wana JF,
Leo nimeshuhudia abiria mbishi alyeingia kwenye basi baada ya kudai kuchoka kukaa kituo cha basi, wale wote wanaoanzia katikati ya safari ambao sio wa kituo kikuu, hawa wanakuta mabasi yote yamejaa, hivyo hukaa sana kituoni kuona kama kuna abiria aliyepungua ili nao waingie.
Konda ilibidi asaidiwa na abiria wengine ili kumtoa nje asije kukabiliwa na adhabu ya tshs 200,000 kwani leo traffic hawana mchezo.
Leo kwa mara ya kwanza abiria wameaanza kukataana na kusaidiana na konda ili gari iende level sit trafic wasikamate gari na kuanza kucheleweshwa.
Suruhisho la muda au la kudumu, ni polisi kufanya kama nchi za jirani, yule mtu aliyesimama ndiye anatakiwa kushushwa na kuchukuiwa hatu hivyo abiria wote watakuwa makini na konda hatapata shida kugombana na watu.
Mabasi mengine yaanzishe ruti fupi fupi ilikukabiliana na janga hili. Mfano basi linatoka posta linaweza kuishia Africana hili lianze na watu ambao wanakuwa hawajawa wengi. Awepo mabasi yanayoanzia kawe-posta. Posta mbezi chini mpaka Africana.
Sehemu nyingi waanzishe hivyo. Wfanye kama mwendo kasi wanavyofanya kwamba, kuna zinazoishia ubungo na nyingine kimara na nyingine mbezi mwisho