Usafiri wa Dar - Mtwara umenikosha roho

Usafiri wa Dar - Mtwara umenikosha roho

Sasa kutokana hali hiyo nikakumbuka safari yangu ya 1995 kutoka huko Kusini kuja Dar ambao tulisafiri na lory kwa siku sita, usafiri mwingine ilikuwa meli siku mbili majini, duh Kusini tumetoka mbali.
Nini siku sita... nakumbuka long time, wakati nipo mdogo kabisa... Bi. Mkubwa alikuwa na tabia akisafiri kwenda bush, anahama na duka kabisa kwa ajili ya wazazi wake... atatoka na viroba vya sukari, mchele, unga, maharage, n.k! Safari moja tukazima mitaa ya Rufiji hapo! Kiroba cha mchele kiliishia hapo hapo... ingawaje sikumbuki vizuri lakini, safari ya Dar-Lindi ya saa sita ilitufanya tubaki pale almost two weeks... mbele ya safari hakuendeki kurudi ulikotoka haiwezekani! Ilikuwa ni kawaida kwa bi. mkubwa enzi zile kusafiri akiwa ama na jiko la mchina au stovu (watoto wa cku hizi cjui kama wanayafahamu haya majiko!)...
 
Aiseee kitamboooo sana.
....kuna siku tulikimbizwa na mbwa mitaa ya shangani kule nyuma ya Parish...break ya kwanza kiyangu sokoni....tulikomaje

Hahaha hata shangani ya Majumba saba kule kulikuwa na mbwa sana na kule shangani pale mifugo kwa marehemu Komba palikuwa na kunazi nyingi ila wamezungusha fence haha
 
ila twende mbele na kurudi nyuma, wasichana wa kota za bandari walikuwa malayaaaaa......
qn of sheba wewe ulikuwa kota za wapi?....maana Mtwara karibia yote imajaa kota

Huo ni ukweli aisee na walikuwa wanaongozaga kwa scandal mji mzima unamjua fulani kafanya nn na hv mji ulikuwaga mdogoo.

Me nilikuwa Indian Quarters palepale kwenye zile kota za Vigae. Kipindi cha embe tunakoma watoto wenyewe kwa wenyewe tunarusha mawe mpaka tunavunja vigae. Nilikuwa Maeneo ya kwa Mtingita au kwa Msaki kama unawakumbuka maana walikuwaga maarufu enzi hizo ule upande wetu.
 
Last edited by a moderator:
mpaka leo watoto wanaenda kuokota kunazi huko na pale maeneo ya ttc

Kunamiji mingine nimeshangaa hawali kunazi wanaona matunda ya ajabu hahaha Zanzibar kuna sehemu panaitwa Mkunazini nashangaa kuna mtu alikuwa hajui kama yale matunda yanaliwa kapiga picha tu nikamwambia aonje ajionee utamu hahaha. Dodoma pia kuna kunazi nyingi ila wenyeji hawajui kama zinaliwa, me hata leo hii niikute kunazi mji wowote hata siachii najikumbushia enzi.
 
Ni kupanga na kuchaguwa matumizi ya fedha za Tanzania alizokabidhiwa kuzisimamia, ndiyo maana ya kuwa kiongozi.

Wa kabla yake walifanya nini?

Wewe ulizaliwa na pesa yako. Wacha kiherehere.

Nashindwa kuelewa tatizo ni nini? Kama ni kweli aliyesimamia haya mafanikio ni X au Y, unataka tufanye nini? La msingi ni kujikita kwenye mada iliyopo badala ya kuihamishia katika kusifia watu. Badala yake ianzishwe mada nyingine kujadili nani kaleta maendeleo haya yaliyopo kwa sasa Mtwara. Michango yetu ni vema ikajikita katika kichwa cha habari badala ya kutuhamisha kwenye mada yetu ya kijamii na kutupeleka kwenye mambo ya Ubungo Plaza.
 
nilivyofika mtwara mara ya kwanza mwenyeji wangu akaniambia ngoja nikakuonyeshe coco beach!!! dah kumbe ni stand ya bodaboda!!! nilipapenda sana Msemo Beach na Makonde kabla hawajajenga ile club

Hahaaa kweli mtu asiyejua coco neach mtwara anaweza dhani ni pwani haha
 
We dada nahisi nakufahamu sana, kama ukienda FINI kuokota kunazi...basi tulikuwa mkumbo mmoja, manake tukitoka tu ligula primary school tunaenda shangani kuokota kunazi, wale watoto wa kishua nikiwaonea gele sana manake mikunazi ipo mbele yao tu, tulikuwa tunavuka msitu wa ufundi pale!! Siku hizi kuna college ya utumishi maeneo yale!! Nikipita baharini kule nakuta wamama wanaokota viokolo na kumbwa!! Hahahaaa lazima tutie timu tukawasaidie

Hahaha humo humo Kunazi za Fini, Mtepwezi kule majumba saba bila kusahau kunazi za Shangani ya mifugo sikuiz Veta palikuwa na kunazi sana sema mbwa sasa. Kutoka ligula p school unazama TTC bwawani kuchimba udongo na lile pori ambalo sasa hivi kuna Shule ya Sekondari ya Shangani palikuwa na vitoro vingi sana hahaha
 
Afu unajua mie nimesoma Ligula primary?
Wapi mwl Mayele, Chimpepo, Haule, Mandanda,Nachi alikuwa na mkono uliolemaa....mdogomdogo, nitakujua tu

Hahaha Mwalimu Masali mbana pua.. Mwalimu Dodi, Manento,Ngonyani,Lingwanda,Mduma ila wengi wamehama kabaki Mwl. Fundi na Mkongwe mwenyewe Mwangata hadi leo bado mwalimu Mkuu.
 
