USAID kuipa Tanzania msaada wa Dola za Marekani Milioni 25

Wawekezaji na wafanyabiashara wadhibitiwe ili kuendesha nchi? Fuatilia data sekta za biashara Tanzania na uwezo wao wa kulipa kodi halafu linganisha na capital expenditure na current exp halafu uone kama wataweza.

JPM alitumia hii mbinu 2017-2020 sekta binafsi ikawa hoi na angeendelea sekta binafsi ingejaa wamachinga tu. Kwanini, sababu sekta binafsi haiwezi kuendesha hii nchi ikalipa mishahara, marupurupu, mafuta ya magari na bado ikalipia miradi mikubwa ya maendeleo. HAIWEZEKANI.

Ukumbuke mpaka sasa Tanzania tunakusanya kodi ya mapato ya wafanyabiashara kabla ya mwaka wa biashara husika kisha kama wakipata hasara tunawafidia mwaka wa biashara ujao.

Ufahamu mishahara sekta binafsi inakatwa PAYE na hizi PAYE na mishahara ni bajeti za wafanyabiashara ili biashara ijiendeshe.

Pia kuna kodi za zuio, sdl, na kodi ndogo ndogo nyingi tu. Bado kuna kodi za manispaa, zima moto, Osha, wcf, Brella na bodi zinazosimamia biashara husika.

Tanzania inahitaji ongezeko la wafanyabiashara na wawekezaji maana ni wachache na tayari tunachukua vingi kutoka kwao, kuwabana zaidi ni kuwakimbiza.

Ukumbuke pia watanzania wa kawaida wenye biashara ndogo ndogo na shughuli za hapa na pale ni walalamishi pale wanapoambiwa lipeni kodi. Mfano hapa tukiongeza TOZO kidogo tu, utashuhudia kelele zisizo na kipimo.
 
Huu ni Ulimbo katika kuelekea Domokrasi
Kifuatacho Vigezo na Masharti Kuzingatiwa
Ndiyo mtajua kazi ya Lisu aliyo ifanya akiwa Ughaibuni!!
MZUNGU siyo mjinga na JIWE hakuwa mjinga
Hii Misaada majibu kwenye uendeshaji chaguzi ndiyo tutaona raha yake Wezi wezi wote wanaopita bila kupingwa jiandaeni kinacho fuatia ni haki kwenda mbele
 
Ikiwa msaada shida, ikiwa mkopo shida yani ni shiida tu kila kitu. Majitu mengine ni Kama mdhuti hata uoshe vipi hauna shukrani.
 
Wenyewe huko kwao huwa wanauliza 'what's the catch'? Maana wanajua there's no free lunch!
 
Nchi ambayo Rais wake anafadhili ufisadi hata ipewe dola za kimarekani trilioni moja haiwezi kufua dafu katika maendeleo๐Ÿ’๐Ÿ’๐Ÿ’
Your browser is not able to display this video.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