Nakubaliana na wewe kwa ubora wa magari na huduma katika mabasi ya JM Luxury. Nilisafiri kwa basi lao toka MTR-DSM mwezi August. Wakati tunaanza safari utangulizi wao ni kama ulivyoeleza ila kwa safari yetu walitueleza tutasafiri kwa masaa 8 tutapata chakula Nangurukuru na Ikwiriri. Mtwara tulitoka saa 1:30 asubuhi, saa 9:30 tulifika Mbagala na saa 9:45 alasiri tulikuwa Temeke mwisho.
Kwa ujumla mleta mada uko sahihi kabisa, kwani usafiri ule na hali hii ya leo kuna tofauti kubwa sana. Hivi sasa unaweza kupata chai ya asubuhi Mtwara, chakula cha mchana DSM na cha usiku, saa 2 ukapata Tanga, Morogoro, Dodoma, hata Iringa.
Mwenye picha za magari ya enzi zile kama MKARAMO, TAWAQAL, AMWENYE, SUPER CONCORD/MWAMBAO, KAWAMBWA, SOLLO SR & JR, MAKUTI na hata picha za meli kama MV LINDI, KILINDONI, MAPINDUZI, MAENDELEO, MS MTWARA, NK. atuwekee tujikumbushe. Ila pia tuwashukuru wenye yale magari maana kwa njia ile mtu kupeleka gari yako, yataka moyo.