Mkanganyiko kukanganya
JF-Expert Member
- Jun 26, 2022
- 1,204
- 5,053
Siyo kila mtu anataka hizo Comedy. Waweke Headphones anayetaka asikilize yeye binafsi.Mkuu kwa upande wa movie hapo kidogo unataka kupotoka ile ni comedy ya kibongo ifike mahali tupende vya kwetu bongo movie mmediss sasa hata comedy mkuu?
😁😁😁Wanaeka mamuvi yametafsiriwa afu ya zamani
Ujinga mtupuSio muziki tu na zile movie zao za kina Mkojani na Tin white, yaani inakera sana au wanaweka movie za kutafsriwa!
Sasa unapendekeza ni wewe.Fikra zako za kiwiziwizi tu.Wakiweka headphones zitakuwa zinaibwa kila siku, au umetusahau wabongo na tabia zetu
HaviingilianiNi ukweli usiopingika. Tafadhali Mamlaka inayohusika ifuatilie kero hii. 'Noise pollution' inayosababishwa na sauti iliyopitiliza kiwango ndani ya baadhi ya mabasi yetu inakera na kuathiri 'comfortability' na afya za abiria.
Sababu mojawapo ya kufunguliwa sauti kubwa ndani ya mabasi haya ni kuhakikisha 'speed limit alarm' haisikiki wakati imefikiwa, hivyo kukuta dereva anaendesha mwendo wa kasi uliopitiliza kiwango kilichotegeshwa i.e. 80Km/hr
Unazungumza na sheikh unajiuliza jee yuko baaKuna Basi la IMANI Dar - Mbeya , sikutegemea kuwa na nyie mnaweka sauti kuuubwa hivyo, basi lenu la kiistaarabu,
rekebisheni sauti, yaani kadiria kwamba mtu anasikia kitu kinachoendelea ila hakereki. yaani hata akitaka kuongea na simu isiwe shida, sasa unakuta unaongea na simu mpaka mtu anakuuliza '' uko wapi hapo ? "
kharaam. Hata hawamuogopi Mungu anayeona machafu hayo.Ikitokea ajali watasema nini ?Music juu hasa jioni,mtu kuchoka na mizunguko, stress za maisha na smtmz video za nusu uchi wale wadada wa uswazi wanaobenua matako juu wakiyachanganua!
Astalahaleee!!
Smtmz uko na watu wa heshima "wazazi,wakwe,wakuu wa kazi" video kanga moko iliyopigwa maji wala wala, wadada wako bize wameinama wengine wamechana misambakharaam. Hata hawamuogopi Mungu anayeona machafu hayo.Ikitokea ajali watasema nini ?
Ziwekwe headphonesKwenye basi kila mtu ana hobi yake, Kuna wanaotaka mziki tena sauti kubwa na wengine hawataki kabisa. Labda kuwe na demokrasia, wanaopenda mziki wakiwa wengi wapewe haki yao, wakiwa wachache mziki uzimwe kabisa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa teknoljia ya sasa na mifumo ya kutunza data iliyopo , huwezi kuiba headphones kwenye Bus usipatikane. Tiketi za siku hizi ni Electronic. Huwezi kijificha.Hatujafika huko bado, watz wengi si wastaarabu hata kwenye maisha ya kawaida tu, hizo headphones zitaibiwa zote na kuharibiwa...Kama hutaki kelele ongea na konda umueleze unavyojisikia kwa sababu na naamini asilimia kubwa ya abiria wanapenda vyote vinavyooneshwa kwenye basi hasa michezo, utakuta Basi zima linacheka.