Southern Giant
JF-Expert Member
- Sep 1, 2018
- 621
- 1,298
ukiandikiwa oral interview inamaana hautofanya written, moja kwa moja upo ktk mahojianoHivi kwenye account yako ukiandikiwa oral interview inaanisha hautafanya Written ama vipi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ukiandikiwa oral interview inamaana hautofanya written, moja kwa moja upo ktk mahojianoHivi kwenye account yako ukiandikiwa oral interview inaanisha hautafanya Written ama vipi
Tunatofautiana kazi tulizo omba ukiona ivyoSo ww una fanya interview Moja mbna mm nafanya mbili??
hakuna atakaye sahihisha mtafanya kisasa zaidi, mara baada ya kujibu maswali max zako zitatokea papo hapo ktk kompyutaWritten nani atasahihisha makaratasi ya watu 8,000?
Hapa ndio ulemsemo wa kumeanza kuchangamka inaonekanaWewe kama Mimi ..niliomba mtwara 😄
written ni multiple choice? If this is the case, then that is OK maana kuna programs za kusahihisha multiple choice!hakuna atakaye sahihisha mtafanya kisasa zaidi, mara baada ya kujibu maswali max zako zitatokea papo hapo ktk kompyuta
Sas nimeelewaTunatofautiana kazi tulizo omba ukiona ivyo
Nikiwaza lab tech wanahitajika 300 tu na pdf imetema 2000 na something nachanganyikiwa😄😄Hapa ndio ulemsemo wa kumeanza kuchangamka inaonekana
ndio ni mwendo wa multiple choice tuwritten ni multiple choice? If this is the case, then that is OK maana kuna programs za kusahihisha multiple choice!
Enhe lete plan yako,wewe ungewapangaje? Nyie ndio mnatukwaza majoblessOver 8,000 applicants kwa nafasi ngapi? UJINGA MTUPU WA SERIKALI HII. Why call all that mass for 600 slots? Rubbish!
Nakwambia ukoo wenu wote hakuna mwenye kazi kama yangu!Enhe lete plan yako,wewe ungewapangaje? Nyie ndio mnatukwaza majobless
Nikujaribu huwezi jua bahati yako huenda huu mwaka ukawa wakwakoNikiwaza lab tech wanahitajika 300 tu na pdf imetema 2000 na something nachanganyikiwa😄😄
Mbona wakata tamaa mapema hivyo. Sometimes hizi mambo ni bahati kazi nayofanya tulikuwa elfu ishirini na mbili tukaenda hivyo hadi tukabaki 100Nikiwaza lab tech wanahitajika 300 tu na pdf imetema 2000 na something nachanganyikiwa😄😄
kama uliomba kwa anuani ya tanga, utakwenda tanga! nyie vijana vipi? mbona ni self explanatoryMkoa husika ni mkoa uliombea kazi!
Poleni! Ila Allah yu nasiLeo utumishi wametoa majina ya wasailiwa kada ya afya, usaili huo utaanza septemba 2 mpaka tarehe 9, katika mikoa waliombea nafasi!
Niwapongeze sekretariati ya umma kwa kazi nzuri ambapo kwa sasa ni imani yangu saili zote zitafanyika kwenye mikoa ya waombaji hii itawaondolea vijana gharama na itawafanya wote kushiriki usaili huo tofauti na mwanzo, maudhurio yalikuwa ni madogo kwa sababu wengi walikuwa wanashindwa nauli na gharama za kwenda Dodoma!
Niwatakie wasailiwa wote mithani mema! Niwahakikishie tu kama wewe ni compentent wala huna haja ya kuogopa lakini mtihani ni mtihani tu hata kama wewe ni kichwa kusimama mbele ya panel yamkini wengine uzoefu huo hamna! Lakini kila jambo ni kumtanguliza Mungu!
All the best madaktari wetu!
2000 umezijuaje pleaseNikiwaza lab tech wanahitajika 300 tu na pdf imetema 2000 na something nachanganyikiwa😄😄
Sawa mkuuDONDOO ZA USAHILI WA WRITTEN KUPITIA MFUMO WA KIDIGITALI
Mtihani unafanyika kwa njia ya kidigitali, cha muhimu unatakiwa ufike kwenye kituo utakachopangiwa siku ya interview mapema kabla ya saa 1 asuhuhi maana huwa kuna heka heka za hapa na pale. Mnaweza kuhamishwa darasa au kupewa maelekezo ya ziada. Kituo ulichopangiwa utakiona kwenye akaunti yako ya ajira portal. Hakikisha unaenda kwenye kituo hicho na si vinginevyo.
