Kwa wahusika hasa halmashauri ya jiji na TAMISEMI, wasafiri tunaotumia usafiri huu tunakerwa na tabia ya wafanyakazi wenu kukatisha tiketi na kuchukua pesa hali wakijuwa hakuna either magari au magari yapo ila madereva hakuna. Hali imekuwa ikijitokeza mara kwa mara.
Leo asubuhi na mapema watu tumefika kituoni na kukata tiketi kama kawaida, matokeo yake tumekalishwa pale kituoni takribani saa zima bila kuambiwa chochote.
Ukiuliza kulikoni wale wafanyakazi na viburi vyao wanakukalia kimya. Ushauri wangu ni kwamba kama mnajua kuna tatizo lolote kwenye mfumo wenu wa usafiri ni bora mtuweke wazi sisi watumiaji wa huduma hii ili tujipange kivingine, sio mnachukua pesa zetu halafu huduma hakuna.
Tafadhali wahusika hebu lifuatilieni hili, linatia doa huu mradi.