Usain Bolt... hatumii madawa?

bolt ni kipaji tu, mbona hata David rudisha jana kushinda tena hamsemi a natumia madawa? Messi na ronaldo nao wanatumia madawa? Manake wanapokezana wao tu uchezaji bora wa Dunia
 
nadhani ulimaanisha Marion Jones,huyu mwanamama ndiye aliyenifanya nipende Track and Field kwa upande wa kina dada..
ndie aliekuwa kinara wa kudanganya. alitumia madawa ya kuongeza nguvu
 
Dharau hizi,mtu anashindana mbio huku anatabasamu na kugeuka nyuma wakati wenzie wamekunja nyuso na kutweta.huyu dawa yake unamchokoza mnapigana tu kabla hata mbio hazijaanza alufu wote mnakuwa disqualified
 
ni mazoezi tu mkuu ;halaf si unajua wszungu walivyokuwa vimbelembele kama jamaa angekuwa anatumia dawa za kussmua misuli wangeshamtumbua ktaambo ukiona kimya ujue hatumii
 
Huyu jamaa huenda akawa na undugu na chui, jamaa anakimbia zaidi ya mwanga wa jua
 
Usain Bolt ataendelea kuchukua gold medals kila Sikh kwasababu anajituma na ana nidhamu ya hali ya juu! Phelps hawamsemi mtu kila Sikh anashinda yeye kuogelea mpaka anastaafu akiwa champ ila Leo ishu ni bolt,he hakuna chembechembe za ubaguzi hapa? Binafs naamini kwenye malengo ,kujituma na nidhamu na nitaendelea kumwamini na kumkubali mpaka watapoprove anatumia madawa ila so far huyu ndo nyota ambaye huwa nasubiriaga kumuona kila Olympic
 
Spidi ni mazoezi tu, dawa zinakufanya uwe na nguvu usichoke mapema ila suala la mbio Juu yako
 
Doping test wanazofanyiwa siku hizi si za kitoto technology iko juu sana... Urusi walipigwa marufuku wote coz most of them walipatikana wanatumia but wakaruhusu wachache ambao walikuwa clean 100% few days michezo ianze. Kushinda ni kipaji chako, yule muogelejai Phelps na gymnast Simone Biles kila competition wameondoka na gold kushinda hata za Bolt
 
Could be......
ila mimi bado simuamini....
Hivi na sisi tunaye sprinter Olympic rio!!?
Ni kama umekuwa coach wa timu yetu ya riadha.
Tuangalie mbio tuwaachie wataalam wa kubaini wasisimua misuli wafanye kazi yao.

Mimi ni mshabiki wa "Big Ben"

Kama vipi peleka pendekezo yaandaliwe mashindano ya wasisimua misuli, maana umedokeza sehem fulani kuwa Big ben aliwahi kuwashinda pamoja na wasisimua misuli wenzake.
 
The boss unapingana na wanakemia phd Olympics wanaowapima na kila baada ya gemu?tungekwisha sikia zamani usicheze na mzungu.


swissme
Inawezekana lakini haielezeki. Si mnakumbuka kesi ya Marion Jones? wengine hugundulika au hukiri baadaye, ilhali walipopimwa vipimo hvikuonyesha dawa zozote. Nevertheless, sina comment kuhusu Bolt kutumia dawa au la.
 

Mkuu umezungumza kitu kilicho kuwa moyoni mwangu kwa muda mrefu, kuna vitu mwanadamu anaweza kufanya ambavyo vinaonekana ni natural, lakini vitu vingine vinakuwa beyond human endurance na ngumu ku comprehend kama unacho ona kina ukweli wowote au kuna udanganyifu wa kibaiolojia wa ku tax mwili - kisa, ushinde medali by all means - ujali long term madhala ya ku abuse madawa.

Kimaumbile binadamu kadri miaka inavyo kwenda na wewe stamina inapungua hata ufanye mazoezi ya kufa mtu aisandii kitu - sasa huyu Usain Bolt awezi akawa na uwezo wa kushinda tuu kwa muda wote wa miaka kumi na mbili - hii aingii akilini hata kidogo, Usain Bolt angekuwa ni Mrusi basi Waingereza na Wamerikani wangelazimsha achukuliwe samples za damu na urine kwa mara ya pili ili zifanyiwe uchunguzi wa kina au hata kudanganya kwa kuzi- contaminate aonekane ni mdanganyifu.

Nashukuru kwa kunikumbusha visanga vya Lance Amstrong na Karl Lewis na wenzake, nikiona America inawakomalia Warusi mpaka kufikia hatua ya kumlahumu Putin, ndiyo nawaona walivyo wanafiki -niliangalia michezo ya Olympic ya 1988, mpaka leo hii na amani kwamba hata kama Johnson asingetumia dawa angeweza kumshinda Lewis kirahisi - baada ya Lewis kushindwa alitoka pale uwajani anafoka foka kuhusu ushindi wa Johnson kwamba ushindi wake unatokana na matumizi ya madawa - suala hilo alilivalia njuga kweli kweli mpaka anafikia kuonekana kero! Kumbe shutuma anazo msema mwenzake kumbe na yeye ni teja mzuri tu!!

Haya tuje kwa Lance Amstrong, yeye alikuwa anashinda tu mbio za baiskeli miaka nenda rudi mpaka wezake wanashangaa, katumia madawa kwa muda mrefu mpaka yakamsababishia ugonjwa wa cancer, cha ajabu ni kwamba wasimamizi wa mbio za baiskeli walikuwa awajui kwamba Amstrong alikuwa atumia dawa za kuongeza nguvu/stamina - walijua sana lakini walikuwa wanamfuchia siri, sijui nani alifichua siri yake.
 
Jamaa ukimuwekea boda boda anaweza kuiacha mbali aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…