Tsh
JF-Expert Member
- Aug 26, 2021
- 17,022
- 36,936
Wawekezaji na wafanyabiashara wadhibitiwe ili kuendesha nchi? Fuatilia data sekta za biashara Tanzania na uwezo wao wa kulipa kodi halafu linganisha na capital expenditure na current exp halafu uone kama wataweza.Zote hizo ni rushwa hela za kuliwa na vigogo pia utando wa spider 'spider web' kuinasa nchi zaidi kisaikolojia kwenye utegemezi.
Ndio hiyo tunasema 'ombaomba' ..Rais yuko kwenye simu kuombaomba badala ya kudhibiti wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa kulipa kodi. Sijui tufanyaje kuchange mindset ya mama.
Mungu tuhurumie tufike 2025 salama kupata magufuli mpya.
JPM alitumia hii mbinu 2017-2020 sekta binafsi ikawa hoi na angeendelea sekta binafsi ingejaa wamachinga tu. Kwanini, sababu sekta binafsi haiwezi kuendesha hii nchi ikalipa mishahara, marupurupu, mafuta ya magari na bado ikalipia miradi mikubwa ya maendeleo. HAIWEZEKANI.
Ukumbuke mpaka sasa Tanzania tunakusanya kodi ya mapato ya wafanyabiashara kabla ya mwaka wa biashara husika kisha kama wakipata hasara tunawafidia mwaka wa biashara ujao.
Ufahamu mishahara sekta binafsi inakatwa PAYE na hizi PAYE na mishahara ni bajeti za wafanyabiashara ili biashara ijiendeshe.
Pia kuna kodi za zuio, sdl, na kodi ndogo ndogo nyingi tu. Bado kuna kodi za manispaa, zima moto, Osha, wcf, Brella na bodi zinazosimamia biashara husika.
Tanzania inahitaji ongezeko la wafanyabiashara na wawekezaji maana ni wachache na tayari tunachukua vingi kutoka kwao, kuwabana zaidi ni kuwakimbiza.
Ukumbuke pia watanzania wa kawaida wenye biashara ndogo ndogo na shughuli za hapa na pale ni walalamishi pale wanapoambiwa lipeni kodi. Mfano hapa tukiongeza TOZO kidogo tu, utashuhudia kelele zisizo na kipimo.