Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama kuna mali, weka ata wawili kwa bajeti ya laki 3 kwa mweziMgambo hatoshi hasa kama ni eneo kubwa
Madirisha na milango ya chuma na nondo ni umaskini na mazoea. Mimi siyo mpenzi kabisaaa wa aina hiyo ya ujenzi.Nyumba nyingi zinazodhaniwa kuwa zipo salama ndio hazipo salama hii ni kwasababu watu wengi wame focus kwenye kuzuia mhalifu kuingia ndani ila wamesahau kuhusu hatari ikitokea ndani na ukawa unataka kutoka nje.
Unakuta nyumba ina ukuta mrefu, juu waya za umeme au seng'enge huku madirisha ni nondo hata kichwa hakipiti, unakuta hadi milango ni chuma paa limeziba kila kona hakuna hata kunapopumulia kamamoto ukiwakandani moshi utoke nje.
Huu sio ulinzi bali ni balaa kubwa sana.
Tunashika kwa mikono kabisauliwahi kushika hizo nyaya au huo umeme?
Kwa lugha rahisi ni kuwa umeme wa AC utakutetemesha. Ila DC utakurusha/kukukausha....
Usijaribu kushika umeme wa DC wenye current kubwa utakauka kama mgomba.
Usifanye mchezo na ule Umeme. Wezi walikuja kwangu wakajaribu kukata nyaya. Na kuvaa kwao gloves za plastic walipigwa na Umeme tukawakuta wamelala flatJe, ukiweka hizo nyaya za ulinzi za umeme bila kuweka cameras, wahalifu wanaweza kata hizo nyaya na kuingia ndani kirahisi?
Ninachopendelea technology haina hisia wala haiangalii sura ya mtu katika kufanya maamuzi. Mimi ndiyo maana naikubali sana internet.Kama kuna mali, weka ata wawili kwa bajeti ya laki 3 kwa mwezi
Hii ni kudhibiti vibaka wasumbufu. Ila watu wakiamua wanapitia getiniUnaingia getini wahuni wanaingia nyuma yako kabla geti halijafungwa.
Na hawajali alarm ya wala king'ora wala kelele.Hii ni kudhibiti vibaka wasumbufu. Ila watu wakiamua wanapitia getini
Hii ni kudhibiti vibaka wasumbufu. Ila watu wakiamua wanapitia getini
Mageti nayo yanahitaji kuyawekea vizingiti vyake ikiwemo uimara na utaratibu mzuri wa uingiaji na utokaji. Hapa umuhimu wa cameras na Mlinzi mwenye silaha ndiyo unapoingia.Na hawajali alarm ya wala king'ora wala kelele.
Kitu pekee kitakachowabadilisha mawazo ni mlio wa kilipuzi
Kuna Mbwinu Kiboko Ya Mbwa Sitoiweka Hapa Kwa Usalama Wa Wafuga Mbwa.MBWA, MBWA, MBWA.
Moja ya kumi.Kuna Mbwinu Kiboko Ya Mbwa Sitoiweka Hapa Kwa Usalama Wa Wafuga Mbwa.
Hata Awe Mbwa Wa Nani Au Wa Nini Kikubwa Awe Mbwa.Kuna Mtu Mmoja Aliwahi Kuweka Dau La Laki Moja Kwa Mtu Atakae Weza Kwenda Kumfunga Kamba Mbwa Wake Ndani Ya Banda Mwenyewe Alijiamini Kwamba Mbwa Wake Ana Mafunzo Na Mkali.
Kilichotokea Kuna Mwamba Akaichukua Laki Mapema Sana Kabla Ya Misa Ya KwanzA.
Paka hawakujua?Kuna jirani yangu kwake kuna paka walikua na tabia ya kuruka kuingia ndani kwake sasa hawakujua kuwa kuwa jirani kaweka kitu cha moto.... kuna siku tumesikia tuu nyuuuuuuuuuuu.....paaaaaaa
Kwishney....
Walizoea kupita hapo juu ya fance..... maybe alipita b4 haijawashwa...so wakati anarudi zake ndo akapata dhahma...Paka hawakujua?
inamaana mkuu ukiwa umewasha umeme haifai hata kushika geti lako maana naonaga nyaya zimepita hadi juu ya geti kubwa au hazinaga madhara sehemu hiyo.? na vp kama utazipiga piga nyaya hizo kwa fimbo au mti ama jiwe nako itapiga shoti si unajua watoto watukutu wa mtaa kupenda kujaribu jaribu.Yaan ukikosea hata wewe mwenyewe zinakuadhibu vibaya sana halafu zina umeme mkali hatari sana ule umeme unaobabua haufai kabisa
kweli mkuu sio poa maana watu wenye visa na ww wakitaka kukuchonganisha na majirani wanatafita jiti au jiwe anarushia kupiga nyaya basi mikelele mtaa mzima..lakini mkuu hio alarm inalia dakika ngapi au itapiga kelele tu mpaka itakapozimwa.? kwani hio electric fence lazima ipige alarm au ini uamuzi wako tu wakati wa kuset mfumo ipige au isipige alarm yaani ifungwe tu bila hayo makelele..maana kule kumchapa mtu shoti inatosha mbona hiyo alarm ya kazi gani zaidi ya kero kwa wengine.!Ile mikelele sio poa dah km kuna zimamoto wanawahi sehemu sasa piga picha ile mikelele ya fire wanawahi kuzima moto ndio inalia nyumbani kwa mtu usiku mwingi majirani wote lazima waamke