USA hata kama akasimama pekeake dhidi ya dunia nzima kivita, bado tutapigwa tu

USA hata kama akasimama pekeake dhidi ya dunia nzima kivita, bado tutapigwa tu

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
Kuna watu wana uelewa mdogo sana kuhusu uwezo wa USA kiichumi, kivita, silaha, technology. Ukweli unabaki pale pale kwamba hakuna taifa lolote linalomsogelea MAREKANI kwenye:

a) Uchumi
b) technology
c) silaha
d) Vita
e) Biashara

Uwezo wa Marekani ni mkubwa mno kwenye hizo nyanja.

Kama ingetokea kwamba dunia nzima tukapigana na USA, bado jamaa watashinda hiyo Vita.

USA kwenye full scale war, hana mpinzani. Jeshi lake liko kila Kona ya dunia. Wana silaha za kisasa na wako vizuri Sana kwenye innovation

Uchumi wao ni mkubwa mno, USA anaweza kupigana full scale war kwa muda mrefu bila kuteteleka.

Nawashangaa Sana watu wanaosema Russia Ina uwezo mkubwa kuliko USA. Najiuliza ni mahaba au kweli wanamaanisha.

Uwezo wa USA dhidi ya Russia ni mkubwa mno.

Mfano mmoja ni huu, uchumi wa California ni mkubwa kuliko uchumi wa Russia Kama taifa. Uchumi wa Russia ni 2 trillion USA GDP. Uchumi wa USA ni almost 29 trillion USD. Russia anawezaji kupigana na taifa lenye nguvu kiasi hicho?

Wengine wanasema Russia ana nuclear bombs, Swali, Nani aligundua nuclear. Nani amewahi kutumia nuclear weapons?

Putin anajuwa Sana uwezo wa ki nuclear wa USA. Anajua vizuri kwamba akitumia nuclear tu, utakuwa ndio mwisho wake

Vitu vingine tuache mahaba. Tujifunze ya mwaka Jana ya Nancy Pelosi. Tulipata jibu sahihi
 
Hebu tuache porojo.. ni vita gani ambayo amewahi kupigana peke yake akaishinda.

Vita ya Vietnam alipigwa hadi akajiondoa, Afghanistani aliwakuta taliban na kawaacha yani sawa ameshindwa, pale Iraq alikuwa na collabo.

Sasa unaweza kusemaje akisimama na dunia nzima atashinda au movie zinakuchanganya mzee?

Hitler tu alishindwa na teknolojia aliyokuwa nayo kipindi kile. Hivi unajua wanasayansi wa Nazi ndio aliwachukua US wengi wakawa viongozi wa vitengo ikiwemo NASA, maana walikuwa ni wabobezi wa rocket propellant?
 
Anachezeshewa kichapo na waasi wa Yemen balaaa


1717105722201.jpg
 
Mm nilipo fungua Uzi nikajua labda utatuelezea na kudadavua kinaga ubaga nguvu aliyo nayo USA kitakwimu mitambo aliyo nayo kama vile ndege za kivita, manoari, aircraCarriers compare to the rest of the world. Kumbe ni stori za kwenye vijiwe vya kahawa ?.
 
Watu wanaakili ndogo hawajui maana ya vita na mapambano dhidi ya kikundi fulani.

Kwa mfano USA angekuwa ametangaza vita kamili dhidi ya vietnam tungekuwa tunaongeea kitu kingine.

Kvp? Kwenye vita kamili haki za binadamu,sijui huyu ni mwanajeshi huyu sio hamnaga wanachang'anywa wote.
Ni hivyo hivyo kwa Russia akiamua kupiga ukraine bila kujali sijui raia nakadhalika hata bakiza kitu.

Tuje upande wa US vs Russia hapa ni mbingu na ardhi!

Hitler tu na jeshi lake ambalo halikuwa na branches wala nn liliimidi vita miaka 6?

Mwenye akili ajiulize je? Vp US wenye military bases all over the world?

Siitakuwa balaa plus uchumi plus well intergrated intelligence agencies.
 
Kwa mfano USA angekuwa ametangaza vita kamili dhidi ya vietnam tungekuwa tunaongeea kitu kingine.
Kvp? Kwenye vita kamili haki za binadamu,sijui huyu ni mwanajeshi huyu sio hamnaga wanachang'anywa wote.
Ni hivyo hivyo kwa Russia akiamua kupiga ukraine bila kujali sijui raia nakadhalika hata bakiza kitu.
Vita ya USA na Vietnam ilikuwa vita kamili kabisa....hata vita ya Sasa ya Urusi na Ukraine ni vita kamili.
 
Mifano ya marekani kushindwa vita mbona ipo mingi sana mkuu. Vietnam na Cambodia walishindwa , Afghanistan wameshindwa Somalia hapo jirani zetu operation Black hawk down walichinjwa kama njiwa miili ilitapakaa Mogadishu mpaka leo marekani hajawahi kukanyaga Somalia. Mifano ni mingi sijui unazungumzia vita gani
 
Kuna watu wana uelewa mdogo sana kuhusu uwezo wa USA kiichumi, kivita, silaha, technology. Ukweli unabaki pale pale kwamba hakuna taifa lolote linalomsogelea MAREKANI kwenye....
Wamarekani washenzi sana, wao ndio wenye dola wanachokifanya ni ku print hizo dola kisha mnapewa watanzania mnaambiwa msaada, mara dola hizohizo zaku print zinaenda Ukraine, mara zinaenda Israel, mara wapi sijui....
 
Marekani ina mashirika zaidi ya 10 ya Intellejensia, Wizara yao nishati yenyewe ina Shirika lake la Ujasusi.

Mtu anayedhani shit holes countries zinaweza kupigana na Marekani ni mjinga sana na hana strategic understanding ya mambo ya Dunia.

Hadi sasa only Russia na USA ndio wana Nuclear TRIAD, vita kubwa kuliko zote na ya hatari ni Marekani na Russia. Na hiyo vita atakaye pigwa in coventional war ni Russia.

Sababu kubwa Russia hataki Ukraine wawe NATO ni kuogopa Jeshi kubwa kama la Marekani liwe mpakani mwake
 
Umenikumbusha mabishano ya utotoni; Ronaldo (R9) peke yake akicheza na taifa stars anashinda 😅

Anyway, kila mtu duniani ndoto yake ni kufika nchi ya maziwa na asali- USA 🇺🇲🇺🇲🇺🇲. Marais wa Ulaya wenyewe wanacheza green card lottery.
 
Back
Top Bottom