Usaili wa jana wa TRA kuna mtu aliniambia hajaona mtoto wa Kihindi pale, Unajua kwa nini?

Usaili wa jana wa TRA kuna mtu aliniambia hajaona mtoto wa Kihindi pale, Unajua kwa nini?

A job is really short term of solution to long term problems

great thinker
 
Wahindi ukiachilia mbali mambo yao mengine wale jamaa huwa ni watu wenye akili sana, Hatuwezi lingana nao kwa akili.

Wahindi huwanandaa sana watoto wao Kisaikolojia tangu wakiwa Chekechea.

Wahindi huwaandaa watoto wao kuja kuwa Wafanya biashara au kuja kurithi Biashara zao.

Wahindi ni Made Entrepreners.

Ndo maana Chuoni hutawakuta aanasoma kozi tofauti na zinazo endana na Kile wanacho fanya wazazi wao.

Wahindi utawakuta wanasoma.
- IT
-Law
-Marketing
-Accounting
-Procurement
-Na Uhandisi

Wanaosoma wakimanisha kabisa.

Niwakati sasa wa kuwaandaa watoto wetu kisaikolojia, waandae wasome waje kuwa Wafanya biashara wakubwa, wakulima wakubwa, wafugaji wakubwa na kadhalika.

Wacha kuwaaminisha kwamba wanasoma waje kuwa na maisha mazuri au waje kuwa Mameneja wa benki
8b91126a46b94152c00d30e76fb3f558.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
Dogo uliyo yasema yote kuhusu wahindi ni poa. Lakini hata sisi wazawa mbona tumesoma hayo masomo pia?

Kuna watanzania wamefanya vizuri sana katika masomo yote uliyo yataja tena wengine vizuri zaidi kuliko hata hao wahindi Nina uhakika. Lakini katika implimentation hilo ndilo tatizo. Tuna matatizo makubwa ya kutumia elimu yetu kujikwamua sisi wenyewe kimaisha na kiuchumi. Ni hapo tu ndiyo tunashindwa.
Na sio sisi tu bali mtu mweusi yeyote yule na kokote kule duniani.
Hata hao wahindi utaona huko kwao weupe ndiyo wengi matajiri na walio endelea zaidi kuliko wahindi wenzao weusi. I mean wenye ngozi nyeusi.

Mimi nahisi Tatizo letu kubwa ni kutojiamini. Nafikiri tuna kitu ambacho kimetupa sisi shock na kujiona inferior.

Nafikiri pengine wazungu, waarabu na hao wahindi wametunvunja sisi nguvu kwa namna fulani. I don't know!

Sisi watu weusi hatujiamini na wala hatumwamini mtu mweusi mwingine. Hatujipendi wala hatupendani. Tunajidanganya tuna pendana kumbe ni uongo. Tunapendana kiunafiki. Tuna wivu wa kuumizana na sio ule wivu wa maendeleo.

Kwa akili ya vitabu hiyo sio hoja! Tena sisi dogo tukiwa nje kwenye vyuo vyao wanatuheshimiwa sana.

Nikupe story moja ndogo. Wakati nikiwa katika safari moja kwenye ndege nilikutana na Dokta mmoja wa kike mzungu. Baada ya mazungumzo mafupi ya kusalimiana, akaniuliza ninakotoka. Nika mjibu mimi ni mtanzania na naishi katika hiyo nchi ambaye yeye anatoka na nika mweleza profession yangu na kampuni ambayo nafanya kazi. Aliguna kidogo na kukaa kimya. Nikumuuliza, kwani kuna nini? Akaniangalia weeee, huku akitabasam. Aka nijibu "haoni ajabu". Nilicheka kwa sauti kubwa ya mshangao! Nikamwuuliza, Huoni ajabu kivipi? Akaniambia haoni ajabu kuwa mimi nafanya kazi kwenye hiyo kampuni niliyo mtajia, kwani hiyo kampuni kwa bahati mbaya au nzuri iko kwenye mji ambao yeye anaishi na kwamba wagojwa wake wengi ni wafanyakazi kwenye hiyo kampuni.

Akaanza kunipa story ndefu sana kuhusu mtanzania mmoja msichana ambaye alisoma naye huko Hungary. Alikuwa roommate wake. Aisee huyu mzungu alimsifu sana yule msichana!

