Kutokana na ongezeko kubwa la vyombo vya moto, vyombo vya usafirishaji na mitambo mbalimbali inayotumia barabara, ipo sababu ya mitaala na miongozo ya ufundishaji au utoaji mafunzo yoyote nchini kujumuisha mada ya usalama barabarani ili kupanua wigo katika uelewa wa matumizi sahihi ya barabara ndani na nje ya nchi ili kupunguza na kuondoa ajali zitokanazo na uzembe wa madereva, waendesha mitambo barabarani na watembea kwa miguu (pamoja na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo wanyama)