Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Kwanini umeassume hajui? Ukimsoma vizuri unaona ni mtu asiyejua?

Punguza kuwa sensitive, ATC si ukoo wa mtu.
Hajui sababu hajengi fact ndege alixopanda kwanza za hadhi gani,status na season gani na alikata kipindi cha muda gani ksbla kupanda hizo ndege zake koko na alipanda class gani ya ndege ndege brand aina gani za kikorea,kirusi ,kichina au Airbus au Boeing,Hiyo route kutoka hapo Airport alipanda demand ikoje kutoka hapo kwenda huko aendako na je hixo ndege alipanda hizo route ni mpya kwao kuwa walikuwa na bei za chini za promotion nk?

Swali lake nonsense kuna vitu vingi anatakiwa kufafanua sio hiyo generalisation yake anaonyesha hajui hata kama alipanda matongotongo ya ushamba bado yako machoni mwake
 
I second you. 🫡
 
Hoja yako ni nzuri na ina mashiko lkn sio sawa kulinganisha bara la africa na mabara mengine, vilevile ungeweza kulinganisha kwa umbali/kilometa/Neutical mile ingekuwa sawa, nchi ulizotulinganisha nazo yawezekana mafuta wao wanapata lita moja ni kwa senti 200 na sisi ikawa ni kwa dollar 10 yawezekana wao service ya kwaida ya ndege ni dollar 20,000 lkn sisi ni dollar dollar elfu 70.
 
Tanzania imewahi kuona uwepo wa hizo unazozitanabaisha kama low budget airlines, ni nini kilipekea kusitisha huduma zake ilhali zilikuwa zinatengeneza faida?
Community airlines ilikuwa ndege ya mumiliki wa Star TV ANTONY Diallo ilikuwa moja tu na alinunua ndege used iliyokuwa grounded ya shirika la Air Tanzania waliyoamua kuiuza kwa mnada akaifufua akaianzishia shirika la ndege la Community Airlines lakini matengenezo baadaye yalimshinda akafunga kampuni kwa kushindwa kuifanyia service

Fast Jet ilikuwa shirika la ndege la vigogo serikallini wakishirikiana na vibaka wa nje
Mmoja aliyekuwa na mkono wake humo ni waziri Masha wakawa hawakawa hawalipi kodi stahiki.

Walipoanza kudaiwa kodi wakajitia ohh tutalipa .Siku hiyo ndege zote zikaruka zikakimbia nchi asubuhi watu wanaenda ofisi yao imefungwa kuanzia wafanyakazi wakabaki wameduwaa waliokata tickets hadi leo ticket wanazo hawakusafiri na ofisi ziliifugwa ghafla pale mtaa wa samora sio na serikali walifunga wenyewe na kutoroka



Tax evasion hakuna ali
 
Tatizo wanataka faida kubwa badala ya kuongeza miruko na seat cap
Washushe bei kama Fastjet kisha miruko iwe mingi hata miruko 100 kwa siku.
Dar Mwanza iwe 150,000/ return 280,000/
Dar Dodoma iwe 120,000/
Dar Mbeya iwe 150,000
Dar Kia iwe 150,000/

Hapo watakuwa na uhakika wa kurusha ndege kila baada ya Masaa 2
 
Sahihi factors nyingi mno anaongelea tu general kama layman tu
 

Pamoja na hayo yote, bado usafiri wa ndege Tanzanaia ni gharama sana tusitake kuhalalisha huu uharamia, haijalishi unawahi kukata tiketi kwa muda gani tofauti haiwezi kuwa kubwa kiasi hicho tena hasa safari za ndani, Kuna option Kwa safari za ndani hazimati sana labda international flight.

Utofauti mkubwa wa gharama unakuwa kwenye aina ya shirika, class unayokata, huduma za ndani, muda wa kusubiri connection, pahala unapofanyia connection nk, hii inafanya kazi sana kwenye international flight na sio hizi local flight.
Mfano kwenda Europe kutoka Tanzania, ukapita DXB na Emirates, au Hamad na Qatar au Bole Addis haiwezi kuwa sawa na direct connection ya KLM amsterdam au BA kutoka Joburg.
 
Pascal Mayalla pitia hapa...
 
Sahihi factors nyingi mno anaongelea tu general kama layman tu
Caracas to Madrid
4347 miles / 6995.82 km / 3777.44 nautical miles.

Bukoba to Dar es Salaam
638 miles / 1027 kilometers / 555 nautical miles.

So the other fact inayobaki ni mafuta na services ndiyo ina-determine gharama?!
 
Caracas to Madrid
4347 miles / 6995.82 km / 3777.44 nautical miles.

Bukoba to Dar es Salaam
638 miles / 1027 kilometers / 555 nautical miles.

So the other fact inayobaki ni mafuta na services ndiyo ina-determine gharama?!
Venezuela uliko uwanja wa ndege huo wa carcas ni wazalishaji wakubwa wa mafuta yakiwemo ya ndege sisi tunanunua nje hatuzalishi domestically kama wao hivyo haiwezekani utulinganishe nao
 
Kuna wakati mwingine una lazimika kusafiri kwa dharula. Utakataje mapema?
 
Venezuela uliko uwanja wa ndege huo wa carcas ni wazalishaji wakubwa wa mafuta yakiwemo ya ndege sisi tunanunua njev hatuzalishi domestically kama wao
Oke,

Seoul, South Korea to Oslo, Norway
4797 miles / 7720.02 km / 4168.48 nautical miles.

Bangkok, Thailand to Frankfurt, Germany
5599 miles / 9011 kilometers / 4866 nautical miles.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…