Aliniambia hajawahi kumwona mtu mwenye discipline na bidii kwenye masomo kama huyo mtanzania. Na yeye mafanikio aliyo yapata mpaka akawa dokta au Doctor of Medicine ana mshukuru sana yule mtanzania. Na kwamba hata msahau mpaka anaingia kaburini.

Kwa taarifa hii nilijisikia vizuri sana kama mtanzania. Na mimi sita msahau huyo mzungu. Mzungu ambaye ni Dokta ana msifu mtanzania mwenzangu hivyo na kwamba ana tu respect! Hiyo ilinipa mimi imani kubwa sana, kiasi ambacho napenda kutumia Slogan ya Obama, "YES WE CAN". Ndiyo tuna weza.

Watanzania tunaweza. Tujiamini. Tusiwe na tamaa ya pesa kama wafanya kazi. Tatizo letu sisi tunataka tuwe matajiri na kuwa na ufahari kama wafanya kazi. Haiendi! Mfanya biashara anaweza akawa tajiri lakini sio mfanya kazi. Mfanya kazi yeye analipwa mshahara. Kipato chake kina vary kulingana na kazi yake. Kutaka utajiri na ufahari lazima uibe. Hapo ndipo matatizo yanapo anza. Tunaiba hela ya uma ili kujitajirisha sisi wenyewe kiasi kwamba serikali ina kosa pesa za kuendesha miradi ya maendeleo ya nchi na hivyo kushindwa kuboresha maisha ya wana nchi.

Viongozi wetu ambao wako madarakani wanatakiwa wajue majukumu yao na watusaidie tuwe pia na maabara au research institutes zetu wenyewe za uhakika na sio tu zile za kungojea wazungu watupe donation na wataalam wetu wenyewe.

Watu wenye sifa zote hapo juu za utaalam dogo tunao, tena wengi sana. Pesa na vitendea kazi na surppot ya serikali katika ubunifu wa miradi ya maendeleo ya watu binafsi ina kosekana. Viongozi au watu wenye madaraka wanatumia nafasi zao pia kuchukulia mikopo bank wakati watu wengi wenye nia za kweli kuleta maendeleo kwa kutoa ajira kwa wana nchi wenzao huwezo huo wa kukopeshwa hela hawana.

Huo ndiyo umasiki wetu!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa baba yupo kazini si ndio anampanga mwanawe ajindae kuajiriwa ili aje ampachike kwenye ofisi za serikali ili yeye akistaafu mtoto wake anaingia......nadhani hatujatofautiana na wahindi isipokuwa sisi tunawaandaa watoto wetu kuja kukaa kwenye ofisi za serikali kushikiria nafasi ili ukoo mzima uhamie ofisi aliyofanyia baba

SONY Xperia Z5 Premium
 
Mkuu usikatishwe tamaa na wajinga Tupo tunao fatilia vizuri Mafundisho mazuri Toka kwako
 
Wahindi ukiachilia mbali mambo yao mengine wale jamaa huwa ni watu wenye akili sana, Hatuwezi lingana nao kwa akili.

Wahindi huwanandaa sana watoto wao Kisaikolojia tangu wakiwa Chekechea.

Wahindi huwaandaa watoto wao kuja kuwa Wafanya biashara au kuja kurithi Biashara zao.

Wahindi ni Made Entrepreners.

Ndo maana Chuoni hutawakuta aanasoma kozi tofauti na zinazo endana na Kile wanacho fanya wazazi wao.

Wahindi utawakuta wanasoma.
- IT
-Law
-Marketing
-Accounting
-Procurement
-Na Uhandisi

Wanaosoma wakimanisha kabisa.

Niwakati sasa wa kuwaandaa watoto wetu kisaikolojia, waandae wasome waje kuwa Wafanya biashara wakubwa, wakulima wakubwa, wafugaji wakubwa na kadhalika.

Wacha kuwaaminisha kwamba wanasoma waje kuwa na maisha mazuri au waje kuwa Mameneja wa benki
8b91126a46b94152c00d30e76fb3f558.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
Usiropoke ropoke kuna wahindi wachawi,kwa nguvu za Giza na misukule wapo vizuri,sio kila mfanyabiashara mwenye mafanikio ni ya halali wengine wana siri zao nyuma ya pazia
 
Back
Top Bottom