Nini siku sita... nakumbuka long time, wakati nipo mdogo kabisa... Bi. Mkubwa alikuwa na tabia akisafiri kwenda bush, anahama na duka kabisa kwa ajili ya wazazi wake... atatoka na viroba vya sukari, mchele, unga, maharage, n.k! Safari moja tukazima mitaa ya Rufiji hapo! Kiroba cha mchele kiliishia hapo hapo... ingawaje sikumbuki vizuri lakini, safari ya Dar-Lindi ya saa sita ilitufanya tubaki pale almost two weeks... mbele ya safari hakuendeki kurudi ulikotoka haiwezekani! Ilikuwa ni kawaida kwa bi. mkubwa enzi zile kusafiri akiwa ama na jiko la mchina au stovu (watoto wa cku hizi cjui kama wanayafahamu haya majiko!)...Sasa kutokana hali hiyo nikakumbuka safari yangu ya 1995 kutoka huko Kusini kuja Dar ambao tulisafiri na lory kwa siku sita, usafiri mwingine ilikuwa meli siku mbili majini, duh Kusini tumetoka mbali.