Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Nahisia kali sana juu ya hili suala ndani ya nchi, kuna mifumo engineered kuwafanya watu wakakaa na kuona umaskini, ukosefu wa standard nzuri ya maisha ni hali ya kawaida.

Hili halikubaliki!
Shida ya Tatizo hili inaanzia mbali:
1.SERA zilizopo zimeshindwa kutafsiri mabadiliko ya Dunia(Tulitoka kwenye ujamaa kuja soko huria, mfano kuagiza gari,kodi na tozo ni sawa na kununua gari 2,ni kama vile ni anasa kumiliki gari).
2.Mamlaka za usimamizi kushindwa kudhibiti anguko la thamani ya shilingi.
3.Mamlaka za upangaji wa bei na tozo mbalimbali kupanga bei kuongezeka hakuna siku wamekaa kushusha gharama(mfano Nauli ya daladala na mabasi,hata bei mafuta kwenye soko la dunia ikipungua,Mamlaka husika hazipunguzi bei) ,ni kama vile haya mambo yanafanywa kuwanufaisha wachache.
4.Mwekezaji akipanga bei ndogo ya huduma na bidhaa anajikuta anapigwa vita(mfano FastJet,),badala ya kujifunza kwa wenye uwezo wa kusha bei tunaleta zengwe na kuwakatisha tamaa.
5.Bado sheria za kodi hazina mtazamo wa "viwango vidogo vya kodi,wengi ili walipe "
 
Mambo haya yote na mengine mengi ambayo hujayaandika yamesababishwa ccm
Wanaiba sana pesa za uma. kupanda ndg kwenda na kurudi mara4 ni mtaji mjubwa kabisa wakuanzia biashara
ndogondogo na hii ccm wanajua tukitajirika wengi hatuta wasikiliza kwa porojo zao
 
Ni kweli kabisa kuna safari za mashirika mengine ya ndege Afrika kutoka nchi moja kwenda nyingine ambayo inachukua takribani masaa 4 angani lakini nauli yake ni cheap sana si zaidi ya dollar 150.

Na mara nyingi ndege za ATCL kwa viwango hivyo vya nauli seats nyingi zinakuwa wazi. Ndege ina siti zaidi ya 120 badala yake abiria wanakuwa ni 44 tu.

Naona kabisa hasara ni kubwa mno.
 
Nchi hizi za ulimwengu wa 3 Bado zimejenga Uchumi wa kikoloni na unyonyaji.

Harafu sio Tzn pekee ni African yote.

Ukitaka kwenda Lagos kutoka Dar gharama ni kubwa Bora utoke Dar Hadi London.
 
Wanasema kodi ya viwanja vya ndege Tanzania ipo juu sana ndio maana wageni wengi wanashukia Nairobi harafu wanaletwa na Coaster kutoka Nairobi au mwenye kampuni ya Utalii anapeleka gari lake Nairobi nadhani tuna shida sehemu sio bure ukishakata hiyo Tiketi ukaangalia hiyo kodi na bei ya nauli zimetofautiana kidogo sana..
 
Sasa hapo utashangaa Fast Jet alifanya kazi nchi hii hii lakini bei ilikua chini na hakuendesha shirika kwa hasara. Watu walikula sana mwewe Mwanza Dar kwa siku zilikua safari 4 hivi kwenda na 4 kurudi na zote ndege zinajaa abiria
Kuna mda ukitafakari hupati majibu kabisa kuna mambo mengi ya hovyo sana
 
Kuna risk kubwa sana kwa pilots unaendesha ndege mbovu, au zisizo brand za abiria za made in Korea au China etc roho mkononi

Compensation ya mshahara lazima iwe kubwa kwa pilots na cabin staff
Acha uongo china wameanza kuzalisha ndege za majaribio recently wapo kwenye majaribio tena bado hawajaanza kufanya mass production acha uongo

Ndege nyingi za abiria zinanazalishwa na boeing au airbus
Mfano korea hawana historia yeyote ya kuzalisha ndege
 
Nauli ya ndege Dar mwanza ni kama Dar Dubai. Tanzania shida iko kwenye idadi ya ndege.

Tuko Milioni 65+ lakini ndege hazizidi 28, hizo hizo zitumiwe na viongozi wa serikali, hizo hizo wananchi wa kawaida.

Shida iko kwenye idadi ya ndege zilizopo na mahutaji ya ndege kua makubwa sana lakini fleet yetu bado haikui kuendana na mahitaji makubwa ya usafiri wa anga.
 
Dar - Kigoma round trip 750,000/=. In short tuna nchi la hovyo sana! Viongozi wetu wote ni average people wala hawana tifauti na mwananchi wa SangaMwalugesha! Au Itongolyangamba! Fast Jet alitaka kuleta mabadiliko akapiga spana!
 
FAST JET warudi haraka sana
 
Wengi wangapi? Malizia
 
Hii
Hii inch imejaa wezi, Ina viongoz wa ajabu sana, rushwa, ufisadi na Kila Haina ya uhuni, na wanainch hawana habari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…