Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe

Usajili wa ‘Kanisa la Neema’ uchunguzwe

Uko sahihi then ana dini yake tofauti na ukristo, hilo ni kosa huyo ni Mamluki ndani ya ukristo ili aangamize ukristo
na kama ana dini yake tofauti, hiyo dini yake ndio alitakiwa kusajili kule wizara ya mambo ya ndani kitengo cha usajili wa makanisa/taasisi. wenzake mbona wapo wengi tu, wengine wamejisajili kama waganga wa kienyeji wa kuagua kabisa, sheria imewatambua hivyo, wengine wanauza madawa ya kienyeji etc. na sheria haitegemei waganga wa kienyeji waende kinyume na vile walivyojisajili. ndio maana ya usajili ili ijulikane nini unakifanya. sasa yeye kajiweka kama mkristo wakati sio mkristo, ni mpinga kristo. kama iyo ni dini mpya akarekebishe usajili kule ili serikali imruhusu atambulike hivyo na imfuatilie nyendo zake ikijua ni mtu wa aina hiyo. la sivyo, anatukera wakristo, anatuchafua na anaumiza mioyo yetu hasa pale anapoongea kuwa BIBLIA NI KITABU CHA KAWAIDA TU. kifupi ni kwamba hatutaki hata kumwona akihubiri mapotofu.
 
asilimia kubwa wanaotoa thread za kutukana makanisa na wachungaji na huduma zao ni waislamu! wanakuja humu kila siku kulalamikia utapeli wa makanisa lakini ukizungumzia misikiti wanalipuka kama vifutu!na nyinyi wakristo mnapoona makanisa yanatukanwa mnakenua tu
 
asilimia kubwa wanaotoa thread za kutukana makanisa na wachungaji na huduma zao ni waislamu! wanakuja humu kila siku kulalamikia utapeli wa makanisa lakini ukizungumzia misikiti wanalipuka kama vifutu!na nyinyi wakristo mnapoona makanisa yanatukanwa mnakenua tu
wengi tunaomlalamikia huyu antichrist sio waislam, ni wakristo kabisa, hakuna muislam atamlalamikia huyu jamaa wa neema, kwasababu yeye kwanza kanisa lake hata halina watu wengi, popularity yake kubwa ni kwa njia ya tv ile ambayo yeye na mkewe wanatangaza bidhaa za grace zoazoa. majority ya wakristo wanaumia na mahubiri ya huyu jamaa. pia, hakuna maana kuwa na wakristo waliopotea, unajifanya mchungaji, nabii au apostle uwapeleke watu motoni. kuna maana gani kutetea ukristo wa mtu anayesema BIBLIA NI KITABU CHA KAWAID AKABISA. wewe upo tayari utetee dini kuliko kutetea biblia. ni walewale.
 
Angejaribu kudhiahaki kile kutabu cha wavaa kubazi siku iyo iyo pangepigwa moto nae angejikuta futi sita chini, wakristo wapole mno
 
Angejaribu kudhiahaki kile kutabu cha wavaa kubazi siku iyo iyo pangepigwa moto nae angejikuta futi sita chini, wakristo wapole mno
anahubiri kwamba BIBLIA NI KITABU CHA KAWAIDA TU, na kwamba duniani hakuna kutenda dhambi kwasababu Yesu alishachukua dhambi. ni mpinga Kristo kabisa, kuifananisha Biblia na vitabu vya shigongo. anakera sana.
 
anahubiri kwamba BIBLIA NI KITABU CHA KAWAIDA TU, na kwamba duniani hakuna kutenda dhambi kwasababu Yesu alishachukua dhambi. ni mpinga Kristo kabisa, kuifananisha Biblia na vitabu vya shigongo. anakera sana.
Mpuuzi sana kwaiyo anatumia nini kufundishia watu, mi hayo makanisa siwezi tia mguu
 
hizi ni siku za mwisho, manabii na wapotoshaji ni wengi kwelikweli.kama Yesu alisema mmepata bure, toeni bure, inakuwaje wao wanauza vipawa vya MUngu,
Leo nilikuwa naangalia hiyo channel yake hao sijui ndo praise and worship team walikuwa wanaimba
eti "Kama siyo mimi top plus ingetoka wapi
nimejawa na rehema na neema tele[emoji849][emoji849]

nikasema aloo mbona hatari hii

Halafu mdada kavaa hicho kimini uwii
 
Wengi ya hawa manabii na wachungaji huwa wana bifu zao na kuchongeana kwingi kwa sababu ya sadaka za waumini,wana vita baina yao yote hii ni sadaka za waumini wanagombania.

