Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe

Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe

Kweli kabisa. Sio sasa hivi kila mtu anajiita nabii. Anafungua kibanda anaanza maunabii yake yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Tujifunze kwa wenzetu waislamu huwezi kuswalisha mpaka umepata mafunzo ya Quran au kwa wakatoliki ambao ili uwe padri lazima usomee muda mfrefu.

Mtu unaamka asubuhi unajiita nabii Econonist , huna elimu unadanganya watu kuhusu maono. Maoni bila kuijua Biblia utaangusha watu kama walivyofanya akina Kibwetere.
Kwani biblia inasemaje kuhusu ili?.
Relax, kuna makubwa yanakuja zaidi ya haya.
 
Pale Kongowe Mbagala Mpakani mwa Dar na Mkuranga Pana she'll pembeni Pana Kanisa na Msikiti vimedumu kwa miaka mingi sana bila mgogoro wowote! So long sio ardhi ya Msikiti kanisa linatumia au Msikiti unatumia ardhi ya kanisa hakuna tatizo wewe ndio una tatizo!

Ukifika KAMATA makutano ya barabara ya Nyerere na Ile ya chang'ombe kama unaenda mjini kabla ya daraja upande wa kulia Pana Kanisa na Msikiti na vimetenganishwa na ukuta tu miaka mingi sana sana na hukujawahi kutokea mgogoro au mtafaruku.

Msikiti wa Kichangani na kanisa la kilutheri magomeni vimetenganishwa na morogoro road na Wala hakuna shida Ibada unaendelea huku na kule bila shida.

Huku mitaani tumewekeana mipaka wakristo na waislamu Wala hakuna shida!
Maofisini na sehemu za mikusanyiko tunakaa pamoja bila shida yoyote na kubwa zaidi tunazikana kama ndugu!

Kuna Sehemu Moja Huko Rombo Kilimanjaro waislamu walitoa sehemu ya eneo lao Ili pajengwe kanisa katoliki na likajengwa!

Punguza chuki kama hakuna chochote mnaingiliana au kuhitilafiana wakati wa Ibada !
Asalam
Na makaburi wanazikwa eneo moja
 
imagine leo mtu anasimama anaasema, BIBLIA NI KITABU TU kama vitabu vingine. anachukua kil akilicho kwenye Biblia, anageuza kuongea kinyume chake na anasambaza kwa tv. haya mambo yanakwaza sana Wakristo, kupita kiasi. hadi wamemtungia jina kuwa anaitwa MPINGA KRISTO. lakini serikali bado tu inamwangalia mtu aliyejifanya anamhubiri Kristo lakini anahubiri upinga Kristo.
Yuko sahihi, biblia ni kitabu tu
 
ndiomaana Kagame anataka watu wenye elimu sio makanjanja hawa wakuagiza mavu.. na kucha zipelekwe kanisani
 
Nimeshawahi kumsikiliza huyo Jamaa, aliumiza sana kichwa changu kujaribu kumwelewa.
 
Back
Top Bottom