Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

Usafiri wa umma watakiwa kubeba abiria kwa idadi ya viti 'Level Seat' ili kupambana na mlipuko wa Virusi Corona

Habari wakuu, natumai huko muliko hali zenu ni nzuri na mmechukua tahadhari madhubuti dhidi ya Corona.

Hakika corona imeleta mabadiliko katika nyanja nyingi, mabadiliko hayo nayaona yakiwa na faida katika sekta ya usafiri wa umma ndani ya jiji la Dar es salaam.

Hapo awali iliaminika kwamba Dar bila daladala kusimamisha abiria haiwezekani, sasa korona imefanya hili swala limewezekana.

Kila kitu kinapoanza kinachangamoto zake, tumeahuhudia changamoto kubwa ya usafiri imeibuka kutokana na gari zote kubeba abiria level seat lakini naamini hali itazoeleka serikali ikisema hali hii iendelee hata baada ya korona.

Watu wanaosafiri ni wengi kuliko mabasi ndani ya jiji hili, hii naona ni fursa kwa wawekezaji kununua basi nyingi kuweza kuenda na hitaji la abiria.

Pia serikali angalau ingeongeza bei kwa daladala kwa route iliyokua 400 iwe 600, route ya 600 iwe 800 hii itasaidia kwa wamiliki, madereva na makondakta kupata faida ya kuendesha maisha yao kila siku.

Chondechonde, serikali ya nchi hii tunaomba mutangaze wazi kwamba hata baada ya korona usafiri kwa level seat ndani ya jiji ni lazima na uendelee, kwa sasa faini ya 30000 mnayotoza madereva wanaokyuka ni ndogo, inatakiwa iongezwe mpaka 50000 hii itawafanya waheshimu!

Level seat ndani ya jiji inawezekana.
 
Wale wote wenye leseni za kusafirisha abiria iwe mabasi ya mikoani au daladala za mjini watakaogoma kwa kisingizio cha level siti ni uhaini kwa nchi na USALITI kwa taifa.

Wenye magari wanatakiwa waelewe tuko kwenye Vita isiyo ya kawaida hivyo wanatakiwa wapunguze kipande cha siku Kama kujitolea kwao kwa taifa lao.

Kumbukeni mkijua serikali inauwezo wa kuamuru magari yote yafanye kazi kwa lazima kwani mmesahau wakati wa Vita idi amini?

Magari ya watu binafsi yalichukuliwa kwa amri ya serikali na kupeleka askari vitani.

Niwaombe wamiliki wa magari kwa muda huu msiangalie maximum profit fanyeni Kama huduma na msaada kwa Jamii na taifa.

Mjue nchi iko vitani sio utani msiilazimishe serikali itumie nguvu za ziada na hatua zisizo za kawaida.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Naanza kwa kuipongeza serikali kwa kusisitiza umuhimu wa level seat ikiwa ni njia ya kuwaepusha watanzania wasiambukizane virus vya corona.

Ukifanya tathimini lwenye vituo vya abiria, hasa mijini, na hususani Dar, kinachotokea ni kupunguza mrundikano wa watu ndani ya vyombo vya usafiri na kuuhamishia kwenye vituo. Walati route ya mwendo kasi, ferry au daladala inachukua dakika 30 hadi 90, watu wanarundilana vituoni dakika 45 hadi 120 kabla hawajapata usafiri.

Hapo ndipo nikakumbuka hadithi ya kuku na yai, ni kipi kilianza kuumbwa. Tunaepusha watu wasiambukizane ndani ya vyombo vya usafiri, na tunawawekea mazingira waambukizane vituoni. Inabidi serikali ibuni mbinu ya kudhibiti mikusanyiko na mirundikano ambayo itawakinga watu wasiambukizane vituoni na kwenye usafiri.

Nawasilisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kupitia Tamko la serikali la kupunguza abiria kujaa kwenye daladala, daladala zimeendelea kujaza mbele ya kituo cha polisi matangini (kawachokoza polisi), tusubir Tamko la jeshi la polisi sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshuhudia daladala kadhaa zitokazo Kimara kuelekea Mjini na Makumbusho zikiwa zimejaza abiria kupitiliza.

Ndiposa najiuliza zoezi la level seat limeshindikana au kuna namna ya kusimamisha abiria inayoruhusiwa?

Maendeleo hayana vyama!
 
Mungu atuepushilie mabli lakini yanayoendelea baada ya wiki hakuna atakayesema laxzima niende kazini tuta ji lockdown wenyewe .
Italy walikuwa na dis obeyance kama sisi wanakoma sasa america wanachapwa na arrogance yao china wanaokolewa na discipline yao africa especially Tanzania tutakufa kwa ignorance yetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
“Mwendo ni level seats, kusimamisha ni kwa mkeo”.
 
f54c43e1-592e-4524-8562-346727658132.jpg
 
Yet lanzini in Lazio za serikali tu, kama unaenda Kenya kazi zako, au kazi binafsi hanna shida.
Amekosa kuelewa his kazi zinategemeana, Luna ofili Huawei separates Walter kuwahudumia kama Gandhi ya ofili zimedungwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! Ni nini hiki umeandika!?
 
Back
Top Bottom