Usajili wa Wahandisi ERB waendelea kukwama kisa bodi iliyopo imemaliza muda wake. Rais tunaomba uteue Mwenyekiti mpya wa Bodi

Usajili wa Wahandisi ERB waendelea kukwama kisa bodi iliyopo imemaliza muda wake. Rais tunaomba uteue Mwenyekiti mpya wa Bodi

BrownRange

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2020
Posts
927
Reaction score
1,191
Wakuu poleni na majukumu.

Kuna ndugu yangu ameomba kufanya Usajili wa kuwa mhandisi. Amewasilisha report zake katika bodi ya maengineer yaani ERB. Kila akiulizia Usajili umefikia wapi, anaambiwa bodi ya ERB iliyopo imemaliza muda wake.

Ombi kwa RAIS, tunaomba uteue mwenyekiti mpya wa bodi, na wajumbe wachaguliwe, ili vijana wasajiliwe kuwa wahandisi.

Nawasilisha
 
Hii nchi ni ya kijinga sn, pamoja na usajili kutokufanyika kuna shughuli gani imekwama?
 
Na rais nae anapochelewa kuchagua mwenyekiti na ndio tanzania tutakuwa na upungufu wa ma- engineer.............ila Tanzania katiba yetu imempendelea sana kimadaraka rais
 
Akiwa waziri, ni wajibu wake kuteua
ndiyo sababu hata wanasiasa wa darasa la saba wanawadharau wataalamu wa nchi hii. kwa nini kusiwepo mfumo maalum kama ilivyo Tanzania Law Society ambao wanachaguana wao wenyewe?
 
Daaa.. Nilikuwa kwenye prrocess ya kuwa proffesional... Sasa naona ntakwama tena kwa mwaka huu
 
Ukiwaambia katiba mpya wanakuona useless... imagine vitu serious kama hivi watu wanamsubiri mtu mmoja mwenye files 15K mezani kwake.

Nchi ya hovyo sana hii.
 
Back
Top Bottom