Shida ya Tatizo hili inaanzia mbali:Nahisia kali sana juu ya hili suala ndani ya nchi, kuna mifumo engineered kuwafanya watu wakakaa na kuona umaskini, ukosefu wa standard nzuri ya maisha ni hali ya kawaida.
Hili halikubaliki!
1.SERA zilizopo zimeshindwa kutafsiri mabadiliko ya Dunia(Tulitoka kwenye ujamaa kuja soko huria, mfano kuagiza gari,kodi na tozo ni sawa na kununua gari 2,ni kama vile ni anasa kumiliki gari).
2.Mamlaka za usimamizi kushindwa kudhibiti anguko la thamani ya shilingi.
3.Mamlaka za upangaji wa bei na tozo mbalimbali kupanga bei kuongezeka hakuna siku wamekaa kushusha gharama(mfano Nauli ya daladala na mabasi,hata bei mafuta kwenye soko la dunia ikipungua,Mamlaka husika hazipunguzi bei) ,ni kama vile haya mambo yanafanywa kuwanufaisha wachache.
4.Mwekezaji akipanga bei ndogo ya huduma na bidhaa anajikuta anapigwa vita(mfano FastJet,),badala ya kujifunza kwa wenye uwezo wa kusha bei tunaleta zengwe na kuwakatisha tamaa.
5.Bado sheria za kodi hazina mtazamo wa "viwango vidogo vya kodi,wengi ili walipe "