The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,475
- 12,281
Zamani, makombora mengi ya Iran yalitegemea GPS ya Marekani, ambapo Marekani aliweza kuizima au kuivuruga (jamming) wakati wa vita.
Iran sasa imehamishia mifumo yake ya kijeshi kwenye mfumo wa BeiDou-3 wa CChina Mfumo huu unawapa Iran uwezo wa kulenga kitu kwa usahihi wa hadi sentimita chache. Tofauti na GPS, mawasiliano ya BeiDou ni vigumu sana kwa nchi za Magharibi kuingilia au kuyavuruga.
Pia Iran imepiga hatua kubwa katika kutengeneza makombora yanayoweza "kufikiri" yenyewe yanapokaribia kutua kwenye shabaha. Makombora kama Fattah-1 na Kheibar Shekan yana kamera na sensa zinazotambua sura ya jengo au eneo lililokusudiwa. Hata kama adui akijaribu kuvuruga mawasiliano ya satelaiti, kombora linatumia "macho" yake kukamilisha kazi.
Ripoti za mwaka huu (2026) zinaonyesha kuwa China na Urusi zimekuwa kama "macho" ya Iran:
Satelaiti za Ujasusi: China inatumia zaidi ya satelaiti 500 kufuatilia mienendo ya meli na kambi za kijeshi za Marekani na washirika wake, kisha inashiriki taarifa hizo na Iran kwa wakati (real-time).
Satelaiti ya Khayyam: Iran pia inatumia satelaiti ya Khayyam (iliyotengenezwa na Urusi) ambayo inatoa picha zenye ubora wa hali ya juu za maeneo ya maadui.
Iran imekuwa nchi ya nne duniani (baada ya Urusi, China, na Marekani) kumiliki makombora ya hypersonic.
Makombora haya yanatembea kwa kasi ya ajabu (zaidi ya mara 5 ya sauti) na yanaweza kukwepa (maneuver) katikati ya safari. Hii inafanya mifumo ya ulinzi kama Iron Dome au Patriot kushindwa kuyazuia, hivyo yanafika kwenye target kirahisi.
China haisaidii Iran bure tu; ina maslahi yake pia kama
Mafuta: Iran inaiuzia China mafuta mengi kwa bei nafuu kupitia njia za siri.
China inafurahi kuona Marekani ikimaliza silaha na fedha zake Mashariki ya Kati, ili Marekani isiweze kuelekeza nguvu zake zote kule Asia (kwenye bahari ya China Kusini).