US na Israel wanatufundisha kuwa na marafiki/ndugu wanaokufaa wakati wa shida tu

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Hadi leo karibu 1/3 ya jeshi lote la navy la US limeshaizunguka Iran kwa lolote ikitokea kajaribu kuishambulia Israel. Watafiti wanasema US imetoa karibu meli zake zote Pacific na zimeenda kukaa kimkakati kwa lolote karibu na iran na israel.
20240828_161943.jpg

Huu ndio urafiki, huu ndio udugu. Kwa mujibu wa professor wa Masuala yanayohusu Iran wa Chuo kikuu cha Tel Aviv Dr. David Menashri anasema " Hatuwezi kuingia vitani na Iran bila US, Hatuna millitary option".
Screenshot_20240828-161917_X.jpg

My take
Katika maisha ni bora uwe na rafiki na ndugu mmoja wa maana kuliko kuwa na marafiki mia machawa, wachawi, wasio na uwezo wowote wa kukusaidia unapokuwa kwenye hatari kubwa kama inayomkabiri Israel.

Kwa upande wa Iran hakuna aliyeupande wake mwenye "commitment" kama aliyonayo US kwa Marekani. Russia anamtumia kisiasa, China anamtumia kimaslahi, Waarabu wanamshangilia kwenye keyboard tu huku kwenye uhalisia wanamsaidia US kuhakikisha Israel haipati madhara yoyote.

Tukiacha udini na uvita, anachokifanya US kwa Israel kina funzo kubwa la maisha ya kila siku huku uswahilini tunakoishi.

Ni hayo tu...
Mtumishi Matunduizi.
 
US hajafanya hivyo kwa Ukraine kwa sababu Ukraine sio rafiki wake ni kibaraka, Chawa au shambadarasa la kusogelea adui yake Russia. Lakini kama Iran watajifanya kushambulia kama Russia walivyofanya kwenye SMO atashambuliwa moja kwa moja na US bila kujali kuna kibali UN au popote. Hapo ni suala la Udugu na urafiki.
 
Hadi leo karibu 1/3 ya jeshi lote la navy la US limeshaizunguka Iran kwa lolote ikitokea kajaribu kuishambulia Israel. Watafiti wanasema US imetoa karibu meli zake zote Pacific na zimeenda kukaa kimkakati kwa lolote karibu na iran na israel.
View attachment 3081451

Huu ndio urafiki, huu ndio udugu. Kwa mujibu wa professor wa Masuala yanayohusu Iran wa Chuo kikuu cha Tel Aviv Dr. David Menashri anasema " Hatuwezi kuingia vitani na Iran bila US, Hatuna millitary option".
View attachment 3081452

My take
Katika maisha ni bora uwe na rafiki na ndugu mmoja wa maana kuliko kuwa na marafiki mia machawa, wachawi, wasio na uwezo wowote wa kukusaidia unapokuwa kwenye hatari kubwa kama inayomkabiri Israel.

Kwa upande wa Iran hakuna aliyeupande wake mwenye "commitment" kama aliyonayo US kwa Marekani. Russia anamtumia kisiasa, China anamtumia kimaslahi, Waarabu wanamshangilia kwenye keyboard tu huku kwenye uhalisia wanamsaidia US kuhakikisha Israel haipati madhara yoyote.

Tukiacha udini na uvita, anachokifanya US kwa Israel kina funzo kubwa la maisha ya kila siku huku uswahilini tunakoishi.

Ni hayo tu...
Mtumishi Matunduizi.
Israel ni kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya marekani nje ya marekani
 
K

iuhalisia urafiki wa US na Israel unakaribia mataifa haya mawili kuwa ni Taifa moja lenye maeneo maili.

Fikiria wayahudi wanaoishi ndani ya Israel ni wachache kuliko Wayahudi wanaoishi USA. Fikiria kuna wayahudi wawekezaji wakubwa sana ndani ya US, kuna wayahudi wengi ni ma-CEO wa makampuni makubwa kabisa ndani ya USA. Kwa myahudi, USA ni nyumbani kwake.
 
Urafiki wa kuua wasio na hatia huku wao wakipiga hesabu za kuishi milele shetani ndio alivyo kuwatamanisha watu na dunia basi
Ni kweli kuna wapalestina wasio na hatia wameuawa. Lakini chanzo ni yale mashetani ya Hamas.

