NATO kutoa ruhusa ya silaha zao kutumiwa na Ukraine kupiga popote ndani ya Urusi,nchi hiyo imesema ruhusa hiyo itajibiwa kwa namna stahiki.

Jibu jengine la Urusi kwa hatua hizo za nchi za NATO limetolewa na raisi Vladmir Putin hapo jana,pale aliposema nchi yake itawapa silaha wapinzani wa kila nchi itakayotoa silaha kwa Ukraine ili iipige Urusi.

Russian warships headed to Caribbean for drills as tensions rise over Ukraine, US officials say

Hizo ni biti tu, Urusi ameshazungukwa na NATO pande zote hana ujanja. Tena USA ampe Ukraine nuclear kabisa ila vita iishe mapema.
 
Hitler aliiteka karibu nusu ya Ulaya ila alishindwa , Marekan kafanikiwa kuishawish Ulaya kumkabiri Putin , bado huon hili ni pigo kwa Urusi ? kama Ukraine imemsumbua je Ulaya wakiingia itakuwaj ?

Mtu mweusi huchambua mambo kimahaba sana , kama Putin angekuwa na nguvu angesema ataikabiri ulaya na Marekan directly na sio kupeleka meli tu , maana Macron ashasema atatangaza kuwa Ulaya ipo vitani na Urusi
Hivi unafikir vita vya Urusi na Nato vinaweza kuchukua hata masaa 24 havijaisha? Hakuna cha ndege yoyote au askari atakayeenda front ni mwendo Wa ICBM na Nyuklia zinapishana hewani, ni vita vitakavyochua muda mfupi sana katika historia ya dunia, ache ni ushabiki maandazi dunia imesimamia kuchaa hii
 
Back
Top Bottom