Nenda na viambatanisho muhimu la sivyo utazuiliwa kufanya huo mtihani; Hakikisha unabeba
1. Vyeti halisi (original copies) cha form four na form six
2. Cheti halisi cha chuo
3. Cheti cha kuzaliwa
4. Kitambulisho kinachokubalika (NIDA, Pass ya kusafiria, leseni ya udereva au kitambulisho cha mpiga kura)
5. Kama majina yako ya academic certificates na kitambulisho au cheti cha kuzaliwa hayafanani hakikisha unatafuta DEED POLL mapema kutoka kwa mwanasheria au wakili yeyote la sivyo utazuiliwa kufanya mtihani.
Tukirudi kwenye mtihani;
Hakikisha unaijua vizuri email yako na password unayotumia kuingilia kwenye account yako ya ajira portal maana ndio utakayoitumia ku-access mtihani wa written.
Msimamizi ndiye atakaye weka address (URL) ya wewe kuuona mtihani wako, atakupangia komputa ya kukaa ikiwa na Login page (ina sehemu ya kuingiza email na password ileile ya ajira portal).
Ukisha-login, utaona maswali 50 ya kuchagua (multiple choice). Muda wa kujibu ni lisaa limoja (1 hour). Hakikisha unajibu maswali yote kabla ya ku-submit. Unaweza ukachagua jibu na kisha ukabadilisha na kuweka lingine.
Mara baada ya kumaliza mtihani wako, hakikisha unajiridhisha umejibu maswali yote kabla ya ku-submit, kuna panel kushoto itaonesha maswali uliyojibu kwa kuyawekea rangi ya kijani na ambayo haujayajibu kwa rangi ya gray(kijibu). Once ukisha-submit ndio basi huwezi kulog-in tena wala kufanya chochote zaidi ya kusubiri matokeo ambayo utayapata siku hiyo hiyo.
MAMBO YA KUZINGATIA:
Achana na mambo ya kupiga chabo. Maana ule mtihani upo very tricky, swali la kwanza kwako sio la kwanza la jirani yako.
Baada tu ya ku-log in screen ya maelekezo itakuja na itadumu kwa dakika tatu kisha mtihani utakuja. Utakuwa kwenye screen yote. Usije ukathubutu ku-minimize ile screen kwa sababu yoyote ile. Ukifanya hivyo mtihani utaji-submit na utakuwa umeshafeli.
Zingatia sheria zote za mtihani maana ukikamatwa unaibia utafungiwa kufanya mitihani ya PSRS kwa muda usiojulikana pia unaweza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.
Simu, saa zote na vifaa vya kidigitali haviruhusiwi wakati wa kufanya mtihani, ukijanavyo utalazimika kuviacha mbele ya chumba cha usaili.
BAADA YA MTIHANI:
Kama uliomba nafasi zaidi ya moja utaendelea kusubiri kwenye chumba cha mtihani ili kufanya interview nyingine mpaka zote umalize.
Baada ya kumaliza mtihani subiri matokeo yako kwenye account yako kama umekuwa SELECTED au NOT SELECTED kwa hatua inayofuata. Marks ulizopata zitawekwa kwenye tovuti ya ajira utumishi kwa namba yako ya mtihani. Mara nyingi majibu hutoka kuanzia jioni maana interview zote zinakuwa zimeshamalizika za siku husika.
Kama kuna jambo sijalitaja wataalamu wengine watatoa mwongozo. Best wishes watumishi wa umma.
8125 hawa ndio wa clinical medicine oral interview? mbona ni ujinga mtupuLeo utumishi wametoa majina ya wasailiwa kada ya afya, usaili huo utaanza septemba 2 mpaka tarehe 9, katika mikoa waliombea nafasi!
Niwapongeze sekretariati ya umma kwa kazi nzuri ambapo kwa sasa ni imani yangu saili zote zitafanyika kwenye mikoa ya waombaji hii itawaondolea vijana gharama na itawafanya wote kushiriki usaili huo tofauti na mwanzo, maudhurio yalikuwa ni madogo kwa sababu wengi walikuwa wanashindwa nauli na gharama za kwenda Dodoma!
Niwatakie wasailiwa wote mithani mema! Niwahakikishie tu kama wewe ni compentent wala huna haja ya kuogopa lakini mtihani ni mtihani tu hata kama wewe ni kichwa kusimama mbele ya panel yamkini wengine uzoefu huo hamna! Lakini kila jambo ni kumtanguliza Mungu!
All the best madaktari wetu!