Gwappo Mwakatobe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2019
- 1,730
- 2,230
Kuna watu wanatubu madhambi yao kwa watu, si kwa Mungu. Wanaamini anasamehe kupitia wao. Ila ukimkosea mtu unamwomba msamaha moja kwa moja akusamehe makosa yako kwake.Kutubu kwa binadamu na sio kwa Mungu ni aina gani ya kutubu?
Kwa Mungu unatubu kwake kwa maana ya kujutia udhaifu wa moyo wako. Kumbuka, kabla hujamkosea mtu, unakuwa umetenda dhambi moyoni kwa Mungu. Anayeiba au kuzini hashtukizi ghafla, bali huanza mawazo ya wizi au uzinzi moyoni kabla ya kutenda. Mungu anaona ya moyoni asikoona mwanadamu yeyote. 1 Samweli 16:7