Haya magaidi, hakuna nchi inayoyataka. Na hiyo ndiyo sababu pekee inayoyafanya mataifa kama Misri, Saudia, UAE, Bahrain, Qatar kusimama na Israel dhidi ya Iran. Maana haya magaidi yote yameundwa na Iran. Bila Iran, Mashariki ya kati yote itakuwa na amani, na hata Wapalestina wataishi kwa amani na Waisrael.

Mateso yote ya wananchi wa Mashariki ya kati, kisababishi ni Iran.

Hata mwaka 1948 wakati wa mgawanyo wa ardhi ya Canan ili kuunda mataifa mawili, Israel na Palestine, wapalestina walikuwa wameridhia, malalamiko yao pekee ilikuwa ni wao kupewa arshi isiyo na rutuba na kunyimwa bahari, jambo ambalo tayari UN ilikuwa tayari kulishughulikia. Wakaingia mashetani wakawahadaa kuwa wao watawasaidia kuwamaliza Wayahudi. Iran ikasema kuwa eti wazayuni hawatakiwi kuwepo hapa Duniani. Wapalestina wakadanganyika wakawakubalia hawa mashetani, matokeo yake ikawa ni kupoteza ardhi kila walipoanzisha vita.
 
Screenshot_20240829-075240_X.jpg

Huu ndio Udugu na urafiki. US amerisk hadi kuiacha Taiwan na baadhi ya meli za kivita amezileta mumdhibiti Iran dhidi ya rafiki na ndugu yake Myahudi.

Kuna mengi ya kujifunza kimaisha kutoka katika bond hii kuliko kutoka kwa waarabu, Urusi na China. Akufaaye kwa dhiki.
 
Wapalestina wanajitakia wenyewe. Wanatumika na wenye chuki kwa maslahi yao. Naamini wangeshafika mbali. Suala la kutumiwa na watu wachache kwa maslahi ambayo hayawanufaishi itawatesa sana.

Njia waliyotumia Hamas na Hesbullah na Iran inawaumiza wao zaidi ya wayahudi. Hata kama wakikomaa sana US na Israel wako radhi hiyo ardhi igeuzwe kambi ya Jeshi ili wasafishe njia kisha raia wa Israel warudishwe tena kwa wingi kuliko waliopo sasa.
 
Wayahudi US wako zaidi ya 7M, ila ndio wenye ushawishi mkubwa kuliko makabila mengine yaliyobaki zaidi ya watu 300M.
Kwa sasa ukiigusa Uyahudi umeigusa US moja kwamoja. Yaani unapigana na Ardhi ya Marekani. Ndio maana tunaona kisiasa US anapingana na Netanyahu wakati kijeshi vìfaa vinazidi kusogezwa kuozingira Israel na Iran ili kuwe na Back up kwa lolote.
 
Kacharazwa na Hezbullah mpaa wakajita wao makuku ili waonewe huruma, na US hakuweza kuwaokoa.
Vile ni vitu ambavyo viko ndani ya uwezo wao. Na US anamlnitor kila development ya Hesbullah. Ndio maana wakitaka kumuua yeyote Lebanon wanajiulia tu.
Hata kiongozi wa Hesbullah atakuwa anaishi underground kwenye mashimo ambako huwa anarekodia video zake za kuipiga biti dunia.
 
Urafiki wa kuua wasio na hatia huku wao wakipiga hesabu za kuishi milele shetani ndio alivyo kuwatamanisha watu na dunia basi
Kuua wasio na hatia hata wanaouwawa wakipata nafasi watawau wote hapo Israel. Pia wasio na hatia wanatakiwa kushirikiana na Israel kuwafichua wanaotaka kuwaua waisrael wasio na hatia. Poa hiyo vita imejaa hadaa nyingi sana, wote wayahudi na waarabu wanatumia uongo na propaganda kutuhadaa tunaofuatilia. Kikubwa tunaomba amani, Wayahudi waishi na wao waarabu waiishi. Chukulia Israel ingekuwa haina Iron dome au ingekuwa ni TZ alafu lebanoni ndio Burundi mfano alafu warushe maroketi na drone kqma laki hivi kama wanavyofanya Israel ingebaki mapango tu. Na hiki ndicho maadui wao wanatafuta kufanya wakipata nafasi.

