Asante mleta uzi maana umenikutanisha na mmoja wa watoto tuliocheza utotoni Indian kota.
....yaani ilikuwa ikifika msimu wa embe, mtoto hatumwi dukani...ukimtuma tu, haooooo kwenye miembe.
Unapakumbuka kwa Mzee Mwakyoma, baba Hanifa, Mzee George....kule ng'ambo kwa mama Salama alikuwa na mapacha 2 wa kiume.
Unapakumbuka kwa kina Rehema, nyumbani kwao ndio kulikuwa na mipapai mitamu kota nzima, watu tulikuwa tunaamka saa 9 usiku tunaenda kupanda fensi ili kuiba mapapai.
Unakumbuka mibuyu ya pale bwawani?
Aiseeee.....hivi unamjua Ishumi Fadhili?
alikuwa mtoto toka Chikongola, akakosea step akaja kutuchokoza watoto wa kota....alichokipata, alihama mpaka shule