Unadhani kwanini mzee wa upako alikua ana msemo wa watashindana lakini hawata shinda
Mwisho walimkalisha lakini kabakia na stress anakunywa Konyagi tu kwenye fukwe 🤣🤣🤣
 
mojawapo ya kinachopotoshwa ni pale mtu anasema duniani hakuna dhambi, yani wewe fanya chochote upendacho. pia anasema BIBLIA NI KITABU CHA KAWAIDA KAMA VITABU VINGINE TU na kilikusanywa na kuitwa biblia kwa matakwa ya watu tu, na hata ukiiongezea vitu vyako sio kosa. kuna mengi. tangu nianze kumsikia huwa anahubiri kupinga biblia na ukristo, sasa ijulikane kanisa lake amesajili kama kanisa la kikristo au la, ili tujue kama ni mganga wa kienyeji akajisajili huko, asijiweke kweney wakristo sote tukahesabika kwenye kapu lake.
Kwani uongo mkuu? Si watu waliokusanya na kuamua kitabugani kiwe ndani na kipi kisiwemo? Gospel ya maria magdalena haimo, kitabu cha enoch na vitabu vingine 12 havimo.
Hayo yalikuwa maamuzi ya mkutano wa hippo mwaka 397 AD. Na wakakubaliana kuwa Mungu ndiye amewaongoza kuchagua hivyo vutabu. Kwa hiyo ni kazi ya mwanadamu
 
Mwisho walimkalisha lakini kabakia na stress anakunywa Konyagi tu kwenye fukwe 🤣🤣🤣
Mzee wa upako ana stress na ngwajima maana alikuwa anamkandia sana kuwa hawezi kushindana na serikali ila sasa anaona jamaa anaenda tu. Yanj ngwaji boy alikuwa adui yake namba moja. Mimi nimewah sali kwake miaka ya 2016/17 akawa akikuona hakufahamu anawatuma watu wakulete mbele anakuuliza we umetumwa na ngwajima wewe? Ngwajma anatuma watu waniibie waumini 🤣🤣🤣
 
Mzee wa upako ana stress na ngwajima maana alikuwa anamkandia sana kuwa hawezi kushindana na serikali ila sasa anaona jamaa anaenda tu. Yanj ngwaji boy alikuwa adui yake namba moja. Mimi nimewah sali kwake miaka ya 2016/17 akawa akikuona hakufahamu anawatuma watu wakulete mbele anakuuliza we umetumwa na ngwajima wewe? Ngwajma anatuma watu waniibie waumini 🤣🤣🤣
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Kumbe mzee wa Upako alikuwa fara hivyo.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Kumbe mzee wa Upako alikuwa fara hivyo.
Yani jamaa anaburudisha. Siku akitoka kwake kagombana na mkewe anaanza kumchana madhabahuni sema mkewe na watoto wake kasoro mmoja ndiye nliwahi mwona pale. Wengine sikuwahi kuwaona hata mara 1 wanakuja kusali pale.
Na alikuwa anamkubali lowassa hadi anamkandia magu kwenye ibada. Magu akaona usinitanie siku moja akatimba pale ghafla jpili, na akasema wamchongee barabara ya kwenda kansani kwake.
Tangu siku hiyo mzee akabadili gia angani
 
Siandiki ili kupinga uanzishwaji wa makanisa, naandika jambo ambalo kama halitashughulikiwa mapema, kuna siku litaleta matatizo, tena yawezekana yakawa matatizo makubwa sana.

KANISA LA NEEMA la mume wake na grace zoazoa vipodozi, limekuwa kero, linatukana na kupotosha Biblia na amekuwa akigombana na wachungaji wote Tanzania, sema tu kwasababu hawaji hewani kuongea, ila kuna kitu kinafukuta ndani kwa ndani ambacho kinatakiwa kupewa dawa urgently.

Tanzania kuna uhuru wa kuabudu, as long as umefuata sheria na miongozo iliyowekwa. Jambo hili limekuwa limechukuliwa kama uchochoro kwa matapeli wengi kukusanya watu ili aidha kujipatia utajiri kutoka kwao, au kwa malengo yao yoyote wayajuayo kwa kigezo kwamba Serikali haitakiwi kuingilia kati.

Majority ya victims, ni wanawake na watu masikini na wasiosoma...those people who have been stricken with problems na wanaenda kwao kama njia ya kutafuta msaada, badala yake wao wanatake advatage kuwafanya kitega uchumi.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI
1. Kanisa la Kibwetele lilianza hivihivi, mwisho wa siku aliua watu zaidi ya 100 Uganda

2. Tuhakikishe Makanisa yanafunguliwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria. asiyefuata huo utaratibu, ashughulikiwe.

3. hata yale makanisa ambayo tayari yameshapewa vibali, yachunguzwe kuona kama wanacomply.

4. Viongozi wengine wa dini kwenye kamati zao wahusishwe katika kila kada. mfn. Wapentecost wanao umoja wao, waprotestant wengine wanao umoja wao, katholic etc, kama mtu hayupo kwenye aina hizo zote za Makanisa, basi aeleze yeye kanisa lake ni la aina gani ili asije kuleta migogoro isiyo ya lazima.