Ha ha ha ha! Viokolo na Kumbwa na Chikandanga na Ming'oko only in Mtwara and Lindi regions. Dar es Salaam Wazaramo na Wandengeleko Ming'oko wanaiita MIBAO, wakati Vitolo na Makung'u( only in Mtwara) huku Dar wanaita Mabungo na tukapata jina UBUNGO!

Vitoro, Matiri a.k.a Mabungo,P** za paka,Ububudu,Ming'oko,Kumbwa,Viokolo hahahaaa some memories never end... wamama waliokuwa wanakaa Kianga ndio walikuwa wanaongoza kwa kuchokonoa kumbwa
 
Ok kaka! Ni Msambaa wa Lushoto-Tanga huko, kwenye safu za Milima ya Usambaa!

Hivi pale verani bado pako vilevile? Pamoja na kina kirefu tulikuwa tunaoga pale. Nilikuja Mtwara mwaka huu mwezi April, nilikuta Zambia road iko paved kwa lami, pale Magomeni mnadani( sijui siku hizi wako wapi) niliambiwa itawekwa lami hadi VETA huko sasa sijui ilishawekwa? Sizinga utuarifu kama lami tayari Magomen-Veta, Tandika Road, MATC( Inaitwa COTC) lami tayari!?

Yeah lami tayari kutoka pale Magomeni mitumba ile njia inakutana na ile ya kwenda airport .. then imepita kule mangowela mpaka chuno hadi veta kule tena lami yake ni high quality soft na taa zinawekwa kwa sasa wanajengea mirefeji sio siri kumebadilikaa kule shangani jirani na veta kuna appartments kama tatu hv na hotel zinajengwa soon mtwara utakuwa mji mzuri sana
 
Kunamiji mingine nimeshangaa hawali kunazi wanaona matunda ya ajabu hahaha Zanzibar kuna sehemu panaitwa Mkunazini nashangaa kuna mtu alikuwa hajui kama yale matunda yanaliwa kapiga picha tu nikamwambia aonje ajionee utamu hahaha. Dodoma pia kuna kunazi nyingi ila wenyeji hawajui kama zinaliwa, me hata leo hii niikute kunazi mji wowote hata siachii najikumbushia enzi.

yaani kumbe mmeanza zamani kula na madogo wanarithi?
 
Hivi kampuni ya Ng' itu imekufa kabisa? Mbona kimya? Hata zile coaster za Mtwara- Masasi hakuna, au bado zipo? Mulioko Mtwara mutujuze!

Kampuni ya Sollo imekufa kabisa? Mbona kimyaaa?

Vipi Al hamduli llah nae kimya hana basi kabisa? Mutujuze!

Shida ya wenyeji wa kule uswahili sana to be honest hata vitu au biashara maarufu ni za watu wa kuja bora hata Murji hata akiwa fisadi ila anajitahidi kumaintain kampuni yake ya Machinga
 
yaani kumbe mmeanza zamani kula na madogo wanarithi?

Aisee utoto acha tu utakuta tunaokota kunazi tunajaza fuko zima alafu ukifika home unakula kumi tu alafu unaacha hapo zimekukinaii. Ila ukiangalia hiyo suluba ya kufukuzwa na mbwa hahaha
 
Shida ya wenyeji wa kule uswahili sana to be honest hata vitu au biashara maarufu ni za watu wa kuja bora hata Murji hata akiwa fisadi ila anajitahidi kumaintain kampuni yake ya Machinga

kweli umenena ila we angalia wachaga wanavyoshika kasi kina kweka,massawe ht shule kule chache kweli yaani private hazifiki kumi SIJUI TANO ZILE
KUNA MIDECE,OCEAN,CALL AND VISION (HAINA MIAKA MINGI)NMTWARA SISTERS,AQUINAS,MTWARA ISLAMIC(YA HIVI KARIBUNI)NA KING DAVID
 
aisee utoto acha tu utakuta tunaokota kunazi tunajaza fuko zima alafu ukifika home unakula kumi tu alafu unaacha hapo zimekukinaii. Ila ukiangalia hiyo suluba ya kufukuzwa na mbwa hahaha

mi nilikua naonaga madogo kutwa shangani kutafuta kunazi
 
kweli umenena ila we angalia wachaga wanavyoshika kasi kina kweka,massawe ht shule kule chache kweli yaani private hazifiki kumi SIJUI TANO ZILE
KUNA MIDECE,OCEAN,CALL AND VISION (HAINA MIAKA MINGI)NMTWARA SISTERS,AQUINAS,MTWARA ISLAMIC(YA HIVI KARIBUNI)NA KING DAVID

Bado sana muamko enzi zetu private ilikuwa ocean tu tena walienda kusoma waliofeli ukienda private enzi zetu ulikuwa unaonekana kilaza we didnt care about St. Kunani yaani ukifaulu serikalini wewe ni kichwa balaa tena hasa shule za vipaji maalum basi nadhan wawekezaji wajitahidi kuwekeza kwenye hiyo sekta. Umesahau na Sabodo pia ni Private
 
Back
Top Bottom