Urusi yatishia kuzuia usambazaji wa gesi kwa mataifa mengine ya Ulaya

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Capture.JPG
Baada ya Urusi kusitisha usambazaji wa gesi kwa Nchi zaPoland na Bulgaria, sasa taifa hilo limesisitiza kuwa itafanya hivyo kwa mataifa mengine ya Ulaya ambayo hayatakubali kulipia gesi kwa fedha ya Urusi (rubles).

Taarifa ya Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amesema uamuzi wa Urusi wa kuchagua sarafu yake kuwa njia ya malipo umetokana na Nchi za Magharibi kutumia Euro katika manunuzi kinyume cha maelekeo na mikataba waliyosaini.

Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen amesema wamekuatana kwa dharura kujadili suala hilo, pia baadhi ya nchi zimeanza kutuma gesi kwa Poland na Bulgaria.

Maelekezo ya kuendelea kutumiwa kwa fedha ya Urusi yametolewa na Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin kutokana na vikwazo ambavyo wamekuwa wakiwekewa na mataifa ya Ulaya hivi karibuni.

Source: CNN
 
1. Humu ndani si mlisema ulaya inanunua gas kwa rubble kimya kimya ili kuficha aibu yao? Sasa mbona peskov anadhihirisha kuwa bado wananunua kwa Euro.

2. Humu ndani mkasema kuwa Ulaya haiwezi kusustain pasipo gas ya mrusi. Endapo wao wanalifahamu hili, iweje wakatae kulipo kwa Rubble?

3. Narudia tena kuzungumza, hiki kitu westerns walishapanga kitambo mno, walishapga hesabu siku wakigomea mafuta na gas ya mrusi ni kipi kitatokea na wataishi vipi.

Sisi hatujui ni kipi kipo nyuma ya pazia, muda utazungumza zaidi.
 
Una daladala yako ya Nissan Civilian, kila siku inakuletea hesabu ya 100,000. Leo abiria wana mgomo wa kupanda gar lako, anatakayepoteza zaidi ni nani? Sio wewe ambaye hukutarajia watagomea kupanda gari lako?

Mpaka wanakugomea unafikiri ni wapumbavu tu? Hawana mbadala wa usafiri mwingine hata kama kwa cost ya juu? Tunaelewa kuwa nchi za Ulaya zimemuacha mbali tu Russia kiuchumi?

Hawa hawawezi kupata gas pengine popote? Hata kama ikawa bei juu, wataimudu sababu uchumi wao unawaruhusu.
 
Kuna watu uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo sana. Katika suala hili hatupaswi kusombwa na hisia. Litazame suala hili kwa kucheki pande zote.

Ukweli ni kwamba vikwazo haviathiri upande mmoja tu. Hivi mnadhani vikwazo vya Magharibi kwa Urusi havijawaathiri wao wenyewe? Cheki yale makampuni ya Amerika yaliyofunga bizness kule Moscow,siyo hasara ile? Sekta ya mafuta na chakula pia imeyumba kidunia.

Kwahiyo, Mrusi kufunga mabomba kwa Ulaya kutawaliza Wazungu sana tu. Kumbuka 40% ya nishati hii huko Ulaya hutoka Urusi. Na ni ukweli ulio wazi hata Mrusi ataathirika sana kwa uamuzi huu. Maana ndiyo vyanzo vyake vya mapato. Ukizingatia tayari yupo vitani na ana vikwazo vingine.

Kwahiyo, ni 50/50 , ukichagua upande unaonekana hujui.
 
1. Humu ndani si mlisema ulaya inanunua gas kwa rubble kimya kimya ili kuficha aibu yao? Sasa mbona peskov anadhihirisha kuwa bado wananunua kwa Euro.

2. Humu ndani mkasema kuwa Ulaya haiwezi kusustain pasipo gas ya mrusi. Endapo wao wanalifahamu hili, iweje wakatae kulipo kwa Rubble?

3. Narudia tena kuzungumza, hiki kitu westerns walishapanga kitambo mno, walishapga hesabu siku wakigomea mafuta na gas ya mrusi ni kipi kitatokea na wataishi vipi.

Sisi hatujui ni kipi kipo nyuma ya pazia, muda utazungumza zaidi.
Na kitu kingine,anawakatia gesi wakati wanaelekea kipindi cha Summer muda mfupi tu ujao,mpaka Summer iishe watakuwa walishaweka sawa jinsi ya upatikanaji wa gesi.Russia akae na gesi yake,hakuna anayeihitaji kwa sasa
 
Na kitu kingine,anawakatia gesi wakati wanaelekea kipindi cha Summer muda mfupi tu ujao,mpaka Summer iishe watakuwa walishaweka sawa jinsi ya upatikanaji wa gesi.Russia akae na gesi yake,hakuna

Na kitu kingine,anawakatia gesi wakati wanaelekea kipindi cha Summer muda mfupi tu ujao,mpaka Summer iishe watakuwa walishaweka sawa jinsi ya upatikanaji wa gesi.Russia akae na gesi yake,hakuna anayeihitaji kwa sasa
Waacheni wapigane vita vyao!
 