5. Kuna uzembe na rushwa nyingi sana zinafanyika kwenye ofisi ya usajili wa haya makanisa. mfn. haiji kichwani Nabii Suguye, amekuwa na kanisa miaka kadhaa yote hiyo, hadi ameanza kuomba nywele za utosini, kucha kidole kidogo n.k ilikuwa bado kidogo aagize walete nywele za sehemu za siri manake alishaanza kufundisha namna ya kufanya ngono madhabahuni. hapo ndio wakashtuka, muda wote huo kumbe kanisa lake halikuwa na usajili. INAKUWAJE MIAKA YOTE HIYO MTU ANAOPERATE KANISA BILA USAJILI?

6. kuna kanisa moja linaitwa KANISA LA NEEMA, ni la mzee wa Neema. huyu ni mme wake yule grace zoazoa anayetengeneza sabuni na vipodozi bila kuwa na elimu yeyote ya kemikali. Wakristo karibia wote Tanzania wamekuwa wakimlalamikia huyu mtu kwasababu mahubiri yake yote, ni kupindua Biblia hadi haijulikani kama yeye ni Mkristo au wa dini gani. amefungua pia tv, na anayo night club kama kanisa. ni wazi yeye anasema sio mpentecost, sio mkatoliki, sio wa dhehemu lolote, SASA HATUJUI AMEJISAJILI KWENU KAMA NANI. mtu huyu anakwaza ukristo, ana potosha mengi ambayo tunaogopa kuna siku isijetokea watu wasio na Mungu moyoni wakamdhuru, na pia anakosesha sana amani katikati ya watu kwasababu ya mafundisho yake. tunaomba chunguzwe ili kuona kama ana elimu yeyote ya dini, ametumwa na nani manake hadi anamiliki television ya TOP PLUS anagarimia vipi n.k. ni ushauri tu.

7. Tunaomba Serikali pamoja na kuwapa vibali/usajili, iwaangalie kwa jicho la karibu hao mitume na manabii wa kisasa, hao wanaouza mafuta, maji nk. wanafanya biashara kama biashara zingine tu kwa Jina la dini. iangalie usajili wao, hao kina mwamposa, ngurumo ya upako wanaogawa pesa hata hazijulikani zinatoka wapi, mzee wa upako na wengine wengi. HIVI KWELI HAWA WAMESAJILIWA?

8. kama Nabii Suguye, mzee wa ibada za nywele na kucha, amefungiwa kanisa hadi arekebishe usajili wake, ni kwali kwamba hao mitume wengine ambao ni contraversual wamesajili makanisa yao? au kwasababu wana pesa kama kina mwamposa?.

9. kama suguye aliexist miaka yote hiyo, tunajuaje kama hawapo wengine ambao anaamka tu asubuhi anaanzisha kanisa na kukusanya hela kwa maskini? bila hata kupitia serikalini.

Mambo haya nimeandika wengine wanaweza kufikiri nina bifu nao, sina, ila ni alart tu kwa serikali, isijekuja kushtuka shuka kukiwa kumekucha.

Wasalaam!
Kitunda Dar, pia Kuna kanisa moja la mtu anayejiita Nabii Uswege, nalo lichunguzwe, lina mambo ya ovyo, wanawake wakiingia kwake wanakuwa kama mazombie, hawajali hata Familia zao
 
Utapeli upo kila kona hata huko unako sali kuna utapeli pia,achakuteseka na watu mind your our business.

Waumini wakianza kuyakimbia makanisa yenu yaliyopoa kiroho na kwenda kwenye makanisa yenye upako sadaka zenu zina pungua na kuanzisha bifu. Hizo conflict of interest baina yenu pambaneni nazo wenyewe.
Kanisa gani lililopoa kiroho?
 
Mzee wa upako ana stress na ngwajima maana alikuwa anamkandia sana kuwa hawezi kushindana na serikali ila sasa anaona jamaa anaenda tu. Yanj ngwaji boy alikuwa adui yake namba moja. Mimi nimewah sali kwake miaka ya 2016/17 akawa akikuona hakufahamu anawatuma watu wakulete mbele anakuuliza we umetumwa na ngwajima wewe? Ngwajma anatuma watu waniibie waumini [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]heee!! Ila me ananifurahisha(ga) akiwa anaimba ataimba hiyo amba yawe mpaka mwisho[emoji23][emoji23]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]heee!! Ila me ananifurahisha(ga) akiwa anaimba ataimba hiyo amba yawe mpaka mwisho[emoji23][emoji23]
Napenda nyimbo zake amba yawe, na mungu yupo na sayuni.
Nilinunua cd pale kwake nikaipoteza mwaka jana nikarudi nunua tena.
 
Back
Top Bottom