Kuhusu usafiri kuna jambo moja wafanyabiashara hawajaw wabunifu. Kama basi la kwanza linafika Dar saa7 kwa nini hakuna route ndefu kidogo ya hapo?
Kwa mfano mabasi ya Dodoma( Mohammed Trans) hutoka Dar saa nane na kuingia Dodoma saa 3:30 usiku. Magari ya Tanga yanatoka saa 10 na kuingia Tanga saa3 usiku na Magari ya Moro ndo usiseme! Sasa kama mabasi yanayotoka Mtwara yanafika Dar saa7, kwa nini kusiwe na route ya Dar Moro?! Kama gari la Dodoma linafika Dar saa6:30, kwa nini hakuna route ya Dodoma/ Mtwara- Mtwara/ Dodoma!? Watu wanalazimishwa kulala Dar bila sababu ya msingi! Ni suala la Uthubutu tu lakini inawezekana! Changamoto kubwa ni jinsi ya kuvuka foleni ya Malori pale TAZARA na Ubungo. Lakini njia Mbadala zipo. Basi likipita Kisarawe au Kinyerezi kwa yale yanayounga moja kwa moja hamna foleni yoyote. Kipande cha vumbi pale Kinyerez hadi Mbezi Luis ni kilometa10 tu ambazo kwa basi ni dk25tu.
Matajiri wa kusini na Watanzania kwa ujumla wawe na uthubutu.
Au yule wa JM Luxury Coach ajaribu kwa kuwa anauzoefu wa route ndefu za Dar Mbeya. Nina uhakika watamek pesa. Kwa kuanzia trial route ya Mtwara-Moro kwanza,baadae Mtwara-Tanga, Mtwara-Dodoma na mwisho ni Mtwara- Iringa.
Kuna tajir alijaribu Songea Dodoma, alivyopiga hela tu sasa anaendelea!