Nani aondoke Simba na nani Abaki.
1. Kwenye goalkeeping hatuna sababu ya kumuondoa golikipa yoyote kwa sababu wote wanaonekana kufanya vizuri sana ukilinganisha na magolikipa waliopo ligi kuu.
2. Kwenye fullbacks sioni kama kuna hitaji la kufanya mabadiliko upande wa kulia kwani Kapombe na Duchu viwango vyao bado viko vizuri hasa ukizingatia Duchu bado ana muda mrefu zaidi wa kuwepo kikosini ndiyo kwanza ana 20 years.
Upande wa kushoto Gadiel Michael must go ameshindwa kumpa ushindi Mohamed Hussein na anapopewa nafasi hana maajabu yoyote lakini ndani ya Ligi tena sioni beki mzuri wa kufanya replacement ya Gadiel baada ya Manyama kwenda Azam.
Kwenye Central Defence tunawachezaji wazawa watatu na wa kigeni wawili kwangu mimi nafikri tunapaswa kujiandaa na maisha yetu bila Wawa na pendekezo langu ni
1. Adrian Chama wa Zesco
2. Mohamed Quattara wa Al Hilal Omdurman
3. Captain Salomon Emilie Bindjeme Banga wa Cotton Sports ya Cameroon.
Wazawa tuendelee kuwa nao kwani Kennedy anafanya vizuri back up plan Ibrahim yuko vizuri pia Nyoni muda unaelekea ukingoni hivyo hata akipewa contract kwajili ya kuretain uzoefu kikosini sioni shida.
Kwenye Midfield hapa ndiyo tunapaswa kufanya mabadiliko kadhaa.
Tuachane na Said Ndemla, tumsajili Cleophace Mukandala, tunapaswa kuandaa backbone mpya ya Defence midfield yetu ya muda mrefu hatuwezi kumtegemea Lwanga au Nyoni kwa muda mrefu kwani hawa umri umeenda na Lwanga ni mchezaji wa kigeni muda wowote anaondoka tunapaswa kumsajili Kelvin Nahashoni Naftal wa JKT Tanzania kama maandalizi ya backbone yetu huyo mtoto ana potential ya kufika mbali akipata good coaching na kuwa kwenye kikosi Chenye motisha kama Simba huyu ndiyo anafaa kuwa perfect replacement ya kesho kwa Mkude.
Lakini pia wachezaji wetu wengi kwenye midfield ukiondoa Bwalya ni defensive Midfielders tutafute namba nane mzuri atakayekuwa ana uwezo mzuri wa kukaba na kupandisha timu ili Bwalya anapofeli plan B iwepo na huyo kwangu namuona Morlaye Sylla wa Horoya ya Guinea anamaliza mkataba wake msimu huu na ana miaka 21 tu.
Kwenye Safu ya ushambuliaji tuachane na Kagere, Morisson, na probably Chikwende. mbadala wa Kagere tutafute Mshambuliaji anayeweza kucheza kama wing type ya Okwi ili tuwe tunaswitch formation uwanjani kutokana na mahitaji ya mechi.
Kuna wachezaji wazawa ambao kuwaacha haina shida mojawapo ni Miraji Adam.