Usafiri wa Treni ya Abiria Dar Hadi Arusha na Treni ya mizigo toka Tanga ndo basi tena

Usafiri wa Treni ya Abiria Dar Hadi Arusha na Treni ya mizigo toka Tanga ndo basi tena

Toka mashirika haya yaanzishwe wafanyakazi ni vibarua lazima ife

Ngoja tuandae kwanza wataalam ili tuanze upya
 
Wananchi waliifurahia sana, Abiria walikuwepo mbona , we unafikiri huduma yoyote ikiwa nzuri Kuna mwananchi ataacha kuitumia?
Mtu aliye Dar anaweza kwenda Arusha muda wowote kuanzia alfajiri mpaka mida ya saa mbili hivi. Treni lilikua lina hii convenience?
 
Tatizo la Magufuli. Alikuwa anafanya vitu kwa nguvu bila akili. Siyo treni tu ni mengi aliyofanya yameyeyuka. Ange fix mfumo wa nchi na namna ya kupata na kuwajibisha viongozi kwanza. Huwezi kujenga nyumba mpya kwenye msingi mbovu halafu iwe imara. Tulisema tukaambiwa sisi ni vibaraka wa mabeberu.
Magufuli hata kama alikuwa na mapungufu yake lakini sehemu nyingine lazima apewe maua yake.

Hili la kufufua treni ya abiria kwenda Arusha lilikuwa mojawapo ya jambo la maana alilofanya, alianzisha badala wengine waendeleze, ajabu ndio wameua kabisa.

Hapo unaanza vipi kumlaumu Magufuli kwa kisingizio cha mfumo? Kwani yeye hakuwa sehemu ya huo mfumo alitoka mawinguni?

Tusidanganyane, hii awamu ya Samia imejaa ufisadi wakutisha, na Samia mwenyewe ni mzembe na mvivu hajui kufuatilia mambo ndio maana akakiri hawezi kufuatilia kama mtangulizi wake.

Hata bwawa la Nyerere, Magufuli amejenga licha ya kelele nyingi zilizokuwepo, ajabu leo limekamilika badala ya kutuondoa kwenye migao ya umeme, bado umeme haueleweki na serikali inataka kwenda kununua umeme Ethiopia, huu ni ujinga wa serikali ya Samia, sio kosa la Magufuli kwa kisingizio cha mfumo.
 
Hii nchi ni shida Kila nyanja tangu tupate uhuru Hadi Sasa ni ngumu kukuta huduma ya serikali ya uhakika na wananchi wakaifurahia.

Magufuli alifufua usafiri wa Treni kwenda kaskazini lakini ndani ya muda mfupi toka afariki Dunia usafiri umekufa kabisa Hadi Leo, hakuna usafiri wa Treni ya Abiria Wala ya mizigo Inayotoka Dar ,Tanga kwenda Arusha.

Hii nchi ni huduma Gani haswa ya serikali mwananchi anaifurahia ambayo haina bugtha?
Kwenda mnadani!
 
Reli ile ni muhimu Sana... biashara za usafiri zinamilikiwa na wanasiasa au watu walio karibu na wanasiasa, Wamiliki wa biashara za usafiri wanatoa pesa nyingi Kwa Chama wengine ni walezi wa Chama mkoa...Ni maslahi binafsi tu....
 
Back
Top Bottom