Usafiri wa mwendokasi kituo cha Kimara kero kwa wananchi

Usafiri wa mwendokasi kituo cha Kimara kero kwa wananchi

kyata

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2015
Posts
2,535
Reaction score
2,499
Kwa wahusika hasa halmashauri ya jiji na TAMISEMI, wasafiri tunaotumia usafiri huu tunakerwa na tabia ya wafanyakazi wenu kukatisha tiketi na kuchukua pesa hali wakijuwa hakuna either magari au magari yapo ila madereva hakuna. Hali imekuwa ikijitokeza mara kwa mara.

Leo asubuhi na mapema watu tumefika kituoni na kukata tiketi kama kawaida, matokeo yake tumekalishwa pale kituoni takribani saa zima bila kuambiwa chochote.

Ukiuliza kulikoni wale wafanyakazi na viburi vyao wanakukalia kimya. Ushauri wangu ni kwamba kama mnajua kuna tatizo lolote kwenye mfumo wenu wa usafiri ni bora mtuweke wazi sisi watumiaji wa huduma hii ili tujipange kivingine, sio mnachukua pesa zetu halafu huduma hakuna.

Tafadhali wahusika hebu lifuatilieni hili, linatia doa huu mradi.
 
Nakumbuka mwaka 2017 September nilichoma mahindi zaidi ya saa na zaidi nimesimama namsubiri mchina,nikasema hapo sirudi tena
 
Sjajua mmiliki haswa wa haya magar ya mwendokasi ila kuna sehem kdogo anakwama yaan akirekebisha tu bas hakuna mteja atapanda dala dala kwa hz route znazosapot mwendokasi.
yaan wahudumu wamejaa dharau, watu wanajaa ktuon kama nyuki kwny mzinga, gari znajaza abiria kama mizigo yaan i wish kuwa mkurugenz wa mwendokasi just for one month hakika haitakuwa mwendo kasi hii.

mfano wanajua kabisa mida ya asbuh route ya GERRZANI-KIMARA inakua na wateja weengi mnooo lakn unashangaa wanaruhusu gar moja then wanasubiriiii baada ta dakika kama 30 hv ndo wanaruhusu gar nyngne hapo abiria wamejaa ktuon kama nyomi yaan daaah

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku wakiamua kuweka mtu muelewa sahihi wa uendeshaji wa biashara ya magari nadhani haya malalamiko tutafanya historia.

Watu wanamiliki magari 200-300
Na hauwezi kuona mapungufu kama ya udart.

Biashara ya cash lakini matatizo uradhani kuna watu wanayapanda hayo mabasi kwa mkopo
 
Back
Top Bottom