Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Usafiri wa Anga Tanzania chini ya ATCL ni ghali kuliko hata usafiri kutoka Bara moja kwenda lingine kwa mataifa mengine

Nadhani moja ya sababu ni " ECONOMIES OF SCALE. Mifano uliotoa wanatumia ndege zinazibeba watu zaidi ya 250 and almost full booked. But still, Atcl na wenzake, nauli zipo unfairly high.
ujinga ni kutumia ndege za kurushwa masafa ya kimataifa kwa safari za ndani. kingine pale atcl kuna lundo la wafanyakazi waliajiriwa kiholela bin kujuana bado ufisadi. ukiwaza mambo ya ukimani utachanganyikiwa.
 
Usafiri wa anga nchini Tanzania ni usafiri ghali na wa gharama ya juu hadi kufikirisha ukilinganisha na mataifa mengine yakihusisha na safari kutoka bara moja hadi bara jingine.

Usafiri wa anga chini ya Air Tanzania kwa kiasi kikubwa ukisaidiana na Precision Air unaonekana kama umewalenga wanasiasa na wafanyabishara wakubwa.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Caracas, Venezuela hadi Madrid, Uhispania ni takriban $290 sawa na TZS 864,311 - hiyo ni nchi hadi nchi kwenye mabara mawili tofauti.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Bukoba, Tanzania hadi Dar es Salaam, Tanzania ni takriban TZS 631,000 sawa na €212 - hiyo ni mji hadi mji ndani ya nchi.

Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Fort Lauderdale, USA hadi Cartagena au Barranquilla, Colombia ni takriban $69 sawa na TZS 189,000 - hiyo ni nchi hadi nchi.

Safari ya ndege ya unganisho kutoka Mbeya, Tanzania hadi Mwanza, Tanzania ni takriban 1,100,000 sawa na $403 - hiyo ni jiji hadi jiji ndani ya nchi.

Hii ni mifano midogo sana maana kuna safari za kutoka Seoul, Korea Kusini hadi Barcelona kwa TZS 1,023,000.

Swali langu ni kwanini ATCL na washirika wake ndani ya nchi wana gharama kubwa katika usafirishaji! Je wanatumia teknolojia na mifumo tofauti na ghali ukilinganisha na mataifa mengine?

Ni sababu zipi za msingi zinazofanya flights za ndani ya nchi kuwa ghali maradufu kiuhalisia na hata ukilinganisha na mataifa mengine?

Ni maelekezo kutoka juu kuendelea kuwafinya watanzania wazidi kuishi kijamaa?

JamiiForums naomba msaada wa kuwatafuta ATCL, Mamlaka ya Anga na Wizara ya Uchukuzi watupatie ufafanuzi na statistics zinazohalalisha gharama za usafiri wa anga.
Ni wapi ulisoma kuwa sababu za kuanzisha upya Air Tanzania zilikuwa ni kushusha bei za nauli ya ndege?
 
Kufariki kwa Magufuli lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa nchi hii
 
Mindset za watawala wanaona usafiri wa ndege ni anasa, hivyo hizo anasa wanatakiwa kuzifaidi wachache. Hii pia ipo kwenye umiliki wa magari hapa nchini, inakuaje TRA hujatengeneza gari lakini unachukua kodi sawa na bei ya kununulia hilo gari!!. Nchi hii watu tunafanywa maskini kwa makusudi kabisa. Watawala wameona sisi kuendelea kuwa maskini ndio mtaji wao kuendelea kutawala na kujilimbikizia mali ili kila siku tuwaabudu wao kama miungu watu.
Sema hapa kwenye magari hata JPM alifeli, yaani aliendelea kuifurahia kodi kubwa. Magari kodi ilitakiwa iwe sio zaidi ya 1/3 ya bei ya manunuzi. Punguza kodi, wengi wanunue magari upate kodi nyingi na maduka ya vipuri yaongezeke, unakua umekuza na ajira.
 
Fastjet si alikimbizwa ili watunyonye vizuri. Kutoka kumlaani kabaila mpaka kuwa kabaila.

Hapa tatizo serikali huwa hailipi ghalama zake, viongozi wanasafiri Bure tu bill zikija zinatupwa kabuni, inabidi wewe msafiri tukunyonye kufidia hasara ya viongozi.

Kumbuka mdaiwa sugu ni serikali, Hata World Bank and IFM wanalijua hili.
 
Inasikitisha sana flights hazigusiki ndani ya nchi – zinaonekana ni kwa ajili ya watu baadhi.

Leo hii wakipunguza gharama na kuongeza flights, kuna faida kubwa shirika litaingiza na kuchagiza uchumi.
Kweli kabisa, kuna abiria wengi tu hawajawahi kupanda tena ndege baada ya Fast Jet kufurumushwa. Yaani ATCL wangezidiwa na abiria.
 
Hii ndiyo shida ya monopoly, ATCL hakutaka ushindani zikafanywa figisu kuwatoa players wengine kwenye soko ili abaki mmoja tu atawale

Huko ulipotolea mifano unakuta mashirika yapo mengi kwa hiyo bei itakuwa nafuu maana watakuwa wanashindana kwenye bei ili kupata wateja hapa kwetu huna option aliyepo atapanga bei atakayo, hutaki ni mwendo wa magufuli pale ukachague ally's, kisbo, maning nice nk
 
Back
Top Bottom