The golden
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 1,382
- 2,582
Kutokana na hali mbaya ya uchumi, watu wengi tunatumia usafiri wa basi kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Mabasi ya siku hizi yanakuja na Tv set. Wamiliki wa mabasi haya wana tabia ya kufungua mziki kwa sauti kubwa sana wakidhani labda ni burudani kwa abiria wote waliomo ndani ya basi husika.
Kiwango cha sauti kinapokuwa kikubwa hugeuka kuwa kero hasa unapokuwa na safari ndefu mfano kutoka Dar mpaka Mwanza. Siyo kila mtu anahitaji kelele hizo. Wapo watu wanasafiri na Tablets au vitabu wangependa kujisomea ndani ya basi wakiwa wanasafir safari ndefu kama hiyo. Wapo watu wanaopenda utulivu na ukimya ili watafakari mambo yao wakiwa safarini, hivyo mziki wa sauti ya juu ni kero kwao.
Ningependa kushauri wamiliki wa mabasi kuweka headphones kwenye kila siti ili anayependa kusikiliza mziki afanye hivyo kwa manufaa yake binfsi. Mazingira ya chombo cha usafiri yasigeuke kero.
Napenda kumaliza kwa kusema kelele ina uhusiano mkubwa sana na umasikini, ujinga.
Jiulize maswali haya:
1. Kwa nini kwenye usafiri wa ndege hakupigwi mziki mkubwa? Halafu Angalia aina ya watu wanaopanda ndege.
2. Kwanini maeneo wanaoyoishi watu wenye mafanikio hayana makelele? Angalia Masaki, Osterbey au Upanga halafu linganisha na maeneo wanaishi watu masikini.
3. Kwanini baa au sehemu za kupumzika wanazoenda watu waliofanikiwa hazina mziki mkubwa? Halafu linganisha na baa za makabwela.