1. Humu ndani si mlisema ulaya inanunua gas kwa rubble kimya kimya ili kuficha aibu yao? Sasa mbona peskov anadhihirisha kuwa bado wananunua kwa Euro.

2. Humu ndani mkasema kuwa Ulaya haiwezi kusustain pasipo gas ya mrusi. Endapo wao wanalifahamu hili, iweje wakatae kulipo kwa Rubble?

3. Narudia tena kuzungumza, hiki kitu westerns walishapanga kitambo mno, walishapga hesabu siku wakigomea mafuta na gas ya mrusi ni kipi kitatokea na wataishi vipi.

Sisi hatujui ni kipi kipo nyuma ya pazia, muda utazungumza zaidi.
Mkuu nchi kumi tayari zimefungua akaunti ya rubo na hata hao wanaosaidiwa pia ni gesi ya Russia wanayonunua kwa rubles.
 
Kuna watu uwezo wetu wa kufikiri ni mdogo sana. Katika suala hili hatupaswi kusombwa na hisia. Litazame suala hili kwa kucheki pande zote.

Ukweli ni kwamba vikwazo haviathiri upande mmoja tu. Hivi mnadhani vikwazo vya Magharibi kwa Urusi havijawaathiri wao wenyewe? Cheki yale makampuni ya Amerika yaliyofunga bizness kule Moscow,siyo hasara ile? Sekta ya mafuta na chakula pia imeyumba kidunia.

Kwahiyo, Mrusi kufunga mabomba kwa Ulaya kutawaliza Wazungu sana tu. Kumbuka 40% ya nishati hii huko Ulaya hutoka Urusi. Na ni ukweli ulio wazi hata Mrusi ataathirika sana kwa uamuzi huu. Maana ndiyo vyanzo vyake vya mapato. Ukizingatia tayari yupo vitani na ana vikwazo vingine.

Kwahiyo, ni 50/50 , ukichagua upande unaonekana hujui.
Mbona wewe umechagua upande huku hujui lakini wajifanya wajua?!
 
Na kitu kingine,anawakatia gesi wakati wanaelekea kipindi cha Summer muda mfupi tu ujao,mpaka Summer iishe watakuwa walishaweka sawa jinsi ya upatikanaji wa gesi.Russia akae na gesi yake,hakuna anayeihitaji kwa sasa
Russia ni kama amejiwahi tu, anafahamu anytime hawa jamaa wataachana na Gas yake.
 
Na kitu kingine,anawakatia gesi wakati wanaelekea kipindi cha Summer muda mfupi tu ujao,mpaka Summer iishe watakuwa walishaweka sawa jinsi ya upatikanaji wa gesi.Russia akae na gesi yake,hakuna anayeihitaji kwa sasa
Kwani gesi inahitajika kwa ajili ya baridi tu?
Gesi inayo tumika kukabiliana na baridi ni kiasi kidogo mno , gesi nyingi inahitajika kuendesha viwanda , kuendesha mtambo mikubwa ya kuzalisha umeme na kupikia majumbani na kwenye migahawa.

Kusema hakuna anaye hitaji gesi ya Urusi hapo umetanguliza hisia badala ya uharisia gesi ya Urusi ni muhimu kwa Uchumi wa Ulaya tofauti na hapo utasambaratika kabisa ,na hili viongozi wa Ujerumani wameliongea sana.

Hiyo Poland na Bulgaria hakuna walicho kikwepa maana sasa watarazimika kununua gesi ya Urusi kupitia Ujerumani tena kwa bei kubwa kuliko mwanzo sasa hapo wamekwepa nn?
Gesi ya Urusi ni muhimu kwa Uchumi wa dunia tuache tabia kuchukulia mambo kirahisi.
 
Ukweli ni kwamba mataifa ya magharibi mwanzo yaliona km Russia anataka kutumia kitisho tu kwa Ukraine,lakini hawakutegeme km ataivamia mazima na ndio maana na wao wakaanza kutia mkwara kwa kufanya mazoezi ya kijeshi na Ukraine ili kumuogopesha Urusi,ila hali ilivyozidi kubadilika na intelligence zao kuona kuna ukweli anaweza kuivamia na wakanza kutafuta namna nyengine ya kumtia moyo jamaa yao Ukraine..hata hivi vikwazo walivyoviweka hawakujipanga vizuri kuona madhara gani yatawakuta kwa upande wao,

Na ndio maana kuna baadhi ya nchi za ulaya wanaona hawana sababu ya kuingizwa kwenye mgogoro wenye madhara kwao,ila kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa wakuu na wao wanalazimika kufanya hivyo kwa matakwa ya wakuu wao kwenye muungano huo..

Kuna wachambuzi wa uchumi kutoka mataifa ya ulaya wanakili wazi kwamba hivyo vikwazo walivyoviweka vinawaumiza na wao,kuliko matarajio yao viwaumize waRusi tu.
 
Naaaam.
FRXDfWIVEAUCI-a.jpg
 
Poland na Bulgaria sasa wataanza kuinunua gesi ya Urusi kupitia Ujerumani tena kwa bei kubwa kuliko mwanzo.
Acha tabia ya kichukulia mambo kirahisi.
Wananunua gas kutoka Azerbaijan
 
Back
Top Bottom