Marafiki wazuri ndio watakusaidia tu. Bora ubaki na mtu mmoja wa maana kuliko kiwa nq rundo la machawa wasio committed na usalama wako.
 
Ndugu US na Israel sio swala la
Urafiki ni swala la Usalama Wa nchi
.. US hamsaidii bega kwa bega Israel sababu ni rafiki.. anguko la Israel ni pigo kubwa kwa US and vice versa.. US kuwa upande wa Israel ni kwa
maslah mapana zaid kwake kuliko Israel wenyewe.. Israel ni proxy muhimu kwa US kuliko zote.. it has nothing to do with friendship.. simply a matter of national security.. ndo maana kila
Mwaka US anatoa pesa kwa Israel kwenye bajet.. maana hiyo pesa inakwenda kwenye mambo mbali mbali ikiwemo research za kila kada.. sio
Kijesh tu.. kwa kifupi Israel ni marekan na Europe ya middle East.. US na Europe hawataruhsu Israel ianguke pale.. at all cost
 
🤝
 
Ni kweli kuna wapalestina wasio na hatia wameuawa. Lakini chanzo ni yale mashetani ya Hamas.

Haya magaidi, hakuna nchi inayoyataka. Na hiyo ndiyo sababu pekee inayoyafanya mataifa kama Misri, Saudia, UAE, Bahrain, Qatar kusimama na Israel dhidi ya Iran. Maana haya magaidi yote yameundwa na Iran. Bila Iran, Mashariki ya kati yote itakuwa na amani, na hata Wapalestina wataishi kwa amani na Waisrael.

Mateso yote ya wananchi wa Mashariki ya kati, kisababishi ni Iran.

Hata mwaka 1948 wakati wa mgawanyo wa ardhi ya Canan ili kuunda mataifa mawili, Israel na Palestine, wapalestina walikuwa wameridhia, malalamiko yao pekee ilikuwa ni wao kupewa arshi isiyo na rutuba na kunyimwa bahari, jambo ambalo tayari UN ilikuwa tayari kulishughulikia. Wakaingia mashetani wakawahadaa kuwa wao watawasaidia kuwamaliza Wayahudi. Iran ikasema kuwa eti wazayuni hawatakiwi kuwepo hapa Duniani. Wapalestina wakadanganyika wakawakubalia hawa mashetani, matokeo yake ikawa ni kupoteza ardhi kila walipoanzisha vita.
Kule Westbank Hamas hawapo mbona hakuna hali nzuri?
 
Umeanza kufuatilia lini siasa za kimataifa hasa zinazo gusa mashariki ya kati ?
 
Wapalestina wanajitakia wenyewe. Wanatumika na wenye chuki kwa maslahi yao. Naamini wangeshafika mbali. Suala la kutumiwa na watu wachache kwa maslahi ambayo hayawanufaishi itawatesa sana.

Njia waliyotumia Hamas na Hesbullah na Iran inawaumiza wao zaidi ya wayahudi. Hata kama wakikomaa sana US na Israel wako radhi hiyo ardhi igeuzwe kambi ya Jeshi ili wasafishe njia kisha raia wa Israel warudishwe tena kwa wingi kuliko waliopo sasa.
Acha nikuulize swali moja jepesi.

Waafrika wakiwemo baba wa babu yako, bibi wa bibi yako walijitakia wenyewe kuwa katika ukoloni ?
 
View attachment 3081819

Huu ndio Udugu na urafiki. US amerisk hadi kuiacha Taiwan na baadhi ya meli za kivita amezileta mumdhibiti Iran dhidi ya rafiki na ndugu yake Myahudi.

Kuna mengi ya kujifunza kimaisha kutoka katika bond hii kuliko kutoka kwa waarabu, Urusi na China. Akufaaye kwa dhiki.
Hayo ni mapambo tu hawakuweza kuziona Katyusha za Hezbullah wataziona Hypersonic za Iran.
 
Acha nikuulize swali moja jepesi.

Waafrika wakiwemo baba wa bau yako, bibi wa bibi yako walijitakia wenyewe kuwa katika ukoloni ?
Ndio. Wangetumiq akili zao vizuri na rasilimali zilizopo africa sisi ndio tulitakiwa kutawala wazungu sio wao kututawala.
 
Back
Top Bottom