JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Taarifa ya Msemaji wa Ikulu ya Urusi, Dmitry Peskov amesema uamuzi wa Urusi wa kuchagua sarafu yake kuwa njia ya malipo umetokana na Nchi za Magharibi kutumia Euro katika manunuzi kinyume cha maelekeo na mikataba waliyosaini.
Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Ursula von der Leyen amesema wamekuatana kwa dharura kujadili suala hilo, pia baadhi ya nchi zimeanza kutuma gesi kwa Poland na Bulgaria.
Maelekezo ya kuendelea kutumiwa kwa fedha ya Urusi yametolewa na Rais wa nchi hiyo, Vladimir Putin kutokana na vikwazo ambavyo wamekuwa wakiwekewa na mataifa ya Ulaya hivi karibuni.
Source: CNN