Habari wakuu, natumai huko muliko hali zenu ni nzuri na mmechukua tahadhari madhubuti dhidi ya Corona.
Hakika corona imeleta mabadiliko katika nyanja nyingi, mabadiliko hayo nayaona yakiwa na faida katika sekta ya usafiri wa umma ndani ya jiji la Dar es salaam.
Hapo awali iliaminika kwamba Dar bila daladala kusimamisha abiria haiwezekani, sasa korona imefanya hili swala limewezekana.
Kila kitu kinapoanza kinachangamoto zake, tumeahuhudia changamoto kubwa ya usafiri imeibuka kutokana na gari zote kubeba abiria level seat lakini naamini hali itazoeleka serikali ikisema hali hii iendelee hata baada ya korona.
Watu wanaosafiri ni wengi kuliko mabasi ndani ya jiji hili, hii naona ni fursa kwa wawekezaji kununua basi nyingi kuweza kuenda na hitaji la abiria.
Pia serikali angalau ingeongeza bei kwa daladala kwa route iliyokua 400 iwe 600, route ya 600 iwe 800 hii itasaidia kwa wamiliki, madereva na makondakta kupata faida ya kuendesha maisha yao kila siku.
Chondechonde, serikali ya nchi hii tunaomba mutangaze wazi kwamba hata baada ya korona usafiri kwa level seat ndani ya jiji ni lazima na uendelee, kwa sasa faini ya 30000 mnayotoza madereva wanaokyuka ni ndogo, inatakiwa iongezwe mpaka 50000 hii itawafanya waheshimu!
Level seat ndani ya jiji inawezekana.